Ayoub Idd
Member
- Aug 11, 2012
- 36
- 2
UKIUKWAJI WA DEMOKRASIA WAFANYIKA IRAMBA MASHARIKI.
Tukiwa katika mfumo wa vyama vingi bado kuna watu wana mawazo ya mfumo wa chama kimoja. Amani tuliyonayo ni lulu bado kuna watu wanaichezea tena kwa mzaha wa kitoto kabisa. Jana 01/12/2012 tukiwa kwenye tafakari ya siku ya ukimwi dunia kumbe wengine walikuwa na mipango isiyo na tija kwa taifa, majira ya saa 2 usiku ofisi ya CHADEMA KATA ya Iguguno ilivamiwa na watu wanaojulikana na kufutwa rangi, Afisa mtendaji wa serikali ya kijiji bwana Athumani Makiya akishirikiana na Mrisho pamoja na mtumishi mmoja wa serikali kwa makusudi na kiburi walifuta rangi ofisi ya CHADEMA kata ya Iguguno na kisha kuondoka na bendera.
Ofisi hiyo iliyopangishwa kwa shughuli za chama mpaka 2015 ni pango halali kabisa la CHADEMA, Tukiwa kwenye kumbukumbu za vurugu Ndago zilizopelekea mtu kuuwawa wengine tena wanatengeneza jaziba kwa wafuasi wa CHADEMA.
Kwasasa mambo yapo kwenye mwelekeo wa mahakamani, tunapenda sheria itumike kwa vile hili ni suala la kisheria. Kufuta alama za CHADEMA maana yake kufuta moja ya utambulisho wake, Kiongozi wa serikali kujiingiza kwenye itikadi za chama inajenga taswira ya utawala wa mabavu ukizingatia yeye ndio afisa wa usalama hapo kijijini kwa cheo alichonacho.
Rai ya hili viongozi kama hawa wasome nyakati, wajitambue na waache ushabiki wa vyama kazi itawashinda. Kuna fununua ya watu hawa kutumwa, wasitumike vibaya. CHADEMA ipo kwenye mioyo ya watu kama watu wapo basi ujue CHADEMA ipo.
Asanteni sana !
Mwanamikakati CHADEMA.