Benjamin Mkapa alituangusha na kutuingiza kwenye sheria mbovu za uwekezaji na uchimbaji wa madini

m2020

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
979
1,353
Kwa vyovyote vile nchi yetu imetumbukia kwenye mgogoro mkubwa wa masuala ya sheria mbovu za uwekezaji na uchimbaji wa madini kwa kutokawa na kiongozi makini na madhubuti. Huyu si mwingine ambaye ndiye CHANZO cha matatizo na migogoro ambayo leo Rais wetu mpendwa Dr. John Magufuli anapambana kuitatua.

Huyu ni Ben Mkapa ambaye alikuwa rais wa tatu wa Tanzania ambaye alikuja na Sera za ubinafsishaji na uwekezaji zenye sheria mbovu kabisa.

Kwa bahati mbaya zaidi hakutaka kusikia wala kushauriwa lolote kuhusu Sera na sheria mbovu za uwekezaji na uchimbaji wa Madini.

Nampongeza Dr. Magufuli kwa hatua njema na tuko pamoja nae katika kuondoa unyonyaji huu dhalimu uliotufikisha hapa.

Mhe Mkapa ni vema ukatuomba ardhi wa Tanzania kwa madhila haya uliyoteletea katika nchi yetu.

Baadhi yetu tunasema oooh ccm ndo imetufikisha hapa. Swali ni je kwani Magufuli sio ccm ambaye sasa anachukua hatua?

Tatizo ni watu si chama.
 
Naona taratibu wa Tanzania tutafika wakati tutaongea lugha moja. CCM ni janga, wabunge wake wanaungana pamoja kupitisha mambo ya hovyo kwa kulinda chama chao bila kuangalia maslahi ya taifa, leo tunashangaa haya kama vile hatujawahi kuambiwa na wabunge wa UPINZANI!!!???
 
Hata huyu tunaambiwa alishauriwa vibaya. Siwaamini kabisa Viongozi wa CCM. Haya Majambazi yanayoendelea kulipa viinua mgongo vizito huku wakiwa wametukwapulia raslimali zetu.

Wote ni wale wale,tujiulize kwanini leo mikataba mipya ya ununuzi wa ndege inafanyika kwa siri??
 
Kwa vyovyote vile nchi yetu imetumbukia kwenye mgogoro mkubwa wa masuala ya sheria mbovu za uwekezaji na uchimbaji wa madini kwa kutokawa na kiongozi makini na madhubuti. Huyu si mwingine ambaye ndiye CHANZO cha matatizo na migogoro ambayo leo Rais wetu mpendwa Dr. John Magufuli anapambana kuitatua.

Huyu ni Ben Mkapa ambaye alikuwa rais wa tatu wa Tanzania ambaye alikuja na Sera za ubinafsishaji na uwekezaji zenye sheria mbovu kabisa.

Kwa bahati mbaya zaidi hakutaka kusikia wala kushauriwa lolote kuhusu Sera na sheria mbovu za uwekezaji na uchimbaji wa Madini.

Nampongeza Dr. Magufuli kwa hatua njema na tuko pamoja nae katika kuondoa unyonyaji huu dhalimu uliotufikisha hapa.

Mhe Mkapa ni vema ukatuomba ardhi wa Tanzania kwa madhila haya uliyoteletea katika nchi yetu.

Baadhi yetu tunasema oooh ccm ndo imetufikisha hapa. Swali ni je kwani Magufuli sio ccm ambaye sasa anachukua hatua?

Tatizo ni watu si chama.
He was right at that moment of time!!!! Sheria nyingi ziliwekwa iki kuvutia wawekezaji ambao hatukuwa nao kwa wakati huo? Now tumeoata akili/elimika ndio maana twapaza sauti.
 
Huwa nawadharau sana aina ya watu dhaifu wenye uelewa mdogo. Hivi unaposema ccm unawaacha hao chadema na CUF kwani wao hawajawahi kuwa ccm?

Waangalieni viongozi wenu wote kwenye vyama vyenu kama hawajawahi kuwa ccm halafu mjue nini cha kuandaa hapa jukwaani.

Kwa ufupi ni vema mkawalalamikia watu waliotufikisha hapa kwa majina kwani mikataba hiyo haikusainiwa na NEC ya CCM wala CC yake.

Acheni udhaifu katika kufikiri hata kama ni wewe ungekuwa na dhamana ya ubunge iwe ndani ya ccm au Chadema na kiongozi wako mkuu anaone kana kupinga dhana sahihi bdo usingeweza kwenda tofauti naye kwa maslahi yako ya kifamilia.

Mtu Aliyepewa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi yetu ni rais kama hatotimiza wa jibu wake ni lazima asemwe na abebeshwe lawama.
 
Viongozi wakuu wastaafu walisign mikataba hii kwa maslahi yao mapana. Wana kinga za kutoshitakiwa. Lakini kinga hizo ni za muda. Ipo siku safari yao hapa duniani itafika mwisho. Tutakutana huko kwa Mungu, na tutawashitaki.
 
Tusipige kelele, ifike mahala tuseme tunataka nini! Hakuna Rais hata mmoja ukiacha Kambarage alie wahi kusema Tanzania kwanza, tukifanya hivyo vyama vitakuta Sera yavTanzania kwanza. Na Rais wa Tano kwa amekuwa akilisema hili wazi wazi, Tanzania kwanza. CCM na vyama vingine baadaye
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom