Ben Msuya: Askari Mtanzania aliyepata kuongoza Uganda

Ni Maj.Gen.Benjamin "Ben" Msuwakati huo akiwa na cheo cha Lt.Col.

Ndiye aliyeongoza kikosi vya JWTZ kilichotwaa jiji la Kampala.

Huyu ndiye aliyelazimika kulidhibiti jiji la Kampala na Ikulu ya Uganda wakati akisubiri kuwasili Raisi mpya wa Uganda, Prof.Yussuf Kironde Lul

Watanzania hatuna habari na shujaa huyu, lakini gazeti la Monitor la Uganda walimtafuta na kufanya naye mahojiano.

Soma hapa chini.

SOURCE:
Musuya: The Tanzanian general-- who ruled Uganda for three days - Special Reports

cc Manyerere Jackton, Pasco, Ben Saanane, ZeMarcopolo, Mag3, Chademakwanza, Mzee Mwanakijiji, Echolima, Nguruvi3, Ritz
Huo ni uongo mkubwa pamoja na ukweli kuwa Msuya wakati huo alikuwa askari kwenye brigedi ya kwanza kuingia na kuteka Kampala.

Wakati huo Amin Alikuwa bado yuko Uganda sehemu za Arua ma Gulu kaskazini mwa nchi. Na Amin alikuwa akitumia mobile radio broadcasts kudsi kuwa bado ni kiongozi wa Uganda.

Msuya alikuwa captain au Meja wakati huo huko nyuma majenerali wakiongoza movement ya vikodi vingine.

Mkuu,kutawala na kuteka ni vitu viwili tofauti!!!
 
Hakuna kitu kama hicho kwenye nchi za wenzetu kila operation inaandikwa na kuelezewa kiufasaha kabisa ila si Tanzania.

Mkuu,

Nchi nyingi sana zina sheria ya kuzuia askari aliyetoka kwenye combat mission kusimulia waliyo yafanya!Huwa wanapewa miaka fulani hadi ipite ndipo waseme yote.

Nina imani ipo siku makamanda watakao kuwa hai watatueleza yote fichika kuhusu vita vya Uganda hasa kama ni kweli Idd Amin alituvamia au ilitafutwa tu chanzo Nyerere aivamie Uganda amrudishe madarakani rafiki yake Obote?
 
Hakuna kitu kama hicho kwenye nchi za wenzetu kila operation inaandikwa na kuelezewa kiufasaha kabisa ila si Tanzania.

Kuna classified na unclassfied information za vita.Zile unclassfied huruhusiwa kuandikwa.Ujue vitani kuna maeneo hata waandishi wa habari huruhusiwa kuwepo lakini kuna maeneo ni wapiganaji tu huwa maeneo hayo.yale open huwa yanaruhusiwa kuandikwa kama progress report kwa umma ya vita na yaweza andikiwa hata vitabu vita ikiisha.

Lakini si yote
 
huo ni uongo mkubwa pamoja na ukweli kuwa msuya wakati huo alikuwa askari kwenye brigedi ya kwanza kuingia na kuteka Kampala.

Wakati huo amin alikuwa bado yuko uganda sehemu za arua ma gulu kaskazini mwa nchi. Na amin alikuwa akitumia mobile radio broadcasts kudsi kuwa bado ni kiongoxi wa uganda.

Msuya alikuwa captain au meja wakati huo huko nyuma majenerali mwskiongozamovement ys vikodi vingine.

Mkuu,kutawala na kuteka ni vitu viwili tofauti!!!
umekuja na povu la hatari kama umetumwa duhh!!
-hebu rudia kuisoma vizuri mstari wa pili tokq chini mwa posti yako??
 
Mkuu East African Eagle vita vya Iraq makamanda wengi wa USA wameandika habari nyingi sana tena kwa undani.Operation Osama makamanda wameandika habari nyingi sana tena kwa undani.Sisi bado tunaendesha mambo kizamani.Leo ukienda wikipedia ukitafuta majina na wasifu wa makamabda wetu utashangaa hakuna.Rwand anchi ndogo kama wilaya ya Kinondoni utashangaa wameweka habari nyingi sana za makamanda wake.

