Bendera ya CHADEMA yabebwa na afisa mtendaji wa kijiji (VEO), jengo lafutwa rangi

Ayoub Idd

Member
Aug 11, 2012
36
2
UKIUKWAJI WA DEMOKRASIA WAFANYIKA IRAMBA MASHARIKI.

Tukiwa katika mfumo wa vyama vingi bado kuna watu wana mawazo ya mfumo wa chama kimoja. Amani tuliyonayo ni lulu bado kuna watu wanaichezea tena kwa mzaha wa kitoto kabisa. Jana 01/12/2012 tukiwa kwenye tafakari ya siku ya ukimwi dunia kumbe wengine walikuwa na mipango isiyo na tija kwa taifa, majira ya saa 2 usiku ofisi ya CHADEMA KATA ya Iguguno ilivamiwa na watu wanaojulikana na kufutwa rangi, Afisa mtendaji wa serikali ya kijiji bwana Athumani Makiya akishirikiana na Mrisho pamoja na mtumishi mmoja wa serikali kwa makusudi na kiburi walifuta rangi ofisi ya CHADEMA kata ya Iguguno na kisha kuondoka na bendera.

Ofisi hiyo iliyopangishwa kwa shughuli za chama mpaka 2015 ni pango halali kabisa la CHADEMA, Tukiwa kwenye kumbukumbu za vurugu Ndago zilizopelekea mtu kuuwawa wengine tena wanatengeneza jaziba kwa wafuasi wa CHADEMA.

Kwasasa mambo yapo kwenye mwelekeo wa mahakamani, tunapenda sheria itumike kwa vile hili ni suala la kisheria. Kufuta alama za CHADEMA maana yake kufuta moja ya utambulisho wake, Kiongozi wa serikali kujiingiza kwenye itikadi za chama inajenga taswira ya utawala wa mabavu ukizingatia yeye ndio afisa wa usalama hapo kijijini kwa cheo alichonacho.

Rai ya hili viongozi kama hawa wasome nyakati, wajitambue na waache ushabiki wa vyama kazi itawashinda. Kuna fununua ya watu hawa kutumwa, wasitumike vibaya. CHADEMA ipo kwenye mioyo ya watu kama watu wapo basi ujue CHADEMA ipo.

Asanteni sana !
Mwanamikakati CHADEMA.
 
Hao ni wakusaheme tuu maana hawako sawa kichwani
 
Huu ni uchokozi wa watawala ili Vijana wa CHADEMA wachukue hatua(Reaction) kujibu mapigo na hapo ipatikane sababu ya kuwakamata.
Tunaomba Chadema watumie busara zifuatazo.

1/Watoe Tamko la kulaani kitendo hicho.

2/Watoe onyo kali kwa hao wahusika.

3/Wachungue dhumuni na msukumo ya hao watu kufanya hivyo na kuweka hadharani uchunguzi huo.

4/Wachukue hatua za kisheria dhidi ya wote waliohusika kama kuripoti Polisi!, Kwa Tendwa!, Mahakamani.

5/Wapandishe bendera mpya kwenye hiyo ofisi na sehemu mbalimbali kwenye hiyo kata(Ikiwezekana kila nyumba ya wanachama wa Chadema) tena kwa shamrashamra, nderemo, vifijo na mbwembwe.

6/Wapake rangi upya hiyo ofisi na pia sehemu mbalimbali za wazi kama kuta za nyumba za wapenzi wa Chadema.
 
Watafuta rangi ya chama kwenye majengo ila kamwe hawawezi kufuta mapenzi yetu ya chama yaliyojikita moyoni.

"CCM kwenye mabango CHADEMA kwenye mioyo yetu"

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hiyo ni sawa na kushindana na kimbunga!..kitu ambacho hawataweza ni kufuta chadema ndani ya mioyo yetu......
 
Huu ni uchokozi wa watawala ili Vijana wa CHADEMA wachukue hatua(Reaction) kujibu mapigo na hapo ipatikane sababu ya kuwakamata.
Tunaomba Chadema watumie busara zifuatazo.

1/Watoe Tamko la kulaani kitendo hicho.

2/Watoe onyo kali kwa hao wahusika.

3/Wachungue dhumuni na msukumo ya hao watu kufanya hivyo na kuweka hadharani uchunguzi huo.

4/Wachukue hatua za kisheria dhidi ya wote waliohusika kama kuripoti Polisi!, Kwa Tendwa!, Mahakamani.

5/Wapandishe bendera mpya kwenye hiyo ofisi na sehemu mbalimbali kwenye hiyo kata(Ikiwezekana kila nyumba ya wanachama wa Chadema) tena kwa shamrashamra, nderemo, vifijo na mbwembwe.

