Bendera za CHADEMA zimejaa barabarani Mwanza, JK afunga vioo vya gari lake

Apr 9, 2011
38
3
JK yuko MZA na muda huu kaelekea kufungua barabara inayoelekea Geita kupitia Busisi'
Ila cha ajabu ni kuwa baadhi ya bendera za CHADEMA zimezagaa sana barabarani kuashiria kuwa ni ishara ya ngome ya CHADEMA au nini??? bado sijapata jibu, na hili JK kaliona kiasi cha kumfanya afunge vioo vya gari lake la msafara lililokuwa limembeba,

Mimi nilidhani kuwa kwa kuwa tangu atoke MZA kipind cha uchaguzi hajarud hadi leo hii angeweza kuutumia mda huu kufungua vioo vya gari lake na kuwapungia wananchi mkono kwa kuwashukuru kwa kumpa kura nyingi kama walivyodai NEC lakini hajafanya hivyo, mie ni mwananchi wa jimbo la Nyamagana na kipindi cha uchaguzi alishuka kwenye magari na kuwakumbatia wananchi, ila leo sijaona hayo asubuhi hii...

Swali je,
Au kwakuwa majimbo yote ya MZA yameenda upinzani?
Au kwakuwa bendera za CHADEMA zilizagaa barabarani?
Au kwakuwa anajua kura zilichakachuliwa?
Au kwakuwa anajua alichokuwa anakitafuta kashakipata na hana haja ya kushukuru?
 
Hata kuwapungia mkono ameshindwa. Si unajuwa ni mzee wa visasi roho inauma sana.

Bora hata huo mkono angepunga hata ndani ya gari tungeona kupitia vioo lakini kwa jinsi gari lake lilivyokuwa liko kattikati kama pembe mraba harafu gari lake likiwa ndani ya magari mengine, tulichoshuhudia ni gari metaliki nyeusi ikiwa na kibendera na si vinginevyo huku ikiwa speed 180 wakati ni mjini kati.
 
plz if possible aahirishe ziara manke aweza aibika mkuu!
 
Toka lini JMK akatembea vioo wazi? Labda wakati wa kampeni. Wacha pumba.

Kwani mkuu ni sheria ipi au katiba gani inakataza JK kufungua dirisha na kusalimia wapiga kura wake? Jk ninayemfahamu mimi baada ya uchaguzi wa 2005 alitembelea karibu mikoa yote na kila alipokuta watu wengi hasa mijini aidha alisimama au alifungua dirisha kusalimia. Tukubaliane tu kwamba JK maji yamemfika shingoni - matatizo ya kuchakachua kura.
 
Jamani anaona aibu kwani alipokuwa Mwanza wakati wa kampeni 2010 aliwaongopea mchana kweupe watu wa jimbo la Nyamagana kuwa Law Masha ndiye mbunge wao kwa kupita bila kupingwa, lakini leo hii mbunge wa Nyamagana ni Wenje.Pia anaona aibu kwa kuchakachua kura.
 
Rais Kikwete ameenda kufanya nini huko wakati anajua kuwa ile ni ndome ya CHADEMA? Hali ya kufunga vioo ni ishara ya aibu. Subiri mwaka 2014 ambapo CDM watashinda Serikali zote za mitaa Kanda ya Ziwa.
 
:yield::yield::yield:
JK yuko MZA na muda huu kaelekea kufungua barabara inayoelekea Geita kupitia Busisi'
Ila cha ajabu ni kuwa baadhi ya bendera za CHADEMA zimezagaa sana barabarani kuashiria kuwa ni ishara ya ngome ya CHADEMA au nini??? bado sijapata jibu, na hili JK kaliona kiasi cha kumfanya afunge vioo vya gari lake la msafara lililokuwa limembeba,

Mimi nilidhani kuwa kwa kuwa tangu atoke MZA kipind cha uchaguzi hajarud hadi leo hii angeweza kuutumia mda huu kufungua vioo vya gari lake na kuwapungia wananchi mkono kwa kuwashukuru kwa kumpa kura nyingi kama walivyodai NEC lakini hajafanya hivyo, mie ni mwananchi wa jimbo la Nyamagana na kipindi cha uchaguzi alishuka kwenye magari na kuwakumbatia wananchi, ila leo sijaona hayo asubuhi hii...

Swali je,
Au kwakuwa majimbo yote ya MZA yameenda upinzani?
Au kwakuwa bendera za CHADEMA zilizagaa barabarani?
Au kwakuwa anajua kura zilichakachuliwa?
Au kwakuwa anajua alichokuwa anakitafuta kashakipata na hana haja ya kushukuru?
 
Raisi Jakaya asilete ubishoo bwana yeye ni kiongozi wa Nchi hawezi kuwasusia wananchi wake eti bendera za Chadema nyingi barabarani au wanampungia mkono kwa alama ya vema wote wananchi wake bwanaa
 
Back
Top Bottom