Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, amani iwe kwenu.
Binafsi huwa nashangazwa sana na hawa vijana wa BAVICHA. Wakati mwingine ninadhani kuwa wanachokifanya ama ni maigizo au wana matatizo ya malezi kwenye chama chao.
Twende taratibu.
Jumatatu Oktoba 3, 2016, Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya Geita Mhere Mwita, alipata ajali Mjini Dodoma alipoenda kushuhudia hukumu ya Viongozi wa BAVICHA Taifa walioshtakiwa kwa makosa ya Uchochezi, kesi ambayo viongozi hao walishinda baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha madai hayo. Haijaelezwa mazingira ya ajali hiyo. Haijaelezwa pia kama ni ya pikipiki ama ya gari. Haijaelezwa pia wengine waliohusika kwenye ajali hiyo. Inatia mashaka.
Baada ya kuumia, viongozi wa BAVICHA walimkimbiza kwenye Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambako alipata matibabu ya awali. Hata hivyo, taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa BAVICHA ambaye napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa jinsi anavyonipa ushirikiano juu ya kambi yao, alisema kuwa Hospitali ya Dodoma iliamua kumpa rufaa Mhere Mwita ya kutibiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kitengo cha Mifupa (MOI). Hii ni baada ya tatizo la Mhere Mwita kuwa kubwa kiasi cha Hospitali ya Dodoma kushindwa kulishughulikia kwani alivunjika kwenye maungio ya paja na kiuno ya mguu wa kushoto.
Kutokana na rufaa hiyo, Mhere Mwita alisafirishwa kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam na aliwasili Muhimbili (MOI) majira ya saa 12 jioni ya tarehe 4 Oktoba 2016. Logistics za kumpokea Mhere MOI zilikamilika majira ya saa nane usiku wa tarehe 5 Oktoba 2016.
Hata hivyo, cha kushangaza ni kwamba, Makamanda wote ambao walikuwa wanamhudumia Mhere Mwita siku hiyo walielekwa sehemu maalum ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kujipongeza. haijaelezwa ni pongezi za aina gani ijapokuwa walizificha kwenye mgongo wa sherehe ya kuzaliwa kwa Malisa Godlisten. Makamanda hao walikunywa vinywaji vikali huku wakifurahi, kuimba na kusherehekea kana kwamba hakuna tatizo kubwa lililomkumba mmoja wa wanafamilia. Ni sherehe, chereko, nderemo na burudani ya kila aina.
Kinachonishangaza zaidi ni dhihaka wanayoendelea kuifanya kwa Mhere Mwita baada ya kupata ajali hiyo. Haikatazwi watu kumtembelea mgonjwa na kupiga naye picha. Ila kwa kweli si fair kabisa. Wakati huu walipaswa kuwa watulivu na kuendelea kumuombea mwenzao ili apone haraka. Kuendelea kufanya dhihaka mbele ya mgonjwa kwa kupiga Selfie na kukenua meno hakika ni jambo la kusikitisha.
Niwaombe tu ndugu zangu wa BAVICHA. Wakati mwingine muwe mnafanya mambo ya kiutu uzima. Muwe mnakuwa basi japo kwa sekunde moja.