Benki Kubwa kupunguza riba na kutoa masharti nafuu kwa ujenzi wa nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benki Kubwa kupunguza riba na kutoa masharti nafuu kwa ujenzi wa nyumba

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MPadmire, Jan 3, 2011.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Shirikisho la Mashirika na vyama vinavyotetea masuala ya Makazi Tanzania (HAFOTA) wamesema wanaandaa mpango wa kuzibana benki kubwa kupunguza riba na kuongeza muda wa marejesho mpaka miaka 15.

  Kwa mfano kama ukikopa Million 60, utalipa kama elfu 40 kwa mwezi. Hivyo basi, kila mtanzania ataweza kujenga nyumba bora.

  Nawashauri hao Hafota waanzishe Petition, wapate Signature za watu wengi na hiyo itakuwa msukumo mkubwa sana. Kila atakaesaini aseme analipwa mshahara shs ngapi kwa mwezi na ataweza kurejesha kiasi gani kwa mwezi.

  Wadau, toeni maoni Na kama mna mawasiliano na hao Hafota tafadhali wasilisha.
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hizo fweza Benki itazipata wapi?
  Petition bila kuwa na economical/commmercial calculations za kujustify hizo demands ni kazi bure.
  Vinginevyo ni rahisi hao HAFOTA WAANZISHE benki yao ya mikopo nafuu, kitu ambacho wanaruhusiwa kisheria.
  Hapo tutawaelewa.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mpango mzuri,lakina mazingira yetu yamejaa siasa! It is credible only when it's done!
   
 4. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Bwana Lole Gwakisa, ni kweli hujui benki zinatoa wapi Fweza???!!!

  Jibu ni rahisi.. watu wanahifadhi hela zao huko benki.

  Kwani benki inajiendeshaje kwa mfano kupata faida ya kuwalipa wafanyakazi,kulipia bili za umeme na simu???

  Watu wanahifadhi pesa, wanalipwa riba kama 5% kwa mwaka halafu benki inakopesha kwa riba ya labda 10%. Hapo benki imepata faida ya riba 5%.

  Swala ni kukopesa sio kugawa pesa. Kwa mfano mfanyakazi akikopeshwa, kila mwezi lazima apeleke kama elfu 50 kulingana na makubaliano.

  Benking ni mzunguko wa pesa "money circulation"

  hivyo kama benki ikikopesha watu wengi kwa riba ndogo inaweza kupata faida kubwa kuliko kukopesha watu wachache kwa riba kubwa, umeelewa hapo.
   
 5. C

  Chagula Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza ningependa kujua ni akina nani wanaoongoza hilo shirika la HAFOTA? Isije ikawa ni baadhi ya watoto wa wakubwa na vibaraka wao wahindi wanataka kujifaidisha? kama ni kweli watatoa mikopo nafuu kwa wanachi wenye uwezo wa kulipa sh. 40.000 kwa mwezi ni vizuri. Lingine ambali lingekuwa la maana ni kuimarisha mashirika ya ujenzi wa nyumba, yajenge nyumba bora na za nafuu, sio nyumba za gharama na za hali ya anasa kiasi kwamba kaka karani hawezi kuinunua hata akope kwa miaka 100.

  Tanzania ianzishe mashirika mengi ya ujenzi wa nyumba za kuishi za size mbalimbali na bei mbalimbali, then watu wanaenda benki kukopa kununua hizo nyumba. Benki isiwe ya mtu binafsi kama akina BM, iwe ni benki ya taifa au ya wananchi, sio ya mafisadi.
   
 6. C

  Chagula Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli Gad hapa umetambua mazingira ya Tanzania. Asante
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mpadmire,
  Nadhani unaongelea masuala ya banking kwa kutilia maanani money circulation na si long term investment kama mbavyo mwanzoni uliligusia.
  Mimi si mtaalam wa benki lakini kwa uzoefu mdago nilio nao najua kwamba
  -Watanzania wengi si wawekaji wa amana katika benki kwa muda mrefu.
  -wanopitisha hela zao za mishahara benki huzitoa ZOTE bila kubakisha
  -benki zetu zinatoa riba NDOGO sanakulinganisha na inflation, hivyo kutovutia uwekaji wa amana.

  Hivyo basi kutokana na benki nyingi kukosa UBAVU wa kukopesha LEO na ulipe taratibu kwa miaka 15, benki nyingi haziko tayari kukopesha kwa mtindo wa long term loans.
  Hapa bado hatujaongelea RISK ya kibiashara, ya kukopa leo na kulipa katika muda wa miaka kama 15.
  Kimsingi benki zetu zina fanya biashara ya kimachinga, biashara ya kupata faida leo leo.

  Ili kujiondoa katika tatizo hili ni lazima benki zetu kwa kudhaminiwa na Serikali , zipate mkopo mkubwa toka mabenki makubwa ya uwekezaji.
  Mbenki hayo yapo, ni serious ness ya wakuu wetu tu.
   
 8. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 630
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 180
  40,000x12x15=7,200,000 ~60,000,000!? Mkuu mbona sijalielewa hilo hesabu la 40,000 kwa mwezi. Fafanua tafadhalli.
   