6/Wapake rangi upya hiyo ofisi na pia sehemu mbalimbali za wazi kama kuta za nyumba za wapenzi wa Chadema.

poleni.msife moyo. Pakeni upya rangi halafu iteni uongozi wa kitaifa uje kulizindua upya akiwepo tundu lisu.
 
Huu ni uchokozi wa watawala ili Vijana wa CHADEMA wachukue hatua(Reaction) kujibu mapigo na hapo ipatikane sababu ya kuwakamata.
Tunaomba Chadema watumie busara zifuatazo.

1/Watoe Tamko la kulaani kitendo hicho.

2/Watoe onyo kali kwa hao wahusika.

3/Wachungue dhumuni na msukumo ya hao watu kufanya hivyo na kuweka hadharani uchunguzi huo.

4/Wachukue hatua za kisheria dhidi ya wote waliohusika kama kuripoti Polisi!, Kwa Tendwa!, Mahakamani.

5/Wapandishe bendera mpya kwenye hiyo ofisi na sehemu mbalimbali kwenye hiyo kata(Ikiwezekana kila nyumba ya wanachama wa Chadema) tena kwa shamrashamra, nderemo, vifijo na mbwembwe.

6/Wapake rangi upya hiyo ofisi na pia sehemu mbalimbali za wazi kama kuta za nyumba za wapenzi wa Chadema.
Huyo Mtendaji hajui mwisho wa majukumu yaku hata kama alifanyiwa Interview hakuambiwa aangalie vyama vya upinzani na ukifuatilia kwa makini utakuta ni wale walioanza kwa kujitolea kwanzandipo akaajiriwa haelewi majukumu yake yanamtaka kufnya nini wapi na kwa wakati gani
 
Huku ikiripotiwa humu jamvini kuibwa kwa bendera ya chadema pale iguguno,hali ya mambo kwa majirani zao wa iramba magharibi si shwari.
Wanaotarajiwa kugombea watajwa wakipishana huku na huko kama mwewe msaka kifaranga,mengi yaibuliwa,wengine wanasomesha watoto kama alama ya kukumbukwa wakati wa kura.(hii nayo ni aina fulani ya rushwa ),anatokea maeneo ya ndago ana ukwasi mkubwa wa kifedha.mwenye jimbo hana habari ya kuwapelekea maji wakazi wa jimbo hilo.
DK. KITILA MKUMBO atajwa mwenye mrengo thabiti wa chadema.aweza kulinyakua jimbo kirahisi bila nguvu kubwa ya vijizawadi kama wanavyofanya wengine toka ccm.Yumo pia kijana mhandisi wa ujenzi ,ameapa kupeleka kazi yake ya kihandisi kuwatumikia wana iramba kama wakimpa ridhaa hiyo.kwa kuwajengea uwezo wa kuwa na umeme asilia utokanao na kinyesi cha mifugo.umeme ulioshindikana kuwafikia wana vijiji wengi.
Haya.yetu macho na masikio.
 
Halafu kuna watu huwa wanadiriki kusema eti nchi hii ina utawala bora wa sheria. Really?

Tanzania ya sasa kuna sheria za kibaguzi NA sizizo za haki. Zinatumika kuinufaisha CCM tu. 1) UFISADI na 2)VITISHO/MAUAJI (kisiasa) mifumo ya kimkakati.

Vita na harakati za ukombozi wa nchi hii si suala jepesi au la muda mfupi, lakini mwisho tutashinda na kufika tutakako kama Taifa huru, lenye misingi ya sheria, na maendeleo kwa kila raia wake
 
Ofisi haitapiga kura kwa hiyo wanajisumbua. Kama wangeweza kuifuta CHADEMA katika vichwa vya wananchi hilo lingekuwa ni tishio kubwa. M4C inawatesa.
 
hiyo ni kazi ya mchumi wao ndo huwa zake hizo kupambana na wapinzani wake kwa mbinu za hovyo hovyo.
 
watafuta rangi ukutani,wataondoa bendera lakini hawataweza kufuta moyoni mwa watu
 
Strategically publicize the incident to show cheated Tanzanians how people on power will disturb our peace.
 
Kwa kuwa ni serikali imefanya hivyo (mtendaji wa serikali ni kwa niaba ya serikali) na wamezoea kuchezea kodi za walala hoi, wapake hiyo rangi kwa hizo kodi za walala hoi. Hainiingii akilini mtendaji wa serikali afute rangi halafu CHADEMA wawajibike kurudishia.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom