Ben Mwangonda wa KHATCO Management

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,391
39,484
Kuna mtu yeyote anayemjua muhasibu huyu? Niko kwenye process ya kuconnect the dots na jinsi gani anahusiana na mtu yeyote in power? au anayejua hiyo kampuni ya Khatco?
 
Unaongeleza Mzee Apson na mwanae anaitwa Tom .Huyu Ben naye ni yupi ?
 
ah.. hiyo sijafikilia kama kuna uhusiano. Jina la huyu limeandikwa kama "Ben Mwangonda" na siyo "Mwang'onda". ndio maana nimeuliza mwenye kujua anipatie kwani ni muhimu sana....
 
Kuna mtu yeyote anayemjua muhasibu huyu? Niko kwenye process ya kuconnect the dots na jinsi gani anahusiana na mtu yeyote in power? au anayejua hiyo kampuni ya Khatco?

popcorn.jpg
 
Kuna mtu yeyote anayemjua muhasibu huyu? Niko kwenye process ya kuconnect the dots na jinsi gani anahusiana na mtu yeyote in power? au anayejua hiyo kampuni ya Khatco?

Sina hakika sana kama itafit kwenye dots zako, ila Khatco ni company ya mabus yaendayo kati ya Arusha na Kiteto (sijui kama bado inafanya kazi) Huyu mwenye bus ni mtoto wa mzee wa Mberesero aliyekuwa na anamiliki Ngorika. Jina la mmiliki wa Khatco ni Khatibu.

Watoto wengine wa huyo mzee Mberesero ni Oscar anayemiliki OSAKA bus Company, Charles anayemiliki (Chatco), na mwingine alikuwa anamiliki Kimotco jina simkumbuki
 
BowBow.. katika nyaraka ninazoangalia sasa hivi I can tell you this kuhusu hii Khatco and as far as I know SI kampuni ya mabasi.

KHATCO MANAGEMENT LTD
MANAGEMENT AND TAXATION CONSULTANTS
PO.BOX 2291
DAR-ES-SALAAM

ACCOUNTANT: BENJAMINI MWANGONDA

Clue: Je former Intelligence Chief ana mtoto yeyote mwenye jina hilo?
 
niliwahi kufanyanao kazi mara moja,kwenye mwaka wa 2000,walikuwa na ofisi yao pale kariakoo sikumbuki mtaa vizuri ila lilikuwa jengo jipya na wao walikuwa ground floor.nilideal na mzee mmoja wa kihaya na ilikuwa ni kazi ya siku mbili,ilikuifuatilia hii itabidi nifanye kazi ya ziada
 
Ben Mwangonda ninae mfahamu ni yule mtangazaji wa RTD unless kama majina yanafanana?
Aliwai kaa Japani kikazi on journalism for more than 4 years akarudi Tz kuendela na uwanahabari wake
 
Sijapata jibu ninalolitaka ambalo ni la kuridhisha.

Check na huyu mwandishi wa makala hii ya Tanzania Daima anazo full data, make katika hii habari kamtaja Ben Mwangonda.

Natumaini huyu jamaa itakupa mwanga wapi pa kuanzia
Shadowjumanne, 22 Januari 2008


Minara pacha Benki Kuu - Tanuri la uchumi wa Tanzania


na Aloyce Menda

MPANGO wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kujenga minara pacha inayoshabihiana na kupakana (twin-towers), kwa gharama inayozidi sh bilioni 430 na malipo ya sh bilioni 40 kwa kampuni ambayo haina ofisi yoyote, ni ufisadi wa kiwango cha juu.

Tunaambiwa leo hii na vyanzo vya habari vya kuaminika kwamba ujenzi wa minara-pacha hiyo na jengo la Benki Kuu huko Gulioni, mjini Zanzibar ni miradi iliyokwisha kugharimu zaidi ya sh bilioni 600.

Benki Kuu yenyewe ilitoa taarifa yake ya mwaka 2005/06 na kusema hadi Juni mwaka 2006 miradi hiyo ilikwisha kuchotewa sh 430,492,978,000 za walipakodi.

Taarifa za BoT zilisema miradi hiyo ilikuwa iliendelea kugharimiwa. Aidha, mwaka 2004/05 ujenzi huo ulikadiriwa kugharimu sh bilioni 238.59. Hii maana yake ni kuwa kipindi cha mwaka mmoja, gharama ziliongezeka zaidi ya mara mbili bila sababu za msingi.

Katika taarifa ya fedha ya mwaka 2004 ndani ya taasisi hiyo nyeti kwa uchumi wa nchi, minara pacha inayoendelea kujengwa ilikadiriwa kugharimu dola milioni 89.05 za Marekani (takriban sh bilioni 112). Gharama za sasa zimezidi tathmini ya awali kwa sh bilioni 300.

Kwa kutazama kumbukumbu za mnara wa PPF, jingo lililopo katika makutano ya mtaa wa Ohio na Pamba, liligharimu sh bilioni 19 hadi lilipozinduliwa rasmi Machi 20, mwaka 2001 na Rais mstaafu Benjamini Mkapa.

Jengo linalokadiriwa kugharimu fedha nyingi zaidi hapa nchini ni Umoja House, lilipo katika Mtaa wa Mirambo, jijini Dar es Salaam linalohifadhi ofisi za balozi tatu za Uingereza, Ujerumani, Uholanzi na Umoja wa Ulaya. Liligharimu sh bilioni 23 hadi lilipozinduliwa rasmi mwaka 2003.

Hii maana yake ni kwamba maghorofa pacha ya Benki Kuu yana gharama ya pesa mara 20 zaidi ya Umoja House na mara 30 zaidi ya mnara wa PPF.

Tunaambiwa na wataalamu wa ukadiriaji wa majengo kwamba sh bilioni 500 zilizokwisha kutumika hadi sasa kwa miradi ya ujenzi wa Benki Kuu zingetosha kujenga shule za msingi 1,000 kwa kiwango bora au shule 500 za sekondari. Sawa na kusema kila shule ya msingi itagharimu sh milioni 500 na sekondari itagharimu sh bilioni moja.

Kama Rais wa Tanzania wakati huo, Benjamin Mkapa angezuia miradi hiyo na kuamuru fedha hizo zitumike kwa shughuli za maendeleo, basi kila Mkoa wa Tanzania ungeweza kujengewa shule 20 za sekondari za kisasa au shule bora za msingi 40.

Aidha, fedha hizo zingetosha kujenga zahanati za kisasa 250 kwa gharama ya sh bilioni mbili kila moja.


Gavana Ballali

Miradi hiyo ya ujenzi na malipo tata kwa kampuni mpya isiyo hata na ofisi inayoeleweka yalipitishwa chini ya uongozi wa Serikali ya Rais Mkapa na Gavana Daudi Ballali.

Wafuatiliaji tulipoambiwa kuwa Ballali yu mgonjwa, tulifuatilia na kujua kwamba alikuwa jijini Boston, Massachusetts nchini Marekani, lakini jina la hospitali na aina ya maradhi vinafanywa siri hadi sasa.

Usiri kuhusu afya ya Ballali unaendelea, ingawa wapo wanaofuatilia kwa karibu mwenendo wa gavana huyo mgonjwa anayehusishwa kwenye ufisadi wa zaidi ya sh bilioni 133 za walipakodi.

Tuhuma hizo ziliisukuma serikali kwa shinikizo la nchi wahisani kuiagiza Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuajiri kampuni ya kimataifa kufanya uchunguzi kuhusu Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) iliyobainika kuwa kichochoro cha rushwa.


Ufisadi wa kutisha

Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, ililipwa mabilioni ya fedha za walipakodi mwaka 2005 kwa anuani za udanganyifu.

Uchunguzi umebaini kuwa anwani iliyotajwa katika usajili wa kampuni hiyo ni Kitalu namba 87 eneo la viwanda Kipawa, Wilaya ya Temeke, ni ya uongo, kwa sababu hakuna kitalu kama hicho katika ramani kuu ya Jiji la Dar es Salaam.

Habari za uhakika za uchunguzi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, zinatuthibitishia kwamba hakuna kitalu kama hicho popote.

Uchunguzi umethibitisha kwamba Kampuni ya Kagoda haikuwahi kuwa na ofisi popote na kwamba hata Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) haikuwahi kupokea malipo yoyote ya kodi kutokana na malipo ya mabilioni ya biashara isiyoeleweka.

Majina ya wamiliki wa kampuni hiyo ni John Kyomuhendo (hisa 40) na Francis William (hisa 60), ambao wote wana anwani moja (S. L. P. 80154, Dar es Salaam) na kutajwa kama wakazi wa jiji hilo.

Septemba 29 mwaka 2005, Kampuni ya Kagoda ilipewa cheti cha usajili namba 54040. Shahidi wake katika usajili ametajwa kuwa Benjamin Mwangonda, ambaye ni mhasibu wa Kampuni ya Khatco Management Limited.

Majukumu ya kampuni hiyo ni kufanya biashara ya kilimo na ukulima wa aina mbalimbali ya mazao ya kilimo kwa ajili ya chakula au biashara, ufugaji na maziwa. Pia itazalisha kuku, bata, bata-mzinga, kutengeneza jibini na mboga za majani kwa ajili na kuuza nje ya nchi.

Kagoda Agriculture Limited imesajiliwa pia kwa ajili ya kuuza nyama, mayai, kuku, vyakula vya kuku, dawa za mifugo na vifaa vya kufugia kuku, kuuza nje maua na kujenga nyumba mashambani, vyumba vya kupoozesha na barabara.

Kwa mujibu wa taarifa za Kampuni ya Ukaguzi wa Hesabu ya Deloitte & Touche mwaka 2006, ufisadi huo ulifanyika kwa mbinu kabambe za kughushi nyaraka mbalimbali za Benki Kuu ambayo ni muhimu zaidi katika sekta ya fedha na uchumi.

Mgogoro kati ya kampuni hiyo na BoT kuhusu madeni na malipo katika akaunti namba 99915091 01 ya benki hiyo, ulitokea katika kipindi kilichoishia Juni 30 mwaka 2006, huku akaunti hiyo ikiwa na sh bilioni 131.95.

Kutokana na maelezo ya kurasa nne kutoka Deloitte & Touche kwenda kwa Ballali ya Septemba 04 mwaka 2006, zilionekana kasoro katika malipo ya fedha hizo kwa Kagoda Agriculture Limited kama ifuatavyo:

Kwanza , kuna makubaliano 12 ya majukumu ya kutekelezwa kati ya Septemba 10, 2005 na Novemba 05, 2005. Muda huo ni mfupi kulipa wadai 12 dunia nzima.

Pili, makubaliano yote yalitiwa saini jijini Dar es Salaam mbele ya B.M. Sanze, ambaye ni wakili wa Mahakama Kuu.

Tatu, makubaliano matano yalifikiwa kwa kutiwa saini Oktoba 19, 2005 wakati makubaliano manne yaliwekwa saini Oktoba 18, 2005.

Hii inaonyesha kwamba wadai wa nje walisafiri na kuwahi kuweka saini zao katika makubaliano hayo katika muda wa siku moja.

Uchunguzi katika Idara za Uhamiaji unaweza kubainisha kama jambo hili liliwezekana lakini akili za kawaida zinakataa uwezekano huo.

Nne, kuna makubaliano mawili ya majukumu yaliyotiwa saini Oktoba 18 mwaka 2005 yakihusu kampuni mbili za Kijerumani (Lindeteves J Export BV na Hoechst) kuhusu malipo ya Euro 1,164,402.76.

Hata hivyo tarakimu zilikosewa na BoT iliandika barua kwa Kagoda Agriculture Limited kuelekeza kwamba malipo yatathiminiwe kwa fedha ya Kijerumani-Deutsche Marks.

Barua hiyo hiyo ilishauri kutolewa kwa kiasi cha sh 8,196,673,600.53 kwa Kagoda Agriculture Limited. Hatimaye wadai (Kagoda) waliwasilisha makubaliano mapya ya majukumu ya Novemba 03, 2005 siku mbili tu baada ya kuarifiwa.

Tano, tumebaini si kawaida na tuna mashaka makubwa kwamba wadai wa fedha wa nje wanaweza kufanya makosa ya kujichanganya hadi kusahau na kuweka saini katika makubaliano yenye aina ya fedha tofauti na wanazostahili kulipwa (Euro badala ya Deutsche Marks).

Juu ya hapo, inaonyesha udhaifu mkubwa kwa Benki Kuu kushindwa kufanya uchunguzi baada ya kubaini kasoro katika suala hilo.

Badala yake Benki Kuu hiyo hiyo ikaendelea na mchakato wa kutoa malipo makubwa kiasi cha sh bilioni 8.2 kwa wadai (kampuni tata ya Kagoda). Pia inashangaza ni vipi wakurugenzi wa Kagoda waliweza kurudi ghafla nchini katika kipindi cha siku mbili na kushughulikia marekebisho ya ghafla ya makubaliano. Hapo panahitaji uchunguzi katika Idara ya Uhamiaji kubaini safari za maofisa hao.

Sita, makubaliano yote 12 ya majukumu yanaonekana kuwa na lugha na maneno ya aina moja katika wadai wote wa kigeni.

Hili si jambo la kawaida kwani kampuni zisizohusiana haziwezi kutumia lugha inayofanana katika nyaraka zake.

Saba, hakuna makubaliano yoyote ya majukumu hayo 12 yaliyo katika karatasi zenye nembo za kampuni husika, wala anwani za kampuni husika au wawakilishi wake.

Nane, makubaliano yote yametiwa saini ukurasa wa mwisho na wawakilishi wa wadai 12 wa dunia nzima. Hili si jambo la kawaida, kwani nyaraka za kisheria huwa zinakuwa na sahihi kila ukurasa.

Tisa , mihuri ya moto (seal) katika nyaraka zote 12 inaonyesha kwamba inafanana na ya Kagoda Agriculture Limited. Uchunguzi umethibitisha kwamba watengenezaji wa mihuri yote 12 wanaweza kuwa 'wasanii'.

Kumi, kampuni tatu za Fiat Veicoli Industriali (kampuni ya Kitaliano), Valmet (Kampuni ya Marekani) na Adriano Gardella S.P.A (Kampuni ya Kitaliano ) zina mihuri ya moto inayofanana kabisa licha ya mikataba kuonyesha kwamba zinatofautiana.

Aidha, makubaliano ya Valmet, ambayo ni kampuni ya Marekani ni dola 2,398,439.96 lakini mkataba umesainiwa na Patrick Kevin, ambaye wadhifa wake katika kampuni hiyo ni mhasibu. Hii inashangaza.

Mkataba wa Daimler Benz AG umesainiwa na mkurugenzi aitwaye Christopher Williams. Cha ajabu saini inaonyesha herufi W. Christopher.

Kampuni kadhaa zilizotia mkataba zilikwisha kufungwa au kufutwa kama kampuni katika orodha ya usajili wa makampuni tarehe zinazoonyeshwa katika mikataba. Hiyo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa Kampuni ya Deloitte & Touche.

Mfano, Hoechst AG ilishabadilishwa kuwa Aventis mwaka 1999. Daimler Benz AG nayo ilishabadilishwa kuwa Daimler Chrysler AG mwaka 1998. Fiat Veicoli Industriali, ilishabadilishwa kuwa Industrial Vehicle Corporation (IVECO) January mosi, 1975.

Vilevile Mirrlees Blackstone iligeuzwa jina kuwa MAN B&W Diesel Limited kutoka Machi 2002, wakati Valmet ilibalidishwa kuwa Metso Paper toka Mei 10, 2000. Sasa inashangaza kabisa majina ya zamani ya makampuni haya kutumika katika mikataba inayohusu mabilioni ya fedha mwaka 2005.

Hakuna majina ya kampuni zilizopatikana katika majedwali zinazoitwa NS Boma na Lindeteves J. Export BV.

Simu zilizopigwa katika ofisi za makampuni yaliyotajwa katika mkataba zimerudisha majibu kwamba hazifahamu lolote kuhusu majina ya wawakilishi waliotia saini mikataba na Benki Kuu isiyoeleweka.

Barua kwa Gavana Ballali, kutoka kwa Samuel Sithole wa Deloitte & Touche nchini Afrika Kusini, inasema wazi kwamba "matumizi ya majina ya zamani ya kampuni na kasi ya ufanikishaji wa makubaliano na mikataba inathibitisha wazi kuwepo kwa ufisadi uliohusu maofisa waandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania." Kampuni ya Deloitte & Touche ilielezea pia mashaka yake kuhusu Kampuni ya Kagoda, ilivyoundwa Septemba 29, 2005 na kuweza kulipwa dola milioni 30.8 katika kipindi cha wiki tano hadi sita za kuundwa kwake.

"Hatuna taarifa zozote kuhusu uchunguzi wowote uliofanywa na Benki Kuu kuhusu kampuni hiyo. Ni vigumu pia kukubali kuwa kampuni hizo ziliweza kuingia mkataba wa malipo ya dola milioni 30 na wadai mbalimbali nchini Ujerumani, Italia, Yugoslavia, Uingereza, Ufaransa, Marekani na Japan kwa kipindi kifupi," inasema sehemu ya waraka huo.

Wakaguzi hao wa hesabu walimshauri Ballali kufanya ukaguzi wa haraka kwa kina na kusimamisha ajira za maofisa kadhaa wakati wa uchunguzi kuepuka kuharibiwa ushahidi wa nyaraka katika mafaili muhimu.

