Ben Saanane

Aug 17, 2016
69
125
Umetwacha na fadhaa Ben mwana wa Saanane
Fokasi yako ni taa, Ya usiku wa manane
Fesibuku unang’aa, Mithili ya manemane
Mlete wetu shujaa, Ben mwana wa Saanane

Hupimiki kwa dhiraa Si mnyama ulingane
Mizani inakataa, Faru Joni mianane
Hata ukijaza paa , Makumi elfu nane
Tunamtaka shujaa, Ben mwana wa Saanane

Sasa ni siku kadhaa, bila Ben Saanane
Mitandao imejaa simanzi bila Saanane
Nimakini si kichaa, bila hoja apambane
Tunamtaka shujaa, Ben mwana wa Saanane

Hawezi zimika waa ! eti asionekane
Sio kama mshumaa, msitake tubishane
Mtachochea balaa, mapema tuelewane
Tunamtaka shujaa, Ben mwana wa Saanane

Mwachieni bila waa, uwanja wa nanenane
Tutakuja kumtwaa, hata usiku Saanane
Mkizidi kukomaa, tutakuja tupigane
Tunamtaka shujaa, Ben mwana wa Saanane

Hoja zake ni makaa, yenye moto mwanawane
Shuti zake ni balaa, kama zile za Zidane
Mahasimu waduwaa, utadhani masenene
Tunamtaka shujaa, Ben mwana wa Saanane

Kimya sisi tumekaa, leo kwa Ben Saanane
Kesho nani wamtwaa? Kizani wakambane
Hasira yazidi jaa, msitake tubanane
Tunamtaka shujaa, Ben mwana wa Saanane

Nasepa nikitambaa, wanakuja wanibane
Mwaona mi shujaa? nisubiri tupambane?
Mie sitaki balaa , namtafuta Saanane
Tunamtaka shujaa, Ben Rabiu Saanane
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,150
2,000
Mbowe hata huzuni hana,anawaambia wazazi wa Ben watulie,hata yeye ana masahibu mazito
 

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,823
2,000
Pengine kashushwa kwa shetani. Kwa shetani kuna giza. Labda kesho atakapozaliwa nabii Issa a.k.a Yesu, atamshinda shetani na Ben Saanane ataonekana.
 

onkoko

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
514
500
Hapo mtaripua bomu usiku wa saanane
Kwa amani twamtaka saanane
Kwa kweli tume mkumbuka saanane.
Ushairi huu umeniumiza sana moyo.
Pinga ukatili zidi yawapinzani na wakosoaji wa hii serikali.
 

ISIS

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
91,479
2,000
Kazi kweli kweli. ..inasikitisha sana haswa kwa wazazi wake yaani sipati picha. .eeh MOLA wajalie hao ndugu na wazazi amani yako...uchungu. ..
 

Polycarp Isaya Urio

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
2,008
2,000
Hapo mtaripua bomu usiku wa saanane
Kwa amani twamtaka saanane
Kwa kweli tume mkumbuka saanane.
Ushairi huu umeniumiza sana moyo.
Pinga ukatili zidi yawapinzani na wakosoaji wa hii serikali.
Serikali inaingiaje hapo wakati huyo Ben katoweka mwenyewe.
 

balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
8,778
2,000
Makala zake makini ,waovu aliwabana.Wakaanza kutapatapata hata usiku saa nane.Ben akakomaa wasipate kumbana.Hila zao wakapanga hadi usiku wa manane.Ben wakamteka hakuna aliyewaona.Mmoja akakurupukia urafiki na Saanane.Povu jingi kumtoka na kuwataja wanae kumjua saanane.Ben Rabiu Saanane,pambana huko uliko.
 

balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
8,778
2,000
Umma unasononeka,Ben wetu yuko wapi?Ni nani aliyemteka na wapi kampeleka? Tuachie Ben wetu aongoze mapambano.
 

lothrito

JF-Expert Member
Oct 29, 2015
1,495
2,000
Huyu jamaa namkubali sana MUNGU mlinde brother ben popote pale alipo. AMEN
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom