Bendera ya Mwanzo Kabisa ya CHADEMA yaonekana Kigoma

Ikumbukwe kwamba wakati mfumo wa vyama vingi unaingia nchini Tanzania , kutokana na shinikizo la Kimataifa mwaka 1992 , kulikuwa na matakwa ya kisheria yaliyowekwa na Serikali ya Tanzania ili kufuatwa na vyama vya siasa vilivyojitokeza kuomba usajili huo .

Pamoja na masharti Lukuki , yaliyowekwa ikiwemo chama kinachotaka kusajiliwa kuwa na angalau wanachama 200 katika angalau kila mkoa katika mikoa 10 ya Tanganyika , na mikoa miwili ya Zanzibar , Masharti mengine ni chama kuwa na Katiba yake na bendera yenye nembo itakayotumiwa na chama husika .

Sasa leo naileta kwenu vijana na wazee ambao labda kwa sababu mbalimbali hamkuifahamu BENDERA YA KWANZA KABISA ILIYOTUMIWA NA CHADEMA MARA TU BAADA YA KUSAJILIWA , bendera hii amekutwa nayo mwanachama wa Chadema huko Kigoma ambaye alihudhuria Mkutano wa Kanda ya Magharibi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kanisa la Anglican Kigoma Mjini , mwanachama huyo amedai kuitunza bendera hiyo kwa kipindi cha miaka 29 .

View attachment 2181011
Hureeeeee
 

Attachments

  • inbound6571671042161781934.jpg
    inbound6571671042161781934.jpg
    6.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom