Benjamin Mkapa on BBC HardTalk (Video)

I like it, Mh. Mkapa alivyomweka sawa kwa hoja mwandishi mzungu mpaka akalainika na ku-conduct a proper interview. Ni ndoto zangu hali hii ya kujenga hoja ikaeleweka kama Mh. Mkapa ingekuwa inapatikana ktk serikali zote za kiafrika maanake aliyepo sasa hivi Afrika ni Mh. Robert Mugabe pekee anayeweza kujenga hoja.
 
shukrani mkuu manake hii kitu nakumbuka niliisikia wakati niko high school..jamaa alinitonya eti Mkapa nusura arushe ngumi kwenye hardtalk kiwanja!Sikuwahi kuiona kwa macho yangu siku zote hizo.

Ebwana hii niliiona live BBC wakati huo ndio namaliza form 6. Mkapa yuko Nondo sana kulingalisha na vibwetere wengine wako madarakani. Anaongea kiingereza fasaha na anaongea vitu vinavyoelewaka hata kama ndani yake kutakuwa na uongo.

Ebu imagine anangebananishwa president wetu wa sasa hali ingekuwaje?. Maana yeye lazima awe na vi notice kibao mkononi wakati wa kujieleza. Nafikiri Nyerere anaona mbali sana ndio maana akampendezeka jamaa ile 1995, hakumpendekeza huyu jamaa burebure nafiriki aliona anakitu fulani kichwani. He didnt do a lot wakati wa uongozi wake lakini at least anatoa maelezo yanayotia moyo kuliko wazee wa kufunga mkanda daily.....
 
Mkapa ni kifaaa..Uwezo wake binafsi kiakilii ni ngao tosha katika kujiamini kwake.

Uongozii wake bado utaendeleaa kubakia alama ya msingi wa maendeleo ya taifa hilii.
 
Mkapa ni kifaaa..Uwezo wake binafsi kiakilii ni ngao tosha katika kujiamini kwake.

Uongozii wake bado utaendeleaa kubakia alama ya msingi wa maendeleo ya taifa hilii.

Kumbuka ana uwezo lakini akautumia kulisaliti taifa! Mkapa ni rais aliyekosa uzalendo kuliko wote. Kumbuka wajibu rais ini kuifanyia kazi nchi yake, kila alichofanya chema alitimiza wajibu wake, hakutakiwa kufanya uovu. Niyachukiayo kwa Ben Mkapa:

1. Alimhadaa Nyerere kwamba yeye ni Mr. Clean, mzee wa watu akazunguka nchi nzima kumnadi, kumbe anaamsha aliyelala! Awamu yake ya pili akafanya kufuru ya ufisadi.
2. Ni rais aliyekuwa akithamini watu wa nje kuliko watu wake. Alidiriki kuwatamkia wananchi wake nmaneno ya kejeli mara wanapokuwa na malalamiko kwenye utawala wake e.g ""Acheni wivu wa kike"-wakati akifungua mgodi wa Tulawaka.
3. Mkandamizaji wa demokrasia kwa kutumia vyombo vya dola. mfano. mauaji ya Zanzibar, alidiriki hata kuwapongeza polisi walio ua waandamanaji! Pia alilikandamiza bunge pindi kunapokuwa na hot issues, anaitisha kikao cha wabunge wa CCM na kuwatisha ili kuzima issue.

Wandugu, tunao wajibu wa kulifanyia taifa mazuri si na mabaya pia. Mkapa was too arrogant to be a president....my opinion......kwani hata 1995 nilikuwa najua hilo nasikuthubutu kumuunga mkono...kimsingi arrogance yake niliwahi kuishudia laivu akiwa waziri wa sayansi teknologia naelimu ya juu. Hakuwa na muda wa kuongea na wanafunzi, regardless ya shida yenu.Mkiandamana ni mkongóto tu. Pure mmakonde!
 
Ebwana hii niliiona live BBC wakati huo ndio namaliza form 6. Mkapa yuko Nondo sana kulingalisha na vibwetere wengine wako madarakani. Anaongea kiingereza fasaha na anaongea vitu vinavyoelewaka hata kama ndani yake kutakuwa na uongo.