Hata hivyo, hadi leo hakuna ofisa wa BoT aliyesimamishwa ajira yake kuhusiana na suala hilo zaidi ya Ballali, aliyetenguliwa na rais Kikwete baadaya ukaguzi wa mwaka 2005/06 uliofanywa na Kampuni ya Ernst & Young.


Nyerere angekuwapo…

Mpango wa BoT kujenga minara pacha ni wa zamani, ingawa utekelezaji wake ulianza rasmi mwaka 2000. Kwa hakika ni mtiririko wa tabia ya viongozi wa serikali, kampuni na taasisi za nchi fukara 'kuiga tembo kunya' bila tafakari za kina kuhusu umuhimu na faida za miradi kama hiyo.

Alipochaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza Tanzania Oktoba 1995, Rais Mkapa, alikuta mpango huo ukisubiri utekelezaji wake.

Uongozi wa BoT wakati huo, chini ya Gavana Idriss Rashid, uliishauri serikali kuutekeleza lakini ukakataliwa kwa madai hali ya uchumi haikuwa nzuri na kwamba serikali ilikuwa na mambo mengine muhimu zaidi ya kutekeleza.

Ombi la Benki Kuu la kutaka ujenzi wa minara pacha lilikataliwa na Mkapa kabla ya kifo cha Mwalimu Nyerere, Oktoba 1999, kwa sababu Mwalimu asingevumilia kuona ujenzi wa gharama wakati watu wake ni fukara wa kutupwa.

Hakuna shaka Mwalimu angekuwa hai angewakumbusha viongozi wa serikali ile dhana kongwe ya 'Kupanga ni Kuchagua'.

Dhana hii huenda ndiyo dhana kuu kati ya zote alizowahi kuhimiza Mwalimu Nyerere. Maana halisi ya dhana hii ni kuhimiza umakini katika kupanga matumizi ya pato la taifa ili kutoa kipaumbele (priority) kwa mambo muhimu zaidi.

Mwalimu Nyerere, aliamini kuwa heri maskini huru kuliko tajiri mtumwa. Kwa mara ya kwanza alitoa dhana ya 'Kupanga ni Kuchagua' katika mkutano mkuu wa TANU, Mei 28, 1969.

Hakuna shaka kwamba Mwalimu Nyerere angekuwa rais leo, asingeruhusu ujenzi wa minara hiyo, ununuzi wa ndege ya kifahari kwa ajili ya rais na rada ya kijeshi isiyoweza kumulika masafa marefu.

Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa Media Institute for Sustainable Development in Africa (MISDA).

Barua pepe: mendaloycetz@yahoo.com
 
Shadow.. huyo ananukuu kitu ambacho na mimi ndiyo chanzo changu. Wote tunaangalia document hiyo hiyo. Hivyo hatoi jibu.
 
Mwanakijiji,

nimekupata hapo. Basi ngoja jamaa wakiamka huko Bongo lazima tutapata hizo data za huyu Ben Mwangonda. Make kama ni muhasibu na vyuo vyetu vichache lazima classmate wake watashusha data.

Shadow.
 
Mi ninamfahamu sana ila ni mshkaji siwezi kutoa habari zake. Nitamshauri aje humu mwenyewe!
 
Mkuu GT.Tafadhali jaribu kuwa makini na mambo unayoyafanya,mzaa kila mara utakupunguzia heshima mbele ya jamii.
 
Mi ninamfahamu sana ila ni mshkaji siwezi kutoa habari zake. Nitamshauri aje humu mwenyewe!

Sawa kaka, ila kwa ufahamu wangu hata yeye ameshangaa sana jinsi wapelelezi wa EPA walivyokwepa kwenda kumhoji yeye na mabosi wake wadosi pale katika ofisi zao. Kuna mtu anasema hata wao wana hasira sana kwa kuwa hilo dili wao haliwahusu japo mhusika amewahi kuwa mteja wao mkuu mara kadhaa katika mambo yanayohusu 'mazagazaga'. Benjamin Mwang'onda huyu wa Khatco hana uhusiano na Tom Mwang'onda na kwa maana hiyo hana uhusiano na Apson kama iliovyotajwa huko nyuma. Hii haimuondoi Apson na kundi lake katika KAgoda.

Kwa ufupi ni kwamba dola haijaamua kuwashughulikia Kagoda kwa kuwa wanawafahamu bila shaka yoyote wahusika na wana ushahidi wote pasi shaka wa wahusika wote na tena nashangaa sana hata baadhi yao wametajwa katika orodha ya mashahidi watakaosimama upande wa serikali (mashitaka). Ama kweli bado TUNAZUGWA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom