Ben Vs Kikwete

Ngonalugali

JF-Expert Member
Jan 12, 2008
659
102
Ndugu wapenzi wana JF, leo napenda tujadili suala la Mkapa na Kikwete katika awamu zao.

Binafsi huwa nakaa na kujiuliza hivi ni kitu gani ambacho Kikwete amekaa ikulu na kukifanya, nakosa jibu. Na mara nyingine huwa najiuliza, je, kama serikali ya bwana Ben isingegubikwa na matatizo ya ufisadi nchi ya Tanzania ingefika wapi?

Ni kweli kwamba Kikwete ana charisma ya kupendwa na watu na hiyo inampa nguvu kwenye uongozi wake. Lakini mpaka sasa mimi sioni ni nini anakifanya ikulu. Kwa mfano wakati wa serikali ya bwana Ben maisha hayakupanda gharama kiasi hiki na wala watanzania hawakuwa na maumivu kiasi hiki ninachoona kwa saa. Mfumuko wa bei ya vitu ulikuwa minimal na kwa hiyo watanzania waliweza kuishi kwa kumudu gharama za maisha kwa kiasi kikubwa. Je, hali ingekuwaje kama mikataba ya kitatanishi isingesainiwa? Ama ladha ingeongezekaje kama watu wasingejichotea vijisenti na kujilimbikizia? Nafikiri Tanzania ingekuwa kama nchi ya bwana Mbeki ama tungekuwa tunakaribia hapo.

Naomba kutoa hoja
 
Wakati Kikwete anachukua nchi alisema kuwa ndege ya uchumi ya nchi iko kwenye run-way na kwamba kazi yake ilikuwa ni kuipaisha hiyo ndege ya uchumi.

Cha kushangaza ni kwamba tumejikuta katika hali ambayo kumudu maisha imekuwa ni somo la Mtanzania la kila siku.
 
Mkapa alikuwa anashirikiana na wezake wachache kuitafuna nchi ilhali Kikwete katika kipindi chake anafanya wale waliotafuna nchi kuumbuliwa hadharani. Hali ya maisha ni ngumu kutokana na outcome ya ufisadi alioufanya Nduli Mkapa na si sababu ya uongozi wa JK. Mikataba mingi mibovu iliyopelekea hali ya maisha kuwa ngumu nchini ilisainiwa katika kipindi cha Nduli na si JK.

Nduli Mkapa alikuwa na roho mbaya sana hata uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa ni wa kinafki lakini JK hajishughulishi kubana uhuru wa vyombo vya habari na mawazo yenye kuleta changamoto.
 
Naona pana ukweli hapa
 
freetown,sio kama unaona pana ukweli kidogo,bali hayo maneno ya ngugu ni kweli hata mimi yamenigusa,ila nduli tupe solution ya hii njaa itakayoikumba tz wakati wowote
 
Mkapa alikuwa anashirikiana na wezake wachache kuitafuna nchi ilhali Kikwete katika kipindi chake anafanya wale waliotafuna nchi kuumbuliwa hadharani. Hali ya maisha ni ngumu kutokana na outcome ya ufisadi alioufanya Nduli Mkapa na si sababu ya uongozi wa JK. Mikataba mingi mibovu iliyopelekea hali ya maisha kuwa ngumu nchini ilisainiwa katika kipindi cha Nduli na si JK.

Nduli Mkapa alikuwa na roho mbaya sana hata uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa ni wa kinafki lakini JK hajishughulishi kubana uhuru wa vyombo vya habari na mawazo yenye kuleta changamoto.

Mkapa juu ya ubaya wake na wizi wake, na roho mbaya yake lakini amefanya mengi ambayo mazuri. Hii ni nature kwani sisi binaadam hatuna sifa za umalaika. Lazma mtu awe na kitu kibaya watu wapate kumtoa kasoro. Hii ndio Mungu ameumba iwe hivyo!

Mkapa ndie alieanzisha TASAF mafanikio ya TASAF nyote mnayajua na sasa TASAF imeingia awamu ya pili.Kipindi cha Mkapa watu hawakuwa na hali ngumu ya maisha kama sasa. Usalama ulikuwepo japo kwa kiasi ila waliomzunguka walikuwa wanajua "mzee" hatabiriki. Mkapa aliogopwa! Mkapa hakuwa akichekacheka alionyesha kuwa yeye ni kiongozi.