Kuna classified na unclassfied information za vita.Zile unclassfied huruhusiwa kuandikwa.Ujue vitani kuna maeneo hata waandishi wa habari huruhusiwa kuwepo lakini kuna maeneo ni wapiganaji tu huwa maeneo hayo.yale open huwa yanaruhusiwa kuandikwa kama progress report kwa umma ya vita na yaweza andikiwa hata vitabu vita ikiisha.

Lakini si yote
 
Last edited by a moderator:
WaTanzania kwa ubishi siwawezi yaani unataka tukuamini wewe ambaye wakati wa vita pengine ulikuwa shule ya msingi,tudharau alichosema Maj Gen Msuya.

Huo ni uongo mkubwa pamoja na ukweli kuwa Msuya wakati huo alikuwa askari kwenye brigedi ya kwanza kuingia na kuteka Kampala.
Wakati huo Amin Alikuwa bado yuko Uganda sehemu za Arua ma Gulu kaskazini mwa nchi.
Na Amin alikuwa akitumia mobile radio broadcasts kudsi kuwa bado ni kiongoxi wa Uganda.

Msuya alikuwa captain au Meja wakati huo huko nyuma majenerali mwskiongozamovement ys vikodi vingine.

Mkuu,kutawala na kuteka ni vitu viwili tofauti!!!
 
vita vya Iraq makamanda wengi wa USA wameandika habari nyingi sana tena kwa undani.Operation Osama makamanda wameandika habari nyingi sana tena kwa undani.Sisi bado tunaendesha mambo kizamani.Leo ukienda wikipedia ukitafuta majina na wasifu wa makamabda wetu utashangaa hakuna.Rwand anchi ndogo kama wilaya ya Kinondoni utashangaa wameweka habari nyingi sana za makamanda wake.

Nchi ziko tofauti ndio maana zina majina tofauti na watu tofauti na utendaji tofauti.Tanzania is not a copy cat to copy EVERYthing done anywhere.That is why it is called Tanzania and not USA or RWANDA.
 
[video]http://www.jewsnews.co.il/2015/05/21/the-hand-of-g-d-in-the-6-day-war/[/video]
Habari kama hii ilitolewa mapema sana na waandishi wa habari waliipewa tatizo sisi tuna Treat vingi sana kama kuhatarisha Usalama wa Taifa wakati hii ni Historia jambolenyewe tayari limekwisha pita.
 
WaTanzania kwa ubishi siwawezi yaani unataka tukuamini wewe ambaye wakati wa vita pengine ulikuwa shule ya msingi,tudharau alichosema Maj Gen Msuya.

Mkuu Ngogo usisubiri ya kuambiwa, sisi wengine tulikuwepo na tafuta kitabu kilichoandikwa na Tony Arvigan, The War in Uganda.

Tatizo lenu mnaamini kila muambiwacho kuwa ni ukweli. Kampala inspotekwa Idi Amin alikuwa NDANI ya Uganda and thats a fact.

Sasa story za ati Msiya katawala Uganda ni hock pock, Msuya alikuwa katika kikosi kilichoingia na kuteka Kampala, thats the fact.
Soma sana ujiridhishe.
 
Wana siasa ambao hawajaifanyia lolote nchi hii ndiyo wanaongoza kufaidi keki ya Taifa!

Mafao ya akina Zitto,Kafulila,Makamba,Ridhiwani,Mnyika,Lema na wengineo ni MAKUBWA zaidi ya nashujaa kama Brig Msuya na RIP Brig Lupembe

Inauma sana kwa kweki!
Hii post imenigusa zaidi ya post yoyote hapa JF katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita!

Huo ni uongo mkubwa pamoja na ukweli kuwa Msuya wakati huo alikuwa askari kwenye brigedi ya kwanza kuingia na kuteka Kampala.
Wakati huo Amin Alikuwa bado yuko Uganda sehemu za Arua ma Gulu kaskazini mwa nchi.
Na Amin alikuwa akitumia mobile radio broadcasts kudsi kuwa bado ni kiongozi wa Uganda.

