Lile swali kuhusu ile .mu.su. uliyokuwa umepewa ili umshughulikie Zito hivi umelijibuje kamanda. Ni hilo tuuu.Wanabodi
Habari za jumapili!?
Nimepita ktk ukurasa wa facebook wa Ben saa nane na kukuta ameanza kutoa majibu kwa wale waliomtuhumu.
----------------------------------------
"Ben Saanane Unafanya biashara gani na Ubalozi wa Sahara Magharibi"?
Nitatoa Ufafanuzi wa baadhi ya tuhuma ambazo zimesambazwa tangu wiki iliyopita kwenye mitandao na baadhi ya vyombo vya habari .Tuhuma nyingine binafsi sitazijibu hasa zile za kipuuzi. Zile tuhuma za yule anayeleta masuala ya kutooa sitazijibu.Sina muda wa kumjibu mbunge ambae anadhani kumchafua Ben Saanane (kwa sababu ya hasira zake fulani tu) atatibu changamoto zake kisaikolojia kwenye matatizo yake binafsi.Huyu bidada ni wa kuombea!Asitutoe kwenye mstari kwa sababu ya hasira zake binafsi za muda mrefu.
Wale wengine wa upande wetu,Nimewaacha baada ya kupata ushauri sana wa watu ninaowaheshimu.Watakapoendelea sitasita kwenda kinyume na ushauri wao.
Kuna tuhuma iliyozushwa kuanzia JamiiForums yenye kichwa cha habari "Ben Saanane Unafanya biashara gani na ubalozi wa Sahara Magharibi'?
Kisha watoa tuhuma wakaendelea kujenga hoja kuwa kuna fedha zaidi ya Shilingi milioni 12 ziliingizwa kwenye akauntii namba 01J1093293000. Na kwamba kiasi hicho cha fedha kililenga kutumika kulipa watu wanaodaiwa kuwa walitaka kuvuruga ziara ya mfalme Mohammed wa VI wa Morroco na pia kuuuhusisha ubalozi wa Algeria nchini na Kamati ya umoja wa Tanzania na Sahara Magharibi(TASSC).
Wasambaza tuhuma kwenye Mitandao na pia kwenye gazeti la serikali la Habari Leo waliendelea kulalama na kufanya jaribio la kupandikiza hisia kuwa wale waliokuwa wanakosoa ziara ya mfalme wa Morroco ni wasaliti wa nchi na wahujumu wa Uchumi .
Kwamba "Kuishambulia" serikali iliyonisomesha bure ni usaliti na hivyo napaswa kulipa gharama zilizotumika wakati wenzangu waliorudi nchini wanafanya kazi serikalini
Majibu yangu:
i)Sifanyi biashara yoyote na Ubalozi wa Sahara Magharibi
ii) Sina mkakataba wowote na ubalozi wa Sahara Magharibi.
Nina mkataba wa kufanya Consultancy na Balozi mbili za kigeni nchini na Taasisi nyingine mbili za kimataifa tangu mwezi uliopita kuhusiana na masuala ya kisiasa,kijamii,na Kiuchumi nchini sambamba na tathmini ya mwenendo wa haki za binadamu.
Maadili ya kazi yangu na hata Mkataba husika hauniruhusu kuzitaja balozi hizo .Ni suala la professionalism na uadilifu tu.
Ubalozi wa Sahara Magharibi sio miongoni mwa balozi hizo.Vyombo vinavyojiita vya dola kama vina ushahidi wa tuhuma zilizotolewa basi si vichukue hatua?
Balozi zote nchini na Mwenendo wa Mabalozi na maofisa wake huongozwa na mkataba Vienna na ni sehemu ya sheria za kimataifa. Tusichafue balozi na mataifa mengine kwa sababu tu kuna watu fulani wamezidiwa hoja na kuzua propaganda chafu.
iii) Kusomeshwa bure na serikali haimaanishi kuwa nilisaini mkataba wa kunilazimisha kufanya kazi na serikali nirudipo nchini bali kulijenga Taifa langu.Kufanya kazi nje ya serikali na nikaweza kuikosoa na kushauri ni sehemu ya ujenzi wa Taifa na wala silazimishwi kuipenda serikali ya chama cha Mapinduzi.Wapo watu ni watumishi serikalini lakini wanatuletea taarifa na madudu yanayofanyika huko.Vipi hao nao si wanaijenga nchi kwa staili yao? Hasira za nini?
iv) Kijana Noel Shao ambaye ni Afisa Mahusiano wa Kamati ya Umoja wa Watanzania na wapigania uhuru wa Sahara Magharibi baada ya kufanya mkutano na waandishi wa Habari pale Landmark Hotel,wakakosoa na kulaani ziara ile ya mfalme Mohammed.Baadae aliitwa Polisi na kushikiliwa kwa masaa kadhaa na kuhojiwa.Maswali aliyokuwa anahojiwa ni ya kufedhehesha na mengine yakimlazimisha kukiri kuwa wanatumiwa na vyama vya siasa
v)Tuhuma hizi za fedha ni mkakati maalumu wa kutaka kupandikiza mgawanyiko kwa wale wanaoungana kusimamia Doctrine ya Taifa letu kimataifa katika haki na uhuru wa kujitawala"Right to Self-Determination" ambayo mwalimu Nyerere amekuwa akihubiri kwa muda mrefu.
Lengo ionekane watu wanafanya hivi kwa maslahi yao wenyewe ili wengine warudi nyuma.Wameshindwa kujibu hoja za msingi wanaishia kuokoteza hoja na vioja vya kugawa watu na kuwatoa kwenye mstari .
Tanzania kuweka kisingizio cha Diplomasia ya uchumi kukiuka misingi inayokiuka misimamo yetu kwenye haki za binadamu haikubaliki na tutaikosoa hata kama Rais Magufuli(kwa uelewa wake finyu) kwenye maswala ya diplomasia ataendelea kujitetea kwa kauli za ajabu eti "Paka ni Paka ilimradi akamate panya".
Mwalimu Nyerere hakuwahi kuwa na mtazamo juu ya Makaburu kuwa 'Paka ni paka ilimradi akamate Panya".
Kipindi cha kupambana na makaburu aliwahi kujutia kuruhusu kampuni la De beers kufanya biashara ya almasi kule mwadui wakati ilikuwa imezuiwa.Ni kwa sababu ndilo lililokuwa na monopoly ya biashara ya almasi.
Pamoja na kuwa Nyerere alikuwa mwanamajumui(Pan-Africanist) lakini aliwatetea watu wa BIAFRA waliotaka kujitenga kule Nigeria kwa sababu walikuwa wakibaguliwa kama Wayahudi enzi za Hitler na chama chake cha NAZI.Pamoja na kuwa mkutano wa umoja wa Afrika(OAU) uliofanyika Misri kuwa na lengo la kumsulubisha aliwatuma akina Kawawa akaendelea kuwa na msimamo wake ndio maana hata wakati wa Vita na Idd Amin kwa hasira mtawala wa kijeshi wa Nigeria wakati huo Jenerali Olusegun Obasanjo alitoka nje ya Kikako cha OAU baada ya Nyerere kuanza kuongea.Hakutetereka.
Mwaka 1964 kwa sababu ya doctrine yetu ya kupinga Ukoloni na ukandamizaji,Rais Kwame Nkrumah aliwahi kumshambulia kwa maneno makali Nyerere kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika baada ya Tanzania kuchaguliwa kuwa Makao makuu ya kamati ya ukombozi ya Afrika
Nyerere alijibu kuwa yupo tayari makao hayo makuu yahamie Accra Ghana. Miaka 2 baadae Kwame Nkrumah mwenyewe alishindwa kujikomboa alipokabiliwa na uasi na kupinduliwa mwaka 1966.
Propaganda inayofanywa na Rais Magufuli,Serikali na vyombo vyake kuwa kuna nchi tulizowahi kuzisaidia lakini hazitusaidii ni propaganda ya ovyo kabisa na inayochekesha.
Baada ya Nelson Mandela kutoka Gerezani na kuwa Rais Mwaka 1994 huku Tanzania Rais Mkapa aliingia madarakani mwaka 1995 na sera yake ya ubinafsishaji.
Yeye na serikali yake walipigia chapuo kuuzwa kwa makamouni na hata mabenki kama NBC iliyouzwa kwa bei ya kutupwa .Hivi tunataka kuilaumu Afrika Kusini wakati Mkapa ndiye alikuwa kinara wa kupiga chapuo?
Hatuwezi kuacha kusimamia Principle zetu kimataifa kwa visingizio vya ajabu ajabu.Nyerere alisimama kidete hadi Umoja wa nchi huru wa Afrika ukaingiza kwenye mkataba wake azimio la haki za watu na binadamu mwaka 1981.
Fedha za Mfalme Mohammed VI wa Morroco ni fedha za damu.Ni fedha zitokanazo na machozi,jasho na damu za watu wa Sahara wanaoteswa na utawala ule wa kifedhuli kinyume na azimio namba 1514(1960) la umoja wa Mataifa juu ya kukomesha ukoloni.Fedha hizi haramu hazina tofauti na fedha za wauza madawa ya kulevya,Human trafficking,Ujangili na fedha zipatikanazo kwa uharamia.
Morroco imekalia na kuitawala Sahara Magharibi na kunyonya raslimali za nchi ile kisha tunaletewa na kujitapa "Paka ni Paka ilimradi anakamata panya".
Ni sawa na wauaji wa watu wetu wenye ulemavu wa ngozi kukata viungo au hata kuuwa kabisa kisha baada ya hapo wanaingia baa na kujitapa kuwa ilimradi ni fedha hatujali kwa sababu "Paka ni Paka Ilimradi anakamata panya"
Hazina tofauti na wale dada poa wanaojiuza halafu baadae wanajitapa na fedha ni fedha.
Bahati nzuri nae aliwatia aibu maana alivyopokelewa kwa heshima na mizinga 21 ya kijeshi,Red Carpet na Dhifa ya kitaifa kesho yake akaonekana anatangaza Mmea wa bangi na kuwa balozi wake nchini Zanzibar bila kuzingatia Sheria na tamaduni za watu wa zanzibar huku akiwa amekumbatia vimwana.Si mnasema Paka ni Paka ilimradi akamate Panya?
Visingizio kwamba mbona Zanzibar inanyonywa havihalalishi hili la Nchi moja kuikalia kimabavu bila hati yoyote ya kuungana (hata ya kimagumashi kati ya Tanganyika na Zanzibar)
Halafu tunaomba Sala ya Taifa eti "Mungu Ibariki Tanzania...."
Hakuna Mungu wa Unafiki na kuendekeza ufedhuli.
[HASHTAG]#MagufulihakikiPhDyako[/HASHTAG]
[HASHTAG]#MagufuliverifyyourPhD[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Freewesternsahara[/HASHTAG]
Aluta continua,Victory Ascerta...
Ben Saanane