Rais bora wa TZ next to Mwl. J. Nyerere
Aliingia madarakani kwa haki bila rushwa wala kununua vyombo vya habari. Alikuwa na hoja na alieleza WAZI nia yake ya kugombea urais.
Alianza kazi kwa kasi hakungoja wiki mbili au zaidi kupanga baraza la mawaziri.
Aliunda serikali ndogo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Alikuwa na falsafa binafsi, dira na msomi aliyependa kusoma na kujifunza.
Akapambana kijemedari kwelikweli na misukosuko ya Reli, MV Bukoba, Elnino na majanga mengine. Akapunguza mfumuko wa bei toka 48% 1994 na kubakia single digit enzi zote za utawala wake.
Akaboresha utumishi wa umma; kapunguza wafanyakazi hewa na kuboresha maslahi.
Akapunguza deni la nje na kuipa Tanzania heshima.
Akajenga miundo mbinu hususan barabara kwa kasi kubwa
Akavutia wawekezaji wenye tija kama TBL, NBC n.k
Akajenga EPZ alipanga zijengwe 22 nchi nzima
Akaimarisha majeshi yetu kwa kuwapatia motisha vitendea kazi na makazi.
Akajenga Uwanja wa Taifa
Akajenga Benki kuu Twin towers na kule Zanzibar. Twin Towers kama Bank of Canada, Toronto (kwa wanaojua)
Alikuwa na hoja zenye mashiko.
Alikuwa kiongozi kweli jasiri, mwenye kujiamini na hakuogopa mihadhara: iwe ya vyama vya siasa, vyuo vikuu au kimataifa. Alikuwa full of substance.
Ujasiri wake hata vita ingetokea enzi zake angetuongoza vyema sana kumshinda adui.
Hakuwa mwongo katika kauli na ahadi zake.
Alikuwa na maadili na na hekima na aliheshimu mamlaka na taratibu zilizopo.
Akawapa nguvu na haki zaidi wanawake.
Alipigania utandawazi kuwanufaisha wengi.
Alikuwa mchapakazi hakuwa mvivu.
Alikuwa makini na alipinga na kukwepa sana matumizi yasiyo lazima ya serikali.
Alisafiri ngambo pale tu ilipobidi. Alikaa ofisini na kufanya kazi.
Alijiheshimu hakuwa Fataki.
Hakuwa ombaomba, bali alipenda kujenga uwezo, kujitegemea na kuwasaidia ombaomba.
Akanunua ndege bora ya Rais, mafisadi wakaipinga.
Akanunua rada ya nguvu, mafisadi wakaipinga.
Alikuwa na vyeti vya nguvu na alifuzu vyema masomo yake. Alionyesha uwezo. Alikuwa na speech za kisomi.
Alihakikisha nchi inakaribia kupaa ndio akaikabidhi kwa JK. Tukadhani itapaa.
Na mengine mengi.
Huyo ndiye Benjamin William Mkapa, Rais ninayemkubali na kumrank second. Angekuwepo mpaka leo Tanzania ingekuwa emerging economy I am sure.
Mnaomsema vibaya mshindwe ka kulegea. Hamna shukrani. Ni kiongozi ambaye wanaokumbuka, tunamshukuru sana.
Ben Mkapa,
Alimkabidi mkewe mama Mkapa aka first lady funguo za ikulu yetu akawaenzi akina Maro, akutuibia kwa kutumia mifuko ya kiserilikali, akawapa nduguze tender za kiwizi, akajenga majumba ya kifahari kwa kodi zetu.
Jamani WanaJF, Hivi wakati ule walitoa watu walikuwa wanamsifu Mkapa kuwa Kiongozi safi mara baada ya kutoka haohao wanaanza kusema kuwa alikuwa Mla Rushwa mkubwa?? Najua hata Mzee mzima wa Kaya JK atakapotoka Madarakani watakuja kusema alikuwa mla rushwa kwasababu serikali katika kipindi hicho iliangushwa na ufisadi wa Richmond, Sisi tunataka watoke sasa na sio Kesho. tuache kuwa Wanafiki kiasi hicho katika siasa zetu
Mkapa alikuwa Hodari na Kiongozi makini hata kuliko mzee mzima wa kaya Jk, huwezi kumfananisha na Jk hata kidogo, kama angekuwa Jk ndio mkapa kipindi kile basi sisi Watanzania tungeelekea KUzimu maana MKapa alikuwa na moyo japo haya madudu yote kwasababu ya mfumo wetu ulikuwa corrupt hasa katiba, lakini Mkapa alikuwa kiongozi mzuri.Labda hii ndio janja ya Mzee mzima wa kaya kwa kufanya watu waseme Ben ni mbaya na kuona yeye ni safiWengi wetu tuna mtupia Mkapa lawama nyingi mno,ni kweli amefanya mengi mazuri sana ya kukumbukwa,na amefanya mengi ambayo sasa ndio tunaona hadhari zake.kwangu binafsi naona Mkapa ni rais ambae ametutoa kwenye hali mbaya ya umaskini na kutufikisha hapa tulipo sasa.Mkapa uwezi kumlinganisha na JK.Jamani tusiwe wachoyo wa fadhila,tuangalie ni uhuzo alioufanya mkapa kwenye kipindi chake cha miaka kumi,na tuangalie uhozo uliofanyika kwa kipindi cha miaka 4 ya JK.Hapo ndipo utakapo pata jibu sahihi.
