Ben Saanane

Serikali inaingiaje hapo wakati huyo Ben katoweka mwenyewe.
Inaweza kuwa katoweka ama katwaliwa ila yote heri ni nani anawajibu wa kulinda raia na Mali zao, bagamoyo Ile miili Saba ilijibiwa kuwa walikuwa wahamiaji haramu- kesho agizo linatolewa miili ichunguzwe- jiongeze ulink hizo squence of events the take your own mind make personal argument then make conclusion.
 
Na ndio maana mvua hazinyeshi , mpaka mtakapo heshimu pumzi ya Mungu ndoo tutaenda sawa
 
Inaweza kuwa katoweka ama katwaliwa ila yote heri ni nani anawajibu wa kulinda raia na Mali zao, bagamoyo Ile miili Saba ilijibiwa kuwa walikuwa wahamiaji haramu- kesho agizo linatolewa miili ichunguzwe- jiongeze ulink hizo squence of events the take your own mind make personal argument then make conclusion.
Hata hivyo hiyo hoja haifanyi serikali ingie hapo kama unavyodhani.Kwani Ben ni mtu wa kwanza kutoweka mbona watu wengine wanatoweka na serikali haidaiwi?Chakufanya hapo taarifa zifikishe polisi km hazijafikishwa lkn hiyo isichukuliwe kua ndiyo kuitwisha Serikali jukumu km vile ndiyo ili engineer kutoweka kwa Ben.
 
Umetwacha na fadhaa Beni mwana wa Saanane
Fokasi yako ni taa ,Ya usiku wa manane
Fesibuku unang’aa, Mithili ya manemane
Mlete wetu shujaa, Beni mwana wa Saanane

Hupimiki kwa dhiraa Si mnyama ulingane
Mizani inakataa ,Faru Joni mianane
Hata ukijaza paa , Makumi elfu nane
Tunamtaka shujaa, Beni mwana wa Saanane

Sasa ni siku kadhaa, bila Beni Saanane
Mitandao imejaa simanzi bila Saanane
Nimakini si kichaa, bila hoja apambane
Tunamtaka shujaa, Beni mwana wa Saanane

Hawezi zimika waa ! eti asionekane
Sio kama mshumaa,msitake tubishane
Mtachochea balaa ,mapema tuelewane
Tunamtaka shujaa, Beni mwana wa Saanane

Mwachieni bila waa, uwanja wa nanenane
Tutakuja kumtwaa, hata usiku Saa nane
Mkizidi kukomaa, tutakuja tupigane
Tunamtaka shujaa, Beni mwana wa Saanane

Hoja zake ni makaa, yenye moto mwanawane
Shuti zake ni balaa ,kama zile za Zidane
Mahasimu waduwaa ,utadhani masenene
Tunamtaka shujaa, Beni mwana wa Saanane

Kimya sisi tumekaa, leo kwa Beni Saanane
Kesho nani wamtwaa? Kizani wakambane
Hasira yazidi jaa, msitake tubanane
Tunamtaka shujaa, Beni mwana wa Saanane

Nasepa nikitambaa, wanakuja wanibane
Mwaona mi shujaa? nisubiri tupambane?
Mie sitaki balaa , namtafuta Saanane
Tunamtaka shujaa, Beni Rabiu Saanane
Unamtaka saa nane, subiri ukione
Huo wako unene, kwa kioo jione
Utakuwa ka senene, ngoja wakubane
Ulimboka hodi, tia lako neno.

Kwa viwembe wakuchane, wakuchezeshe sebene
Tumbo likutune wakurya twaita "riheme"
Na Magogoni waone, kama huna mapene
Ulimboka sema, je Ben bado yupo?

Sijaribiwi "nahene", ngoja usalama waone,
Meno na koreo vikutane, saa mbili hadi saa nane
Malofa wenza waone, kipigo na ya damu matone
Ulimboka mwambie kijana aache!!!
 
Mods wa facebook km walivyo wakina Max Mello wa JF

Hiyo tabia facebook imeanza lini?, ninachojua Kuna idadi ya watu ikitimia kukulalamikia kinachofuatwa Ni kufungiwa account kwa muda siyo kufuta bandiko, bandiko anafuta aliyeandika, sasa swali huyo mwenye password ya facebook ya Ben Ni nani?, na kaipata wapi kama hawajamlazimisha kutoa hiyo password
 
mwenyekiti ala bata na chaguzi za kitaa
kawaacha mataa waendelee kutapata

yeye kwa mwendo wa kasi akaenda kasikazi ,krismasi kujinafasi
 
Hiyo tabia facebook imeanza lini?, ninachojua Kuna idadi ya watu ikitimia kukulalamikia kinachofuatwa Ni kufungiwa account kwa muda siyo kufuta bandiko, bandiko anafuta aliyeandika, sasa swali huyo mwenye password ya facebook ya Ben Ni nani?, na kaipata wapi kama hawajamlazimisha kutoa hiyo password
Peleka taarifa zako pahala husika (manake hapa JF si phala sahihi) ukawataje hao waliomlazimisha Ben kufanya hivyo,pengine itasaidia yeye kupatikana.
 
Back
Top Bottom