Benki inaruhusiwa kupeleleza eneo lako la kazi unapoomba mkopo?

Sep 27, 2019
17
7
Habari wanajukwaa samahani naomba mbisaidie kuna ndugu yangu alienda kuomba mkopo Bank akapeleka nyaraka zake za kazini, yaani mkataba wa ajira pamoja na salary slips.

Sasa Bank ikaanza kumpeleleza katika eneo la kazi kitendo kilichopelekea kugundulika kwa wafanyakazi wenzake kuwa anataka kuchukua mkopo.

Je hii ni sawa mimi naona kama sio sawa maana ni kama Bank imevujisha taarifa za mteja wake au nyie mnaonaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bank kufuatilia ajira yako ni SAWA ili waingie mkataba na mwajiri wako nawe anakata moja kwa moja kwenye mshahara wako. Kwani hata kazini (Boss au wafanyakazi wenzako) wakijua kuna tatizo gani?
Bank ipo sahihi, maana wengi weshajaza mikopo kwa taarifa feki za kazi
Habari wanajukwaa samahani naomba mbisaidie kuna ndugu yangu alienda kuomba mkopo Bank akapeleka nyaraka zake za kazini yani mkataba wa ajira pamoja na salary slips sasa Bank ikaanza kumpeleleza katika eneo la kazi kitendo kilichopelekea kugundulika kwa wafanyakazi wenzake kuwa anataka kuchukua mkopo je hii ni sawa mimi naona kama sio sawa maana ni kama Bank imevujisha taarifa za mteja wake au nyie mnaonaje

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maana teyali mshahara unapita kwenye Bank yao it means wao watakata huko huko haina haja tena ya kusambaza hizi taarifa za mteja
Kuna ofisi nyingine zinatoa mokopo kwa wafanyakazi wake na wanapenda waone wafanyakazi wanachukua mikopo ofisini hapo sas huoni kama kuna kizuizi anaweza akapata huyu mtu katika kuchukua mkopo??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maana teyali mshahara unapita kwenye Bank yao it means wao watakata huko huko haina haja tena ya kusambaza hizi taarifa za mteja
Kuna ofisi nyingine zinatoa mokopo kwa wafanyakazi wake na wanapenda waone wafanyakazi wanachukua mikopo ofisini hapo sas huoni kama kuna kizuizi anaweza akapata huyu mtu katika kuchukua mkopo??

Sent using Jamii Forums mobile app


naomba nichangie kidogo kwa ufahamu wangu kuhusu salary loan huwa inakuwa hivi lazima kuwe na makubaliano ya kimtaba kati ya bank husika na kampuni yani kampuni iwe kama mzamini unaweza ukakuta mishahara yenu inapitia NBC ila kampuni yenu haina makubaliano ya kimtaba ya kuwakopesha wafanyakazi wa kampuni yenu ilo la kwanza na kwa hali hii mara nyingi kampuni kubwa huwa zinakopesha wafanyakazi wake wao wenyewe bila kutegemea bank na huwa inakuwa bila riba na inakuwa ni mara 3 ya gross salary sasa ukionekana unataka kukopa bank na wao wanatoa mkopo iyo ni changamoto na pia kwa mujibu wa salary loan hakuna njia ambayo utafanya ukakopa na muajiri wako asijue au kusiwe na makubaliano ya kimtaba kati ya bank yako na kampuni

ila kama anafanya kazi serikalini inakuwa taratibu zake ni tofauti kidogo
 
Benki ni lazima iwasiliane na mwajiri wako, kumweleza kuhusu adhimio la mfanyakazi kuomba mkopo.

Ili mwajiri ahakikishe kwamba ataendelea kulipa mshahara kupitia hiyo benki.

Na wakati mwingine ni wao kutaka kujiridhisha kwamba una mkataba endelevu hapo kazini kwako.

Imagine, ukichukua mkopo kimya kimya halafu kumbe umeshatoa barua ya ku-resign, au ukamwambia mwajiri akubadilishie benki.
 
Back
Top Bottom