Elections 2010 Bendera za Chadema zaibwa mtaa mzima mjini Arusha !!!

Lubaluka

JF-Expert Member
May 18, 2009
496
44
Usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa makao mapya mjini Arusha, bendera na vipeperushi vyote vya Chadema vilivyokuwa vikipepea vimeibwa na watu wasiojulikana...!!! Nimepita eneo hilo leo asubuhi kwenda kazini na kushuhudia hali halisi. Pia niliongea na baadhi ya wakazi/wafanyabiasha wa mtaa huo kwa kina zaidi kulikoni, jibu likawa hilo hilo - bendera zote za Chadema zimeibwa !!!!

Kifo cha Nyani , .............. !!!!!!
 
CCM iko hoi bin taabani jimbo la Arusha mjini hasa mgombea ubunge Mama Batilda Salha Buriani hana mvuto wala uwezo wa kutawala siasa.Juzi saa nane usiku CCM mafia walianza zoezi la kubandua picha za wagombea wa upinzani CHADEMA na TLP.Usiku wa kuamkia leo zoezi hilo limeendelea mpaka kwa wagombea nafasi ya udiwani.

CCM Lowasa wanatumia kila mbinu halali na haramu kuwachagulia wakaazi wa Arusha mbunge.CCM wilaya hawana habari na Mama Buriani wameelekeza nguvu zao kwenye kampeni za madiwani na mgombea urais.Zipo taarifa kwamba Lowasa amekuwa katika harakati kubwa za kuwasaidia wabunge wengi watakao muungano katika hazma yake ya kugombea uspika.Ikumbukwe ndani ya bunge lililomaliza muda wake Lowasa hakuwa na nguvu/ushawishi kama ilivyo kwenye halmashauri kuu na kamati kuu ya CCM.Baadhi ya wagombea ubunge mkoani Arusha wanajulikana wapo kambi ya Lowasa ni Sumary Arumeru Mashariki,Medeye Arumeru Magharibi na Mama Batilda Buriani.
 
Ni aibu tupu. Huyu mama ndio anaonyesha waziwazi alivyo kilaza , mbum,bumbu na jeuri ya kijima jima. Walishamkataa na hawezi kuchaguliwa .Akajigumgue zake salama .

Taarifa isiyo rasmi inasema hata mumewe Mzanzibar kashamtosa baada ya kugundua ana mimba isiyo yake. LOH
 
Chadema hata wasingeweka bendera au vipeperushi haijalishi!!! tunachojali ni sera wala sio kuuza sura! JK kuweka mabango ya gharama kubwa kwakuuza sura yake kwani nani asiye mjua JK kuna haja gani yakutumia hela za walipa kodi kuuza sura yake! sisi tunaangalia sera za mgombea sio kutudanganya kwa kuuza sura kwenye mabango Gooo Dr. Slaa Goooo!
 
.....ana mimba???? wrong timing!!!! physiology ya pregnancy inaweza kuhimili mikikimikiki na hisia za kampeni/uchaguzi? ndio maana haishi kudeka kwa 'mamvi' ambaye anataka kuifanya nyeusi iwe nyeupe kwa mabavu!!! kama mimba si ya mumewe ni ya 'mamvi' nini maana jamaa haipiti wiki 2, yupo A-town na mamaaa!!! kama si ya 'mamvi' ni ya yule msomali wake wa Nairobi?
 
zingekua za CCM ndo zimeibiwa leo mtaa mzima ungewekwa ndani na mngeletewa ulinzi hadi wa mbwa mwitu
 
Jana eneo la sokoni kuu Arusha CHADEMA walikuwa na mpango wa kusimika bendera lakini vijana wa CCM waliwazuia jambo lililosababisha vurugu kubwa kabla ya polisi kuingilia kati kwa kurusha mabomu ya machozi.Mlingoti,mfuko mmoja wa cement na bendera vinashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi unaotegemewa kukamilika 01/11/2010.
 
hiyo ndo chichiemu inavyofanya kazi.
sasa ole wake polisi atakayetia pua yake kunusa iyo ishu. kama siyo kuwa demoted, kuhamishwa basi hana kazi.
poleni wenzetu wa arusha
 
Jana eneo la sokoni kuu Arusha CHADEMA walikuwa na mpango wa kusimika bendera lakini vijana wa CCM waliwazuia jambo lililosababisha vurugu kubwa kabla ya polisi kuingilia kati kwa kurusha mabomu ya machozi.Mlingoti,mfuko mmoja wa cement na bendera vinashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi unaotegemewa kukamilika 01/11/2010.
kwahiyo mlingoti na mfuko wa simenti vina bendera ya chama gani?? hawa polisi sasa naona wameamua kuonyesha mapungufu yao...
 
Kwa nini busara isitumike tu kuhakikiksha kila chama masbango yake na bendera vinakuwa salama hadi baada ya uchaguzi?? Je polisi wameshaelezwa kuhusu wizi huu? Mungu Ibariki Tanzania na Watu Wake, Utuepushe na Vurugu na Umwagaji wa Damu.
 
Hali halisi imeshajionyesha. nau pipo ar looking for proper leaders... watu wamechoka sana. sasa hii mbinu mpya ya kuiba bendera tena imeanza lini?.. du they real think it will help them? tunarudi palepale.. tunahitaji watu walio na uwezo wa kuongoza....we dont need suraaaaaaaaaaaaa................... Doktaaaaaaaaaaaaaaaaaaa..................chademaaaaaaaaaaaaaa............................ TUTAPITA BILA BENDERA
 
sheria inasema hairuhusu hata kuchana hizo pics za wagombea....kwenye kunyofoa hizo bendera sijui ndio inakuaje hapo???
 
.... inaonyesha Polisi nao hulala usiku. Hatuna Polisi tunawezi wa Kura....... na bendera za cCm. Bendera zetu wameenda kutambikia. .... Washindwe na walegee....AMINA. CHAGUA Dr.SLAA. BENDERA ZIMEENDA LAKINI MIILI NA UTASHI WA KITANZANIA TUMEBAKI NAO......
 
Mi nionavyo wajameni huyu lowasa hana akili hata kidogo na ndo maana baba wa taifa marehemu alikuwa hampendi hata kidogo.sasa kumchagua mtu anayeandamana nae ni kumsaliti mwalimu na ni sawa na kujitakia laana ya bure.
 
Na kwa hilo tukio, ndio kwanza kama vile wanazima moto kwa Petrol !!! Hili tukio limewapa wakazi wa Arusha
hasira sana.

Dawa ya hao wezi ni 31 OCT 2010 - tunafunguana mashati.
 
Gari la CHADEMA lishapita kutangaza kuwa bendera zake sasa hivi ni deal.
Kuna mchizi wangu kanipigia simu nikiwa job anataka kunipa mwekundu achukue bendera yangu ya CHADEMA iliyoko nje ya ghetto yangu nikamchomolea. Kanipigia tena kapanda dau hadi mbao. Jioni nikitoka job nataka nikamsikilizie. Kama na yeye yuko kwenye hilo deal la kuiba hizo bendera, hakiyanani nitamnyonya macho.
Lakini toka jana, stori kitaa ni kwamba bendera za CHADEMA zinatembea hadi kwa 30. Leo ndio nutaprove.
 
Jana eneo la sokoni kuu Arusha CHADEMA walikuwa na mpango wa kusimika bendera lakini vijana wa CCM waliwazuia jambo lililosababisha vurugu kubwa kabla ya polisi kuingilia kati kwa kurusha mabomu ya machozi.Mlingoti,mfuko mmoja wa cement na bendera vinashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi unaotegemewa kukamilika 01/11/2010.

Du! Kweli vyombo vya usalama ni ccm damu. Sasa uchunguzi kukamilika 1/11/2010 mantiki yake ni nini? Impact gani kwa kampeni itarajiwe?
 
Back
Top Bottom