Msuya alikuwa captain au Meja wakati huo huko nyuma majenerali wakiongoza movement ya vikodi vingine.

Mkuu,kutawala na kuteka ni vitu viwili tofauti!!!

Hapana mkuu alicho andika JokaKuu ni kweli tupu!

Lt Col Msuya alikuwa na cheo vha Major wakati vita vinanza lkn Mwl Nyerere akampandisha cheo katikati ya vita hivyo sambamba na maafisa wengine kama Brig Chitete toka Kanali,Kanali Yunus Abdallah toka Lt Col,Kanali Rajabu Rajabu Rajabu toka LtCol na wenginei wengi!

Historia pia inaonyesha kuwa Lt Col Msuya ndiyo kamanda wa kwanza kuongoza vikosi vya JW kuingia Kampala kumsaka Amin

Kambi yake aliiweka ktk mtaa wa KALISIZO wakatwaa Radio ya Uganda na baadae akaelekea Hospital ya Mulago na Mengo kuona wapiganaji wake walio jeruhiwa!
 
Last edited by a moderator:
tatizo kubwa sana ambalo lilisababisha watu wengi sana wasiweze kuandika au kutoa habari hasa ni uelewa katika jambo hili wengine waliona wakiandika au kuelezea chochote kuhusu vita vya kagera kunaweza kuhatalisha usalama wa taifa kitu ambacho si kweli jambo lingine ambalo wengi walihisi na kuhofu kuwa kandika au kutoa maelezo yoyote kuhusu tukio lolote la kijeshi ni sawa na kuuweka usalama wa taifa matatani maana msemaji wa jeshi ni jeshi lenyewe.pia jeshi lenyewe halikuwa na utamaduni wa kuweka kila kumbukumbu ya askari wake wadogo kwa wakubwa wazi(public) hii pia imechangia kiasi kikubwa sana mashujaa wetu wengi walipopoteza maisha yao jamii kwa ujumla iliwasahau kabisa sababu hakuna kumbukumbu zao kwenye tovuti ya jwtz hata uki-google huwezi pata.ingawaje majeshi mengine duniani huwa yana utamadumu wa kuweka kumbukumbu kwenye tovuti zao.
vita hii nimepoteza ndugu watano 5 na hata majina yao hayapo ubaoni.
 
Mkuu Ngogo usisubiri ya kuambiwa, sisi wengine tulikuwepo na tafuta kitabu kilichoandikwa na Tony Arvigan, The War in Uganda.

Tatizo lenu mnaamini kila muambiwacho kuwa ni ukweli.
Kampala inspotekwa Idi Amin alikuwa NDANI ya Uganda and thats a fact.
Sasa story za ati Msiya katawala Uganda ni hock pock, Msuya alikuwa katika kikosi kilichoingia na kuteka Kampala, thats the fact.
Soma sana ujiridhishe.

Nimenunua vitabu hivi 2 right away nisome vyema,nitamaliza baada ya weeks 2 zijazo anayetaka kuazima ani PM!

Nashukuru sana masopakyindi
 
Attachments

  • 1432296844635.jpg
    1432296844635.jpg
    53.1 KB · Views: 231
  • 1432296892811.jpg
    1432296892811.jpg
    64.6 KB · Views: 231
Last edited by a moderator:
Hivi hakuna mtu anayeweza kuanzisha project ya kudocument vita ya Kagera vizuri naamini kitabu kama hicho kitalipa sana, bado askarina makamanda wengi walioshiriki vita hiyo wako hai, japokuwa kukosa maandiko au maelezo kutoka kwa makamanda kama hawa wliokwishafariki (Maj. Gen. Silas Mayunga, Maj. Gen.Mwita Marwa,, Maj. Gen. John Warden) ni mambo mengi yatakuwa yamekosekana.
 
kukosa maandiko au maelezo kutoka kwa makamanda kama hawa wliokwishafariki (Maj. Gen. Silas Mayunga, Maj. Gen.Mwita Marwa,, Maj. Gen. John Warden) ni mambo mengi yatakuwa yamekosekana.

Yatakuwa yamekosekana uraiani lakini Jeshini yapo kwa matumizi ya jeshi tu.
 
Kuna huyu capt:robert wa mapinduzi mfu ya 1983&84 huwa akianza kuelezea harakati za hii vita umaweza kubaki mdomo wazi!!
--hasa pale ilipotumika nguvu ya ziada toka kwa sir god#
#msuguli ,msuya na komando john nyerere ilikuwa sehemu ya kivutio kikubwa kwa kila mwanajeshi…

Hapa ndipo wanajeshi kutoka znz huwa wanaaminika zaidi.
 
Ni bahati mbaya kuwa mashujaa walioongoza vita vya Kagera hawajaandika simulizi ya vita ile ili kuweza vizazi vingine kuisoma na kujifunza. Hata hivyo kuna simulizi nzuri imeandikwa kupitia kitabu: War on Uganda kilichoandikwa na waandishi habari Tony Avirgan na Martha Honey ambao wakati wa vita hivyo walifuatana na kikosi kilichokuwa kikiongozwa na Ben Msuya.
 
Huo ni uongo mkubwa pamoja na ukweli kuwa Msuya wakati huo alikuwa askari kwenye brigedi ya kwanza kuingia na kuteka Kampala.
Wakati huo Amin Alikuwa bado yuko Uganda sehemu za Arua ma Gulu kaskazini mwa nchi.
Na Amin alikuwa akitumia mobile radio broadcasts kudsi kuwa bado ni kiongozi wa Uganda.

Msuya alikuwa captain au Meja wakati huo huko nyuma majenerali wakiongoza movement ya vikodi vingine.

Mkuu,kutawala na kuteka ni vitu viwili tofauti!!!

..I see ur point.

..labda tuseme Msuya "alitawala" au "aliongoza" Uganda.

..pia ukumbuke source ya habari hizi ni waandishi wa Uingereza Tony Avirgan na Martha Honey walioandika kitabu "War in Uganda --The legacy of Idi Amin." Hawa waandishi walikuwa embedded ktk majeshi ya Tz yaliyoingia Uganda.

..halafu hata huyu mwandishi wa The Monitor gazeti la Uganda naye ameandika habari hiyohiyo baada ya kumhoji Maj.Gen.Ben Msuya.

..kwenye kitabu cha hao Waingereza, wanasema Ben Msuya alikuwa na cheo cha Lt.Col na ndiye aliyeongoza kikosi cha JWTZ kilichoteka jiji la Kampala. Nadhani hilo halina ubishi.

..hii habari haitakuwa na maana kwako bila kwanza kuelewa mambo yafuatayo: 1. kutekwa kwa jiji la kampala na kukimbia kwa Iddi Amin; 2. Oyite Ojok kutangaza kuwa Amin amepinduliwa; 3. vikao vya Waganda vilivyokuwa vikifanyika Moshi kuunda serikali ya mpito na kumteua raisi wa mpito; 4. Prof.Yussuf Lule kuapishwa kuwa raisi wa mpito wa Uganda.

..Iddi Amin hakuwa replaced moja kwa moja, kulipita muda fulani tangu Amini aondoke Kampala, na Prof.Yussuf Kironde Lule kuapishwa kuwa raisi. Sasa tangu Amin akimbie na Lule aapishwe, Lt.Col.Ben Msuya alikuwa incharge wa masuala yote Kampala, na ndiyo maana kuna wanaosema "alitawala" au "aliongoza" Uganda.

NB:

..umesema kweli. Baada ya tangazo la Oyite Ojok, Iddi Amin alitangaza redioni kwamba bado ni raisi wa Uganda.

cc Malafyale, Echolima, MK254, Nguruvi3, Kichuguu
 
Back
Top Bottom