Ben saanane Umeshindwa kutumia ushawishi wako kumaliza ukatili kwa kina mama na watoto Rombo?

Mtimbo

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
1,392
796
Habari wadau?
Bila kupoteza mda nijielekeze kwenye mada.

Leo nimeona nimuulize swali Ndugu yangu Ben saanane ambaye kiasili ni mkazi wa Rombo.

Wakazi wa wilaya ya Rombo pamoja na changamoto na matizo mtambuka yanayowakabili yaani kama vile umasikini wa kipato,Afya Elimu na mengineyo, ambayo yamezoeleka kwani matatizo hayo unaweza kuyakuta sehemu nyingine yoyote hapa Tanzania.

Lakini kwa wakazi wa Rombo kwa sasa wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kimaadili yanayotokana na Unywaji wa pombe Uliopindukia kwa wakazi wake wakiongozwa na akina baba.

Kutokana na unywaji wa pombe uliokithiri tayari kuna visa kadhaa vya kusikitisha vimeripotiwa kwenye vyombo vya habari.

Mathalani kumewahi kuripotiwa tukio la kinamama wa Rombo "kuwavusha" wanaume kutoka nchi jirani ya Kenya kwa lengo tu la kufanya nao Mapenzi chanzo kikidaiwa kushindwa kwa wanaume wa Rombo kuwatimizia haja za kimapenzi kwa wanawake hao kwa sababu ya ulevi wa kupindukia.

Athari za ulevi wilayani Rombo aziishii hapo tu, tayari Familia nyingi zimeshasambaratika na kuacha watoto wakikua bila malezi na maadili ya kutosha kuishi vizuri katika Jamii.

Sambamba na hilo
tayari wilayani Rombo kumeripotiwa idadi kubwa ya watoto walio chini miaka kumi na tatu wakilawitiana.

kabla hilo halijasahaulika vichwani mwa watu,
Magazeti ya wiki hii yameripoti kundi kubwa la watoto wa shule wakinajisi (kufanya ngono) na mifugo.
Kwa kifupi Wilayani Rombo hali ni mbaya na inasikitisha sana na sababu kubwa ikiwa ni Pombe.

Sasa swali langu nalielekeza kwa kijana mwenzangu Ben saanane.

Ben una elimu nzuri, uzoefu na exposure ya kutosha kweli unashindwa hata kufanya kitu ukalipunguza kama sio kulimaliza kabisa tatizo hili la Ulevi Rombo?
 
Yeye ana deal na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati mama zake wamemshinda
Hatari sana ila Ben ana elimu nzuri tu kama angeitumia angalau robo tu ya kipawa alichonacho Rombo ingebadilika
 
Kama ambavyo tetemeko na majanga mengine ya asili yaliyolikumba Taifa letu yasivyoletwa na serikali,vivyo hivyo hayo yote uliyoyaorodhesha hapa na kumtaka Ben akabiliane nayo hakuyaleta yeye.Iweje umtwike mtu binafsi jukumu la serikali wakati mtu huyo unayejaribu kumuhusisha na matatizo ya jamii yake hana facilities zozote za kukabiliana na matatizo hayo?

Serikali iliyoapa kuwatumikia wananchi imefanya nini ili kukabiliana na changamoto hizo za wanaRombo?Au Rombo imekuwa Jamhuri na Rais wake ni Ben?Nafikiri ungesomeka zaidi kama hoja yako ungeilekeza kwa yule anayejitanabaisha kama Rais wa wanyonge na masikini ambaye mnapambana mitandaoni kumuwezesha achukue tuzo ya "Forbes",akichuana na " Peoples of Rwanda"

"Peoples of Rwanda" ni pamoja na walevi,wavutabangi,makahaba,mawaziri,viongozi wa dini,Rais wao na wanyarwanda wote,sasa sijuwi hao Forbes walimaanisha nini walipoamua kumshindanisha mukulu na "Peoples of Rwanda"
 
Acha kufananisha tetemeko la ardhi na vitu vya kijinga
 
Huyu Ben ambaye hupata likes 100 kwenye FB lakini akaambulia kura 3 kinyang'anyiro kura za maoni ubunge Rombo?...inamaana hata familia yao hawamuamini?. Bure kabisa!.
 