Kikwete.

Kikwete ni kweli ana bahati ya kupendwa sana hilo halipingiki ila ni lazma achukue tahadhari maana graph yake ya kupendwa inashuka kwa kasi sana. Ni mtu wa mzaha mzaha tu wengi waliomzunguka wanaujua udhaifu wake na ndio wanatake advantage hiyo. Mtaona jinsi alivyoshindwa kushughulikia ufisadi kwakuwa ni mtu dhaifu!

Mkapa na Kikwete wana kitu ambacho wana "share"

Wakati Mkapa ni Rais Kikwete alikuwa Waziri mwenye dhamana ya ushirikiano wa kimataifa. Kama waziri Kikwete alikuwa ndanii ya baraza la mawaziri lililoamua mambo yote yaliyofanywa kipindi cha miaka kumi ya mkapa kama mikataba iliyonyonga uchumi wetu. Kumbukeni kwenye kikao cha bunge wiki iliyomalizika Nazir Karamagi alisema uamuzi wa kuongezewa TICTS mkataba ulitokana na baraza la mawaziri na ana barua aliyoandikiwa kuwa (wao) serikali kupitia baraza la mawaziri na JK akiwamo wameridhia kuongeza muda kwa kampuni hiyo wa miaka 15.

Sasa hapa kama Kikwete angekuwa anaona wanayoyafanya ni madudu angewashauri wenziwe akajenga hoja wakakubaliana na wakaacha kufanya waliyoyafanya!

Kikwete ameshiriki kila lililofanywa na Serikali ya awamu ya tatu kwani yeye pia alikuwa mmoja wa watendaji wakuu wa Serikali!

Kikwete ameshiriki kuuza nyumba za serikali na yeye amenunua yake mtaa wa ursno regent estate. JK ameshiriki kuuza mashirika ya umma kwa bei chee. Ameshiriki mikataba ya TICTS,AGREKO,SONGAS,IPTL na mingine mibaya!

JK anajua kila baya lililofanyika na Serikali hii.

Sioni mantiki kwa wale wanaomtetea maana hata hoja hii ilivyo letwa imeletwa kiujanja janja hivi especia mchangiaji niliye m-coute. Anataka tumtukuze Kikwete kutupa uhuru wa kutoa maoni!

Kama nyie mtampa Kikwete ahsante kwa kuwapa uhuru wa kutoa maoni mie siwezi kufanya hivyo. Siwezi kufanya hivyo kwasababu najua ni haki yangu kikatiba. Hutakiwi umshukuru mtu kwa kukupa haki yako hata siku moja kwani huo ni utumwa na ukoloni ndani ya nchi iliyo huru.

Mkapa kachukua Kiwira coal mining na Kikwete na rafiki zake wamechukua pesa BoT na Tanesco kupitia Richmond.

Mkapa na Kikwete ni alpha na omega.

Wasalaam,
 
Yeah thats whats up,thats what it is!

Ila huyu JK kaachiwa pesa Hazina za kumwaga hata mwenyewe alikiri hatukutakiwa kufunga mikanda kiasi hichi,ukilinganisha na 1995 Mkapa alipochukua nchi ilikuwa na madeni kibao ya nje na ya ndani na Hazina palikuwa pa kavu.Kwa hiyo JK anatakiwa ku control nchi vema licha ya hizo zinazoundiwa tume still not a good excuse.
Maana sasa hatuongelea kulipa madeni kama kipindi cha Mkapa alishajitutmua kulipa mpaka Wahisani wakamwabia basi baba tumesamehe hayo mengine umeonyesha uko serious.
Ok sasa we here where we are tunahitaji kwenda mbele na rais wetu ni JK no more drama, kama anashughulikia matatizo afanye hivyo na mapema yeye aliahidi maisha bora kwa kila mTZ na hii inamaanisha kutoka tulipokuwa mwanzo kwenda hatua mbele asiwatumie watu kutoa sababu za ajabu kwani Richmond ilikuwa kipind gani ,IPTL nani alikuwa waziri dakika hiyo kama si yeye ,hayo mengine alikuwa baraza la mawaziri anajua in and out akitaka msaada aache serikali ya kishikaji aweke waTZ competent na waadilifu.
Afanye kazi Ikulu ukiwa mwadilifu hakuna raha ni mzigo kwa nchi inayohitaji kuendelea kama TZ.
 
Mimi bado sijaona sehemu ya kumshukuru Kikwete kwani sijaona anachokifanya. Hayuko serious na kazi yake ya kuliletea maendeleo taifa.
Kama Mkapa alimwachia visenti kwenye hazina na hata yeye mwenyewe akakiri kukuta hazina imejaa. Inakuwaje sasa kwamba maisha ya Mtanzania yamekuwa magumu na wala hakuna pesa ya nchi inayoweza kumsaidia Mtanzania isipokuwa za kuombwa kwa wahisani?

Kuna jambo hapa na mimi naona wachangiaji #6 na #7 wamesema yaliyo moyoni mwao. Bado tunahitaji michango ya watanzania ili tujue hatima ya neema yetu iko wapi.
 
ahahhaa nina mashaka sana na miaka 5 ya mwisho kama akibahatika kuipata tena...Jk nae sijui atahomola kitu gani..maana ndio miaka ya lala salama......ila hadi sasa JK hajafanya lolote..na hajajenga na kumaliza zile corridor roads alizikuta hazijamalizika.......
 
Jamani, mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.

Mkapa amefanya mambo mengi na makubwa kwa nchi hii. Ni kweli, alikiuka maadili ya uongozi na ni kweli pia waliokuwa chini yake walifanya mengi maovu ambao leo yanafunuliwa.

Binafsi sifurahii hata chembe uozo uliofanywa na serikali ya Mkapa, na wala siooni kuna jipya linalofanywa kwa dhati na serikali ya amamu ya nne.

Kwa uchache haya yalifanywa wakati wa Mkapa.

Barabara:

Barabara zilianza kujengwa, tena zile ziunganishazo mikoa. Barabara ya Mtukula-Bukoba kwenda mpaka Biharamulo.
Barabara ya Dar-Morogoro ilipanuliwa na kufanyiwa upanuzi na ukarabati mkubwa. Serikali iliahidi kufanyia upanuzi/ukarabati kama huo wa barabara ya Chalinze-Arusha, kitu ambacho mpaka leo hakijafanyika. Tukumbuke kuwa ilikuwa mpango wa serikali kuhakikisha barabara zote (trunk roads) ziwe ni za lami hadi kufikia Februari 2008. Leo hii, barabara ya Dodoma-Singida bado inasuasua. Kulikuwa kuna wakandarasi watatu au wanne, kila kandarasi na kipande chake, kati ya Dodoma-Manyoni-Singida.
Leo hii, serikali ya awamu ya nne imeshindwa kumalizia pale awamu ya tatu ilipoishia.

Hazina ya nchi:
Wakati awamu ya tatu inaondoka, serikali ilikuwa na hazina(monetary reserve) ya kuweza kufanya imports kwa miezi tisa.
Serikali ya awamu ya nne, katika kipindi cha mwaka mmoja tu, hazina hii ilishuka mpaka kufikia imports za miezi sita tu.

Gharama za maisha na kupanda kwa bei ya vitu:
Katika kipindi hasa cha mwisho cha awamu ya tatu, inflation ilikuwa controlled. Inflation haikuzidi 5% kati ya 2000 na 2005.
Tukumbuke hata vita ya Iraq,ambayo inadaiwa ku-create imbalances, bado serikali ya awamu ya tatu iliweza ku-contol inflation na mwananchi wa kawaida aliweza kumudu maisha,japo kwa kiasi kidogo alichonacho. Wananchi wa vijijini walikuwa na hali mbaya lakini walau wafanyakazi kwa mshahara mdogo bado waliweza kujimudu. Sasa hivi si mfanyakazi wala mkulima,wote hali ni mbaya.

Awamu ya nne:
Imekuta nchi ikiwa katika hali nzuri kiuchumi lakini haijaweza ku-capitalize kwenye state hii na sanasana tunazidi kurudi nyuma.