Ebu imagine anangebananishwa president wetu wa sasa hali ingekuwaje?. Maana yeye lazima awe na vi notice kibao mkononi wakati wa kujieleza. Nafikiri Nyerere anaona mbali sana ndio maana akampendezeka jamaa ile 1995, hakumpendekeza huyu jamaa burebure nafiriki aliona anakitu fulani kichwani. He didnt do a lot wakati wa uongozi wake lakini at least anatoa maelezo yanayotia moyo kuliko wazee wa kufunga mkanda daily.....
Unaona heri hakufanya ki2 lakini ana uwezo mkubwa wa kujieleza?? damn!! kwa hiyo uko radhi kudanganywa iwapo tu huyo anayekudanganya atapangilia uongo wake vizuri.
binafsi niko tayari kuongozwa na BUBU (asiyeweza kuongea kabisaaaa) kama tu hatauza utu na rasilimali zetu.katika mambo ambayo mwalimu NYERERE aliyajutia katika uhai wake,basi ni kumpigania MKAPA kuingia madarakani mwaka 1995...(the superfailure in his political carrier) LOL
 
Kwanza Mkapa professionally ni mtu wa media, na amekuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka kadhaa kama sikosei.

Vile vile anao uwezo mkubwa wa kujieleza na hicho ni kipaji sio kila mtu anacho.
 
Kwanza Mkapa professionally ni mtu wa media, na amekuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka kadhaa kama sikosei.

Vile vile anao uwezo mkubwa wa kujieleza na hicho ni kipaji sio kila mtu anacho.

Na kikwete amekuwa waziri ya mambo ya nje kwa muda gani?
 
Watanzania tunapenda mbwembwe sana , yaani mtu ameuza migodi kwa bei ya kutupa, ameuza nyumba za serikali , amejiuzia mgodi , amelitia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi na binafsishwaji feki leo mnamsifia. The question that ought to be asked is what have we, as a country, gained from his eloquence? In his tenure, the guy was good at talk the talk and not at walk the walk. It is really sad that we are even wasting our precious time trying to dissect what this clown said.
 
Wakuu hapa tuzungumzie uwezo wa kujieleza wa viongozi wetu na siyo Mkapa alifanya nini,manake uongozi wa Mkapa na mapungufu yake yameshajadiliwa sana na threads zake zipo hapa.Hata kama uwezo wa kujieleza siyo kigezo cha uongozi bora lakini ni bora uwe na mtu walau hata akikuwakilisha mahali unauhakika kuwa atafanya vizuri na siyo kusindikiza.
Tutofautishe:Unaweza ukawa muongeaji sana lakini usiwe muongeaji mzuri/ukawa unaongea pumba tu.Mkapa siyo muongeaji sana,bali ana uwezo wa kujieleza,ana uwezo wa kujenga hoja vizuri na kukufanya uamini kuwa anajua anachokiongea/kukifanya.
nway nyinyi semeni yote,pamoja na madudu yote ya Mkapa,lakini mimi leo kesho bado namkubali Mkapa walau ame fanya vitu fulani na unaweza kusema kweli nchi ilikuwa na kiongozi.Hata zile kashfa zake sawa kabisa.Wabongo ni mavivu na tunahitaji watu kama Mkapa kuongoza hata kuchapa bakora ili mradi twende mbele.Haya mambo ya kuchekeana chekeana,kuoneana huruma sijui demokrasia kwa vi nchi kama Tanzania ni kuongezea umasikini tu.
 
  • Thanks
Reactions: BMT
Mara nyingi waongeaji sana huwa ni Majizi au matapeli! Utatangazaje unapambana na rushwa wakati wewe ni mla rushwa namba moja?

unapomita mtu mwizi lazima uwe na uthibitisho....watu wengi mumejengewa chuki kumchukia na kumdharau mzee wa watu kwa vitu vya kupandikizwa...mwajitakia dhambi bure mbele za Mungu....As for me I look at him as an historical leader in this country hata kama walioko madarakani kwa sasa wanajaribu kuua jina lake....there is a lot around that will continuously speak for him hata kama yeye akinyamza.

Mkapa ni kiongozi bora hata kama alifanya makosa ni kawaida kwa mwanadamu kwani hata yeye hakua malaika....he has done a lot na hakua na muda wa maeneno mengi ya kujitakia umaarufu usioleta tija yeyote....munamchukia na kumsema vibaya labda mutuambia aliwanyima au kuwazibia mwanya gani lakini musimsingizie yasiyo kweli wala kuthibitika.
 
Duh! Sijui ulitaka akuuze wewe ndio ujue jamaa alikuwa nyangáo?. Tutamkumbuka kwa kukomaza UFISADI mchini mwetu. Jitu limeuza nchi, mnalisifia!
 
Bado Mkapa naona alikuwa kiongozi mkweli kwa tabia yake na pia naona kuwa Mkpa ndiye aliyefanya hivyo
 
Back
Top Bottom