Acha kufananisha tetemeko la ardhi na vitu vya kijinga

Kama unakili kuwa tetemeko la ardhi ni moja ya tukio baya na lililoacha simanzi hapa nchini mbona hadi leo mnyonge mwenzetu hajaenda kuungana na wanyonge wa Kagera waliopatwa na tukio hilo walau akajionea mwenyewe madhara yaliyoletwa na tetemeko lile,badala yake ameishia kuwatazama wahanga wale kupitia vyombo vya habari?
 
Ben yupo busy anataka aione salary slip ya rais, hayo hayamhusu kwa sasa.
 
Ben yupo busy anataka aione salary slip ya rais, hayo hayamhusu kwa sasa.
ningekuwa mimi ningeachana na kishina cha mshahara wa Rais na ningejielekeza kwenye kuokoa maisha ya watoto wadogo wanaolawitiana, hawa watoto ndio baadae wanageuka wanakuwa mashoga
 
Kama ambavyo tetemeko na majanga mengine ya asili yaliyolikumba Taifa letu yasivyoletwa na serikali,vivyo hivyo hayo yote uliyoyaorodhesha hapa na kumtaka Ben akabiliane nayo hakuyaleta yeye.Iweje umtwike mtu binafsi jukumu la serikali wakati mtu huyo unayejaribu kumuhusisha na matatizo ya jamii yake hana facilities zozote za kukabiliana na matatizo hayo?

Serikali iliyoapa kuwatumikia wananchi imefanya nini ili kukabiliana na changamoto hizo za wanaRombo?Au Rombo imekuwa Jamhuri na Rais wake ni Ben?Nafikiri ungesomeka zaidi kama hoja yako ungeilekeza kwa yule anayejitanabaisha kama Rais wa wanyonge na masikini ambaye mnapambana mitandaoni kumuwezesha achukue tuzo ya "Forbes",akichuana na " Peoples of Rwanda"

"Peoples of Rwanda" ni pamoja na walevi,wavutabangi,makahaba,mawaziri,viongozi wa dini,Rais wao na wanyarwanda wote,sasa sijuwi hao Forbes walimaanisha nini walipoamua kumshindanisha mukulu na "Peoples of Rwanda"
Hivi mbunge wa rombo sio selasini? Mbona mamtwisha ben saanane zigo sio lake.
 
Sina imani na bandiko lako... umekuwa msomaji wa vichwa vya habari zaidi ya habari yenyewe... sie kwetu ni marangu na nliwahi kuishi kwa ndg zang rombo... ni kweli wanakunywa pombe lakini si kama mnavyosema... ni wachakarikaji vizur sana na hela wanazo za kutosha... waacheni wafanye yao kama kuna tabia ya namna hiyo ni jukumu la serikali sio la sa nane
 
Mimi nadhani watu waache kukuza mambo....hayo yanayoelezwa Rombo hakuna yasipokuwepo Tanzania yetu. Na haua ukifika Rombo ukaongea na wenyewe bado tatizo watakueleza sio kama linavyojaribu kukuzwa. Lakini isitoshe suala la kupambana na umaskini sio La Ben ni suala la kila mmoja wetu hasa wakiongozwa na serikali iliyoko madarakani
 
Ben yupo wapi. Kila siku kwenye mtandao huku nyumbani kwao watu wakiwa na tabia mbovu kufikia kubaka watoto wa shule.

Kutwa kucha tupo kwenye mitandao.
Wewe ben huwezi kuhamasisha wananchi wa rombo wakaacha tabia hizo mbovu?

Hama huwezi hutufai katika jamii. Maana asiye tunza wa kwao ni mbaya zaidi ya shetani.

Naunga mkono hoja.
 
Acha kufananisha tetemeko la ardhi na vitu vya kijinga
Ujinga kwako kwa wengine janga. Akili yako inaishi ndani ya box ndio maana unadhani yanayotokea hapa tanzani ni upuuzi tu kwako kumbe wengine wanateseka sana.
Nadhani hulijui vizuli swala la rombo. Shida yangu kwa mleta uzii ni kumtwika Ben kama ndie Rais wa nchi au kiongozi wa imani rombo. Serikali inajukumu la kulinda na kuendeleza kizazi chenye afya na maadili katika nchi yake.
 
Back
Top Bottom