Yale yote maovu yaliyotendeka awamu ya tatu yashughulikiwe na wahusika wapewe "haki" yao kisheria, nchi isonge mbele.

Kuna jambo gani, walau moja, ambalo awamu ya nne, imelikamilisha mpaka sasa?

Kusema awamu ya nne imetoa uhuru wa habari sio kweli. Kuna mambo mengine sana yamechangia kwa "unaonekana" uhuru wa habari wa sasa.
 
Wadau linapokuja suala la kujadilia uongozi wa Mkapa na JK, JF ndo mahala sahihi kabisa pa kuonesha msimamo wa kila mwana JF. Kwa upande wangu mimi naamini kabisa ili kuwalinganisha wawili hawa kuna baadhi ya vitu lazima viangaliwe kwa undani. Natambua kuwa mimi si mchumi lakini nikiwa mwanachi wa kawaida kabisa naamini kuwa uongozi wa Mkapa ulikuwa ni bora kabisa ukilinganisha na huu wa sasa. Kuna suala la uteuzi wa nafasi za majaji, kila mmoja najua nafasi na umuhimu wa jaji katika muhimili wa mahakama, Kikwete kwa kuwa aliachiwa hazina iliyoyonenepa na mtangulizi wake, alijikuta akiteua majaji zaidi ya 15 kwa wakati mmoja akiwa na kiburi cha fedha ya Mkapa,

Mkapa katika kipindi chake cha uongozi, kwa takribani miaka 7 bei ya sukari, chumvi,mkate kibiriti na vingine pamoja na vyakula haikupanda. Kikwete amekaa miaka miwili tu lakini sasa hebu nenda ukaguse bei ya sukari, kibiriti hautaamini. Najua wengi mtashangaa ninachoandika lakini kwa yeyote anayeishi Tanzania (sio dar salam) atakubaliana na mimi kabisa kuwa kiongozi mzuri alikuwa ni Mkapa.

Natambua maamuzi yake ya kibabe lakini nadhani hiyo ndiyo ilikuwa aina yake aliyoichagua ya kutawala. Kiwete anaweza kuwa haoneshi ubabe hadharani lakini inawezekana kuwa ndiye mbabe halisi, ni kweli kuna uhuru wa magazeti lakini hebu angalia maisha wa waandishi yalivyo hatarini kiasi cha kufanya neno 'mwandishi wetu' kutamalaki katika kila ukurasa wa kwanza wa magazeti mengi.

Kwangu mimi Kikwete hajafanya chochote cha maana kwa wanachi wa chini ambao kwao serikali inapaswa kuwaandalia na kuwahakikishia upatikananji wa bidhaa muhimu.

MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI
 
Kweli Mkapa alipoingia madarakani nchi ilikuwa na matatizo mengi. Njia kubwa aliyoitumia kupunguza matatizo hayo ilikuwa ni ya kuuza raslimali zetu (madini, mashirika ya umma, majumba nk.) kuwepo kwa vitu vya kuuzwa kuliwavutia watu wengi na hivyo mahitaji ya shillingi yakawa makubwa. Hii ilisaidia sarafu yetu kupanda thamani. Lakini tukumbuke kuwa baada ya kuuza hizo raslimali zetu, hatukuwa na sheria ya kuwalazimisha hao wanunuzi waendelee kuzalisha mali hapa hapa nchini ili tuwe na bidhaa zitakazoendeza kufanya shillingi yetu ihitajike. Tunajua mitambo iliyong'olewa na viwanda kugeuzwa magodown ya mali toka nje (wapi kiwanda cha viatu Bora, wapi kiwanda mama Kilimanjaro machine tools nk). Kwa ufupi kipindi cha mkapa tulikuwa na mali(capital) za kuuza, na baada ya kuziuza,basi hatuna kitu tena. Ni kama ukiwa na shamba ukatangaza kuliuza wengi watakuja na utapata pesa nyingi, lakini baada ya hapo huna cha kuuza tena - si shamba umeshaliuza? Ndiyo maana tulishauri kuwa, tusingeuza namna hiyo, tungeingia ubia na mgao wetu wa faida ndiyo ungekuwa unabakia hapa nchini. Kibaya zaidi raslimali zetu zikauzwa kwa bei ya kutupa (mnakumbuka NBC). Na sasa ndiyo inagundulika kuwa hizo bei za kutupa zilikuwa za maksudi ili watu wapate siyo 10% bali 1000%!. Ukitafakari yote hayo, Mkapa alichokuwa anafanya ni kutuziba macho tu, na sasa tunapozidi kufumbuliwa ndipo tunagundua kuwa alifanaya zero+
Wale aliokuwa anashirikiana nao kula hela zetu ndiyo haohao walimega kidogo kuleta vitu kama TASAF ili tuzidi kulala! Hakika mwaka huu hautaisha kabla ya hao wanaosema Mkapa kuna zuri alilofanya kabla hawajamgeuka.
Kuhusu JK, Huyu amekuwa serikalini kwa muda mrefu na mabaya mengi ya Mkapa alishiriki/aliyajua na hakuchukua hatua yoyote. Hapa inawezekana alishiriki moja kwa moja au alishiriki shingo upande akisubiri kipindi chake kifike achukue hatua. Hapa mkikumbuka yaliyomkuta Mrema pale alipoligeuka baraza la mawaziri na kusema wazi uchafu wa serikali. Si mnakumbuka aliowataja kuiba mali za nji hii - mashamba ya mkonge ( si ndiyo hao hao sasa wamehusika katika Rada na EPA?), wizi wa dhahabu (biashara ikulu nk). Mzee wa watu sasa anaadhirika kwa ukweli aliousema wakati ule. Inawezekana Kikwete aliogopa kuchukua njia kama hiyo kwa hofu, na akaamua kubaki kimya. Sasa kama kweli ni hivyo, sasa analo rungu kamili, namna atakavyowashughulikia mafisadi ndiyo inatupa nafasi ya kusema yeye hakuwa mmoja wao au alikuwa na bado ni mmoja wao. Kwa kuanzia arudishe ile nyumba ya serikali aliyonunua, ili na wengine wafuatie.
Serikali ya JK haijafanya lolote la maana. Kuna sababu nyingi: ya kwanza ni uteuzi wa kiswahba alioufanya, bila kuwa mwangalifu kuwa hao maswahba ndiyo mafisadi. Pili tabia yake ya kutochukua hatua haraka na kutumia lugha laini sana utadhani siyo askari, km. EL alipojiuzuru kwa kashfa ya Richmond - eti ni ajali ya kisiasa?, au kuwambia wale wenye mikataba ya kuchimba madini eti tuwaombe turekebishe mikataba badala ya kuwaambia "mikataba hii ni ya kinyonyaji na hata katika nchi zenu msingeweza kufanya hivi, hivyo tunaifuta na tuanze upya". Tatu ni kushuka kwa thamani ya dola, kukua kwa uchumi wa China na vyote hivyo kusababisha bei ya mafuta kupanda. Nne ni shilingi yetu kushuka thamani kwa kuwa capital goods tulishaziuza, na wale tuliowauzia kwa bei ya kutupa, hata kodi hawalipi (tax holidays), hata mauzo yao hatuyajui (dhahabu sasa ounce ni dola 1000, lakini sisi tunalipwa mrahaba kwa bei ya dola 280!).
JK asipojipambanua na mafisadi, hakika mzimu wa Nyerere walioenda kuuchokoza huko Butiama - utamlamba!)
 
Mkapa alikuwa anashirikiana na wezake wachache kuitafuna nchi ilhali Kikwete katika kipindi chake anafanya wale waliotafuna nchi kuumbuliwa hadharani. Hali ya maisha ni ngumu kutokana na outcome ya ufisadi alioufanya Nduli Mkapa na si sababu ya uongozi wa JK. Mikataba mingi mibovu iliyopelekea hali ya maisha kuwa ngumu nchini ilisainiwa katika kipindi cha Nduli na si JK.

Nduli Mkapa alikuwa na roho mbaya sana hata uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa ni wa kinafki lakini JK hajishughulishi kubana uhuru wa vyombo vya habari na mawazo yenye kuleta changamoto.

