Bendera ya Chama cha Mapinduzi ni kinga? | Bendera ya CCM ni mbadala wa "Plate Number"?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
EhjBzOoX0AEpZ8v.jpg

Hii inamaanisha nini?

Wanaofanya hivi wanajua Askari wa Usalama barabarani lazima "atamezea" kosa lolote watakalolifanya barabarani kwasababu ni gari la chama

Je, wahalifu hawawezi kutumia mwanya huu wakajinufaisha?

Kwanini CCM waache chama chao kitumike namna hii?

FYI: Ukiachana na gari hili, siku kadhaa nyuma nimeona magari yakikimbia maeneo ya Kawe yakiwa yamefunika namba za gari kwa bendera ya CCM
 
Aisee...

Kwanini msajili hakifuti hiki chama?

Najua hili likitokea upande wa pili litaleta shida kubwa, tena wahusika watakamatwa na kufilisiwa nami nauliza kwanini hiki chama hakipewi hata karipio tu achilia mbali kufutwa!?
 
Badala ya kujikanyaga kanyaga jiulize saizi ni wakati gani na Gari lilikuwa wapi?, Jiulize namba ya Gari hilo ulikiisoma itakuongezea nini kwenye Kipato?
 
Aisee...
Kwanini msajili hakifuti hiki chama?

Najua hili likitokea upande wa pili litaleta shida kubwa, tena wahusika watakamatwa na kufilisiwa nami nauliza kwanini hiki chama hakipewi hata karipio tu achilia mbali kufutwa!?
Ataanzaje kwa mfano
 
Nakumbuka miaka ya nyuma pale mitaa ya Kinondoni Moscow,hananasif,manyanya na Brazil Kwenye vijiwe vyote vya wauza madawa ya kulevya kulikuwa na bendera za CCM na vyombo vyote vya Usalama hawakufanya kitu.....hata Leo hii ukitaka kupiga dili kiulaini peperusha bendera ya CCM
 
Hata vijiwe vya bangi hutumika bendera za CCM ili polisi wasikaribie
 
Mie hupeperusha Bendera napokuwa na safari za mbali..ni mwendo wa langalanga tu.

Siku hizi Dom dar fasta tu.
 
Badala ya kujikanyaga kanyaga jiulize saizi ni wakati gani na Gari lilikuwa wapi?, Jiulize namba ya Gari hilo ulikiisoma itakuongezea nini kwenye Kipato?
Sikutegemea hata siku moja kukutana na mnyakyusa mpumbavu kama wewe!
 
Nina Vijiwe vyangu Viwili tu hapo ukija utaweza kudhani upo Jamaica Makao Makuu ya 'Bangi' duniani, ila Bendera za 'CCM' ni Kinga Kutokamatwa.
 
Katika hali ya kushangaza na isiyotarajika, kuna picha ya gari iliyonaswa ikipita mitaani huku number plate yake ikiwa imefunikwa na bendera ya CCM! Pengine wahusika watoe ufafanuzi hili linawezekana vipi kufanyika? Askari wa usalama barabarani Je wamechukua hatua yoyote kwa mhusika aliyefanya hivyo?

Vipi pengine je aliyefunika hizo number plate kwa bendera kuna kibali alipata cha kufanya hivyo!? Na je huwa mamlaka husika zinatoa vibali vya namna hiyo!? What if kama chama kingine cha upinzani kikafanya hivyo...!?

Kwa kweli hilo la gari kufunikwa number plate kwa bendera tena ya CCM inaleta ukakasi, hasa kipindi hiki cha kampeni kwa kuwa wahalifu wanaweza kutumia wigo huo kusafiri au kusafirisha vitu ambavyo ni hatari kwa kufunika number plate za magari kwa bendera za CCM ili wasipate vizuizi endapo hili lililojitokeza halitatolewa ufafanuzi na hatua stahili kuchukuliwa!

IMG_1652.jpg
 

Attachments

  • IMG_1652.jpg
    IMG_1652.jpg
    43.3 KB · Views: 2
Katika hali ya kushangaza na isiyotarajika, kuna picha ya gari iliyonaswa ikipita mitaani huku number plate yake ikiwa imefunikwa na bendera ya ccm!
...Pengine wahusika watoe ufafanuzi hili linawezekana vipi kufanyika?
Askari wa usalama barabarani je wamechukua hatua yoyote kwa mhusika aliyefanya hivyo?
Vipi pengine je aliyefunika hizo number plate kwa bendera kuna kibali alipata cha kufanya hivyo!? Na je huwa mamlaka husika zinatoa vibali vya namna hiyo!?
What if kama chama kingine cha upinzani kikafanya hivyo...!?
Kwa kweli hilo la gari kufunikwa number plate kwa bendera tena ya ccm inaleta ukakasi, hasa kipindi hiki cha kampeni kwa kuwa wahalifu wanaweza kutumia wigo huo kusafiri au kusafirisha vitu ambavyo ni hatari kwa kufunika number plate za magari kwa bendera za ccm ili wasipate vizuizi endapo hili lililojitokeza halitatolewa ufafanuzi na hatua stahili kuchukuliwa!
View attachment 1565484
Hii ni Tanzania ndugu yangu.
Angalia maisha ya watoto wako tu bila shaka bado wadogo, hakikisha wanasoma shule nzuri wapate chakula kizuri n.k
 
Back
Top Bottom