 9. M

  Mlimilavangi Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Afadhali Realtor umeelewa kwanza tatizo la kimahesabu kwamba 40,000 x 12 x15 =7,200,000, ivo kama ni kulipa hilo deni na faida kiduchu, basi itakuwa at least 400,000 x 12 x 15 =72,000,000 kwa mkopo wa mill. 60. Watanzania walio wengi hawawezi kukopeshwa pesa ya kujenga nyumba kwa hapa mjini......labda pembeni ya mji.....kama kibaha au kisarawe.....na maeneo mengine...ambako Mill 15 kwa mfano inatosha kujenga nyumba nzuri...halafu makato yasizidi TZS 100,000 kwa mwezi...bado nayo ni tatizo kubwa tu kwa wafanyakazi wengi wa Tanzania.
  Kwahio ni serikali kupima maeneo ya pembeni na kujitahidi kuweka karibu baadhi ya miundo mbinu kama barabara.
   
 10. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  hizi banki zetu bado ni wavivu mbona benki zenye mitaji midogo kama azania na cba zinatoa mikopo ya nyumba.

  azania
  ukikopa 20m unalipa 323,000 kila mwezi for 10 yrs = 38.76m faida kwa benki 18.76m
  ukikopa 30m unalipa 484,000 kila mwezi for 10 yrs = 58.08m faida kwa benki 28.08m
  ukikopa 40m unalipa 645,000 kila mwezi for 10 yrs = 77.4m faida kwa benki 37.4m
  ukikopa 50m unalipa 807,000 kila mwezi for 10 yrs = 96.84m faida kwa benki 46.84m

  kwa hiyo gwakisa utaona faida bado ni kubwa sana mabenki yatapata hata ukiangalia ulaya mabenki mengi yanaendeshwa na mortagage
   
 11. I

  ISIMAN Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sina hakika na mpango huu ktk kufanikiwa kwako ktk msitu mnene wa wanasiasa labda wafe
   
 12. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  hapa ni majadiliano sio majawabu. So tuendelee kuweka mazingira ya kuwezekana

  OK, hapo kuna tatizo la mishahara.

  Ila pembeni ya mji kiwanja ni kama laki moja kihalali maana Halimashauri itapima viwanja na kugawa. Sio mambo ya kununua. Pia Rasilimali za ujenzi kama cementi na bati zinapunguzwa bei. Kwa biyo wafanyakazi wanaweza kujenga nyumba bora kwa milioni 5 au zaidi

  Na pia serikali itoe dhamana kwa benki.

  Inawezekana watanzania kuishi nyumba bora.
   
 13. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nataka kuanzisha thread ya namna benki zetu zinavyofaidi lakini nikakutana na hii.
  Nilikuwa napitia website ya CRDB hasa nikiwa interested na investors information. Bahati mbaya nikakutana na info hii;
  Key financial Results As of June 2010.
  The total assets of the Bank grew by 35% from Tshs 1,645 billion at the end of June 2009 to Tshs 2,221 billion at the end of June 2010. Deposits grew by 38% from Tshs1,389 billion at the end of 2009 to reach Tshs 1,916 billion at the end of June 2010. The Bank achieved a pre-tax profit of Tshs 38 billion marking an increase of 52% from Tshs 25 billion released in year 2009. After tax profit was Tshs 28 billion being 52% higher than the Tshs 19 billion at the end of June 2009.
  Yaani these banks are ripping of Tanzanians. Faida ni kubwa mno. Wanawakamua saana wananchi hata ukiondoa effect za exchange rates na pia ukaccount kwa inflation, kwakweli kuna haja ya kulijadili hili katia ya serikali na wenye mabenki. Where in the world you can get a pre-tax profit of 52%. Aidha regulators wao wanahitaji kulizungumza hili na nina amini linazungumzika.
   
 14. M

  Mlimilavangi Member

  #14
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo nikuwa watu wengi wanadanganyika sana na neno profit, ambalo lina vitu vingi ndani yake, we nenda kaangalie Cash waliyokuwa nayo hao CRDB na sio profit sijui nini, sisi watu wa finance hiyo huwa sio ishu sana, tunataka kujua cashfloe yso ikoje......kwa mdanganyika usije ingizwa mjini kiurahisi ivo....eti wanapesa sana. Ishu yakujenga nyumba kwa mkopo inawezekana, ingawaje mabenki nayo yanakwabwa sana na regulator....na naomba kwenye ishu ya banking usitolee mfano sana eti mbona europe na marekani sijui nini....hao ndio walichemka na ishu ya Mortgage finance, ndio ikaleta kitu kinachoitwa GFC, au global financial crisis.
   
 15. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Mbona faida kubwa sana? yani ni kama BAYPORT na zile SACCOS za mtaani!
   
 16. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  kadri unavyokaaa na hela yao kwa mmuda mrefu... riba ndo inaongezeka...!!
   
 17. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kweli riba inatisha kwa mabenki mengi tanzania
   
 18. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,636
  Likes Received: 1,417
  Trophy Points: 280
  mabenki nchi hii yapo yapo tu yani nika ma hela za kutunza na kuchukua hela tu mteja hafaidiki na chochote
   
 19. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na hii mikopo itatolewa kwa wenye security au ajira za uhakika. kwa watu ambao wamekaa kimachinga sijui utamwambiaje banker kwamba unamudu kurudisha kwa miaka 10 ijayo!!! nieleweshwe kidogo hapa
   
Loading...