Tafakari yako NDUGU naiunga mkono moja kwa moja. Nina imani kuwa ungekuwa wakati wa BWM vyombo vya habari vyenye msimamo wa Kizalendo kama MWANAHALISI, TANZANIA DAIMA etc na Mitandao iliyokwenda shule kama JF na KLHN vingekuwa vimepata misukosuko mikali tu; na hata wasomaji wake kudhibitiwa kwa nguvu zote kana kwamba ni MAFISADI. Twamuombea Rais Kikwete kwa MUUMBA wetu azidi kupata ujasiri wa kupambana na asirudi nyuma mpaka safu zote za CHAMA na SERIKALI amezisafisha. Hakuna kurudi nyuma kwani kila mapinduzi kokote duniani yana gharama kubwa. Aluta Continua, Pamberi ne Chimurenga!!!.
 
Hivi uhuru wa vyombo vya habari katika habari zipi za maana?, si ndio hao hao wameitwa ''makanjanja''? asa ''kanjanja'' akipewa uhuru wakuandika anachotaka na akiambatanishiwa na bahasha ya khaki what do you expect?

Sometimes huwa nafikiri vyombo vya habari viko zaidi kuandika maovu ya the past wether its true or not while diverting our attention ya Watz kuangalia whats going on on the ground so far!

Jamani tuwe objective!, tunapoongolea ukweli tusionekane na sisi ni ''mafisadi'', pamoja na juhudi za muungwana anazozionesha he is very far from Mkapa, Ben pamoja na mapungufu yake lakini jamaa alijitahidi sana kurekebisha uchumi wa nchi ilo halina ubishi.

Am telling you itafika 2010 nothing have been done on the groung na hali ya MTZ inakuwa kama ile ''state of nature ya THOMAS HOBBES'', ie nasty, brutish, poor, and short na hao mafisadi nothing watakuwa wamefanyiwa, just wait and see!!
 
[Nadhani hamna wa kumlaumu. Tuanze kunyoosheana vidole sisi kwa sisi. Wewe uliyechangia topic hii na baadhi yaw engine wengi ndio mnaopaswa kulaumiwa. Usinyooshe serikali kidole, haina makosa yeyote ya kufanya inachokifanya. Serikali kama serikali haidondoshwi na Mungu, inawekwa pale na watu (wananchi). Sasa inakuwaje leo mnailaumu serikali kabla ya kuwalaumu walioiweka madarakani.

Hali ya maisha tuliyonayo haijaletwa na serikali imeletwa na wewe mwenyewe kwa hiyo ujilaumu mwenyewe. Mfumuko wa bei, kupanda kwa garama za maisha, barabara kutojengwe, uwanja mpya wa taifa kusua sua, ufisadi, mikataba mibovu vyote vimechangiwa na wewe au mimi na sio serikali.

Mwananchi Anachagua Mbunge/Rais Serikali

Huyu wa mwisho akiboronga tusimlaum sio kosa lake, kosa liko kwa huyu wa kwanza kabisa ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuamua nani amuongoze. Siku zote tuwe tunamnyooshea huyu wa kwanza kidole na sio huyo wa mwisho. Serikali isingekuwepo bila process nzima na maamuzi yaliyofanywa na wananchi
 
Nashangaa sana mtu mzima anaposema ana uhuru wa habari. Inawezekana ni miongoni mwa wenye Vijisenti nini?Wewe unajua ni asilimia ngapi ya wananchi wa TZ wanapata habari za kila siku, ni wangapia wanapata habari za kiuchumi,habari kwa nini maisha yamepanda kiasi hiki.

Baadhi ya Magazeti kuandika udaku bila kuchukuliwa wazi wazi sio uhuru wa habari. Ni wananchi na waadhishi wangapi leo hii wanaweza kusimama na kuikosoa Serikali. Wewe unapoficha jina lako halisi hapa JF huo ni uhuru kweli? Tusiwe wanafiki, tuseme ukweli.

Mwananchi ni masikini wa kutupwa atakuwaje na uhuru wa habari
 
Haijalishi umefanya mangapi mazuri kafanya mazuri ndiyo lakini mazuri yote aliyofanya yanazimwa na ufisadi wa hali ya juu waliyoufanya yeye na jopo lake la watendaji akiwemo huyo aliyeko sasa kikwete.

kikwete hawa aliyowarithi wamekuwepo kwa muda mrefu kwa sababu naye ni mhusika hawezi kabisha kuwachukulia hatua kali za kutisha ambazo badae zitaleta tija kwa taifa letu. wengi wao ni waoza.

ni fedha nyingi sana inayozungumziwa kufisadiwa na watu wachache lazima mabaya yao na ufisadi vitajwe wazi wazi mazuri yao yatakuja tajwa wakiondoka. nanake tayari wao wana maagent wa kuyasema mazuri yao. ni kwa mfano niseme hivi sioni sababu ya kuongea mazuri ya kampuni say yoyote ya simu wakati najua yanavyotunyonya, tunawajibika kuyasema yale machungu wasiyoyasema manake mazuri yao wanayatoa kwenye matangazo lakini hawatoi mabaya kwenye matangazo. kwa hiyo sisi wananchi wenye uelewa kidogo ndo tunapaswa kuyasema yale yenye kufichwa iwe ni kwa serikali au kwa makampuni
 
Linapokuja suala la utendaji ninakuwa na hofu na serikali yetu ya matabasamu kumi na saba. Sidhani kama wako seriuos na matatizo ya waliowaweka madarakani kwa kusikia ahadi zao.
Ni watu ambao wamekuwa na mengi ya kuahidi bila kutekeleza. Kwa mfano wakati wanaingia madarakani kulitokea shida ya njaa na vyakula kupanda bei. Hali ya tahadhari ilitolewa na maghala ya siri-kali kufunguliwa ili kupoza bei kwa mwananchi. Hiyo bado haikusaidia. Na baadae waliomba wenye mitaji waagize vyakula kutoka nje na kuwafutia kodi ili bei ziwe zinaendana na pato halisi la mwananchi, lakini kilichofuatia ni kuwa bei hizo zilibaki kwenye vyombo vya habari na sokoni kukawa na bei mara mbili ya ile iliyotangazwa. Katika hilo hakuna aliyeshtuka kwani walishasema na kwa kuwa waaguzaji wakuu walikuwa makambale (wapendao kukaa kwenye uchafu), basi waliachwa waendelee kujinufaisha kwa kumnyonya mwananchi.
Angalia dana dana ya simenti kupanda bei. Waliomba wenye mitaji (makambale) waagize cement kutoka nje ili kukidhi mahitaji ya watanzania na kudhibiti mfumuko wa bei kitu ambacho nacho hakijaleta tofauti.
Hii yote inatokana na ufuatiliaji wa kigoi goi. Serikali yetu inasema kwenye vyombo vya habari wananchi wasikie kuwa wanajaliwa sana huku hiwatendei kwa kadri ambavyo inasema.

Nilifurahishwa na mchakato wa kupandisha bei ya gesi ya Songosongo. Sababu kubwa za mwekezaji kuomba kupandisha bei ni deni alilokopa kwa ajili ya kununulia mitambo ya uzalishaji na usambazaji wa gesi. Eti inabidi nipandishe bei ili niweze kulipa deni hilo kwa muda tuliopatana na mkopeshaji. Swali ni je, hiyo mitambo amekopeshwa mwananchi ama mwekezaji? Ni kwa nini yeye akope halafu sisi tuumie? Na, je, endapo kama deni hilo litalipwa kuna makubaliano yoyote ambayo yanaonyesha kuwa bei itashuka kwa kiwango cha kufikia ile ya zamani?

I wapi serikali inayoyaona matatizo yanayomwelekea mwananchi na kuyatatua?

Hayo tunayoyaona kama mazuri yatakuwa mabaya zaidi wakitoka madarakani kwani hawana jipya ila ni ubabaishaji tu.
 
Huo wote upuuzi,hawajafanya lolote la maana,kazi zote zilianza wakati wa Nyerere,akili ya Mwl ilikuwa inachaji sana hawa jamaa wanashindwa maintainance sijaona jipya!ama daraja la Rufiji na kipande cha barabara cha Somanga Nankurukuru ambacho kimekuwa wimbo wa Taifa,Mafisadi ni mafisadi tu hawana jema.
 
Back
Top Bottom