streetwiser
Member
- Jul 11, 2008
- 30
- 3
Mkuu Phillemon Mikael Musiba nae ni mtu wa kugandamizia sana soma vitabu vitatu James hadley chase kisha niambe, hivyo usimfananishe na Marahemu Mtobwa (RIP).
R.I.P Ben!
Philemon Mikael mastaa wao ni : Ben (Joram Kiango, Neema Idd), vs Musiba (Willy Gamba, Maselina)
Taifa limepoteza kinara mwingine wa kutumia fasihi andishi kufunda jamii yetu. Majumaa kadhaa yaliyopita nilimwona Ben Mtobwa aka Joram Kiango pale kwenye Mkahawa wa Vitabu wa Soma akipanga mikakati ya uandishi na uchapishaji. Kwa wale mnaohitaji vitabu vyake basi msiwe na shaka maana vinapatikana kwa wingi kwenye maduka ya vitabu hasa ukizingatia kuwa Ben alikuwa anatoa matoleo mapya ya vitabu hivyo kupitia kampuni yake ya uchapishaji ijulikanayo kama Heko Publishers. Tumuenzi kinara huyu kwa kuvirejea vitabu vyake na kuvisoma 'katikakati ya mistari' tuvumbue nini hasa kiko 'nyuma ya mapazia' aliyokuwa anajaribu kuyafunua!
"Mpenzi Leo Nitakuletea Nunda" - Joram Kiango akimwambia Binti Mrembo aliyemchunuku na ambaye kumbe alikuwa ndio Nunda Mwenyewe!Kweli Kikulacho Ki Kinguoni Mwako!
Mkuu Companero, vinapatikana katika maduka gani? Tafadhali tutajie maduka hayo.