Pamoja na matatizo yote ya Mkapa, kuna mtu anaweza kutupa walau mambo 10 tu ambayo rais wetu mpendwa JK amelifanyia taifa hili tunapoelekea kufikisha mwaka wa tano?
Binafsi nasema JK is a failure compared to Mkapa. Hata kina Mpendazoe ambao Phillemon Mikael anawakandia wanatumiwa na JK kumwandama Mkapa ili kuficha mapungufu ya JK.
Nipende au nichukie lakini binafsi sifurahishwi na utendaji wa serikali ya JK ambayo ilikuwa inatafuta namna zote za kumpunguza Magufuli lakini Mungu wa Israel na Mungu wa Yakobo bado anamsimamia mtumishi wake Pombe Magufuli.
Nipende au nichukie lakini binafsi sifurahishwi na utendaji wa serikali ya JK ambayo ilikuwa inatafuta namna zote za kumpunguza Magufuli lakini Mungu wa Israel na Mungu wa Yakobo bado anamsimamia mtumishi wake Pombe Magufuli
.Labda hii ndio janja ya Mzee mzima wa kaya kwa kufanya watu waseme Ben ni mbaya na kuona yeye ni safi
Ni kweli kabisa.. maana hata vitu vingine vya kusema kuwa Rushwa wakati yeye alikuapo huko ni kitu kibaya sana. Wanamtandao walikuwa wanavujisha siri nyingi sana za Mkapa na madudu mengine ili yamjenge Mzee Mzima wa Kaya (Jk) wakati mwingine napata shida sana kuona haya mambo na kujua kuwa Jk alikuwa makini?? Tazama hata ile kesi ya Mahalu kama naye alikuwa Waziri alikuwa wapi kushughurikia matatizo hayo??personal intelligence system ya jk ..tangu mwanzo ...ilikuwa na nia ya kuwafanya watu wawe pre occupied kumkandia mkapa muda wote ili wakose muda wa kumchambua yeye ...
na kwa hilo kiasi kafanikiwa...kidogo sasa watu wameanza kuelewa kuwa mkapa pamoja na makosa yake ..lakini he was fa a good leader....which i would say it is an insult to mkapa to compare with jk...time will tell!!..wajanja kuanzia day one jk anakuwa nominated ..tuliwaambia hapa kuwa hili bomu la nuclear...bora salim ,sumaye ,malecela au mwandosya waliogombea naye..he was worst l!!
hatimaye tumemaliza miaka mitano tunapiga umbeya kuhusu mkapa ....kwa kuchezewa akili na system fulani...sasa tunarudi kwa wapiga kura!!
Kumbe mkuu tupo pamoja sio?personal intelligence system ya jk ..tangu mwanzo ...ilikuwa na nia ya kuwafanya watu wawe pre occupied kumkandia mkapa muda wote ili wakose muda wa kumchambua yeye ...
na kwa hilo kiasi kafanikiwa...kidogo sasa watu wameanza kuelewa kuwa mkapa pamoja na makosa yake ..lakini he was fa a good leader....which i would say it is an insult to mkapa to compare with jk...time will tell!!..wajanja kuanzia day one jk anakuwa nominated ..tuliwaambia hapa kuwa hili bomu la nuclear...bora salim ,sumaye ,malecela au mwandosya waliogombea naye..he was worst l!!
hatimaye tumemaliza miaka mitano tunapiga umbeya kuhusu mkapa ....kwa kuchezewa akili na system fulani...sasa tunarudi kwa wapiga kura!!
Hahahaha... Mitizamo inapofanana tutashindwa kujadili hoja... Mi ngoja nikae kimya kwa sasa nisije nikapewa kambi ya Salim sasa hivi!hureee ...well said ..magufuli for presidency 2010!!!... mnajuwa magufuli alikuwa kwa sumaye .na alikuwa awe waziri mkuu wa sumaye...ndio maana alifungwa kweli kweli ...akapewa wizara ya ardhi ambayo ...wanaiita wizara ya kifo...akafurukuta ..., wakaunda wizara maalum ya samaki ...ambayo haina public interest ...akafurukuta...hadi juzi jk imebidi amvulie kofia[jk knows ..if you cannot fight them ..join them...].......
Kumbe mkuu tupo pamoja sio?
Ebana mi namkubali Magufuli sana, ila sitamani awe rais bali Waziri mkuu... Naamini kutakuwa na changes kubwa sana!
Hivi nyakati za 2005 Magufuli na Pinda walikuwa kambi ipi? Ya JK au ya Salim? Mkuu naamini wewe unaweza kunitoa tongotongo