Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,531
Ni nani anapaswa kumwajibisha Kiongozi wa Serikali anayevunja sheria au kupuuzia sheria?
Sisi kama wananchi na Taifa, inakuwaje tunasulubiwa kwa Sheria na ukali tunapofanya makosa ya kupuuza, kuvunja au kupinda sheria?
Kwa nini viongozi wetu wanapenda kupinda ukweli na kutoa maelezo ya uongo bila woga huku wakijua wanavunja sheria?
Kwenye suala la Makontena TICTS na Karamagi, sheria na kanuni zilipindishwa na kuvunjwa, lakini hakuna aliyechukuliwa hatua.
Ukaguzi wa mahesabu wa CAD unaonyesha ukosefu mkubwa wa kufuata kanuni na sheria za kazi na kimahesabu, hakuna anayewajibishwa.
Pesa za BOT kufujwa, hakuna anayewajibishwa.
Mikataba mibovu, hakuna anayewajibishwa.
Hata hili la kuwekeana hirizi au unga wa sumu, ukweli umepindishwa wananchi tunadanganywa kuwa hakuna ushahidi na kilichotokea ni uzushi.
Ni mpaka lini viongozi na watawala wetu wataendelea kupindisha mambo na kudiriki kuvunja sheria bila woga?
Kila wakipindisha jambo na kupiga banana chop, goli twafungwa, je tufanye nini?