Ben Kiko yu wapi jamani?

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,020
576
Ben Kiko kuna kipindi alinifanya nisipende kumiss kipindi cha MAJIRA cha RTD enzi hizo hasa akiwa stesheni ya Dodoma na kisha akahamia Tabora. Taarifa zake zilikuwa na misisimko sana hata watu wengi walifika mahala akimaliza kuongea yeye wanafunga redio kuashiria kipindi kimekwisha siku hiyo. Sijamsikia muda mrefu sana, yuko wapi?????

Ben Kiko alijaliwa kipaji cha kuwavuta wasikilizaji wake na kuwapa haja ya mioyo yao kusikiliza habari. Wakati huo huo kuna mtu ambaye sikutamani hata kusikia sauti yake redioni kwa sababu ya kutangaza habari hasi tu kutokea vituo vya polisi kwa RPC Mbeya (Martha Ngwira) naye hasikiki tena. Au ......??? Tusiseme sana huenda walisharudisha mafaili...... (Mungu anisamehe).
 
Leka umenikumbusha mbali dah, yeah once upon a time in Mazindarani existed a man by the name of Ben Kiko.....
 
Jamani Kiko.... wanamfaidi sana watu wa Tabora. Angetafuta kibarua moja kwa moja RFA au TBC1 au Radio 1 mambo yangekuwa poa sana.
 
Kuna siku alikuwa anatangaza habari za sakata la mwizi wa mfukoni akasema.

."mshitakiwa huyo aliyekuwa na viraka viwili matakoni, mithili ya macho ya bundi, alipandishwa kizimbani akiwa amepigwa sawia"...

Basi vijimaneno vyake vilikuwa na ucheshi mwingi uliomfanya kila msikilizaji kuvutika kusikia alichosimulia!
 
Nasikia wakati wa vita vya nduli alikwenda riport Bukoba sasa watanzania tukawa tunachapwa vilivyo yeye akaripoti hivyo hivyo hakuchuja habari, RTD wakaona noma hii wakamrudisha Dodoma. lkn jamaa alikuwa ana kipaji cha kazi yake.
 
Kuna nyingine aliwahi kusema " kijana yule aliyepigwa teke katikati ya magoti na kitovu alikuwa amelala haoi mithili ya mfu.
 
Nasikia wakati wa vita vya nduli alikwenda riport Bukoba sasa watanzania tukawa tunachapwa vilivyo yeye akaripoti hivyo hivyo hakuchuja habari, RTD wakaona noma hii wakamrudisha Dodoma. lkn jamaa alikuwa ana kipaji cha kazi yake.

Umenikumbusha mbali bwana huyu alikuwa mtangazaji mahiri wa vita vya Kagera
 
Kuna siku alikuwa anatangaza habari za sakata la mwizi wa mfukoni akasema.

."mshitakiwa huyo aliyekuwa na viraka viwili matakoni, mithili ya macho ya bundi, alipandishwa kizimbani akiwa amepigwa sawia"...

Basi vijimaneno vyake vilikuwa na ucheshi mwingi uliomfanya kila msikilizaji kuvutika kusikia alichosimulia!
.....viraka viwili matakoni...mithili ya nani vile? Journalism at its best. kwi!kwi!
 
...na walipompeleka Dodoma, wala hakukata tamaa, aliiboresha sana RTD hasa kipindi cha michezo, enzi hizo CDA walikuwa mwiba mkali katika ligi ya bara.

Alinifurahisha sana pale anapomalizia kuripoti habari za michezo kwa kusema "huyu ni Ben Kiko, michezo, Dodoma"
 
Umenikumbusha mbali bwana huyu alikuwa mtangazaji mahiri wa vita vya Kagera
Mama vipi ulikuwepo wakati wa vita ya Kagera na kushuhudia? Dah, basi we mtu mzima. Heshima yako. Niliwahi kwenda TBR kipindi fulani nikamsikia Kiko Ben yuko Tabora VOT radio ndo alikokuwa anatangaza. Nadhani atakuwa huko bado. Huyu mtu mzima ailikuwa safi best!
 
Aliwahi kutangaza vile vile" Vijana hawa wa kike na wa kiume wakiwa na mashati meupe kama yange yange walishuka moja moja na kuunda mistari miwili kama njia ya train kwenda ofisi ya waziri mkuu kutoa dukuduku lao".
 
Mama vipi ulikuwepo wakati wa vita ya Kagera na kushuhudia? Dah, basi we mtu mzima. Heshima yako. Niliwahi kwenda TBR kipindi fulani nikamsikia Kiko Ben yuko Tabora VOT radio ndo alikokuwa anatangaza. Nadhani atakuwa huko bado. Huyu mtu mzima ailikuwa safi best!

Nimeipokea .Vita hii niliishudia kwa macho yangu wakati huo nilikuwa kanda ya ziwa .Usiombe kuona vita labda usimuliwe tu.
 
Watangazaji wa sasa hata hawana mvuto kama huyu jamaa!

...hujamsikiliza Ephraim Kibonde?...hujui ni kiasi gani vipindi vyake vilivyo na mvuto kwa wasikilizaji. Ingekuwa nchi za magharibi dogo angekuwa booonge la Celebrity-Broadcaster.

Ben Kiko enzi hizo saa tatu usiku, kipindi cha majira hatupitwi! ...Ingefaa sana 'wadhamini' wakafanya matamasha kuwaenzi watangazaji hawa mahiri wa enzi zile kwa mchango wao kwa taifa...

Enzi zile ambapo habari zilikuwa zatokea RTD kwa kina David Wakati, Ben Kiko, Jacob Tesha, Ahmed na Sango Kipozi, Mshindo Mkeyenge etc etc

The Legends!
 
Kuna wakati nilimuona Mwanza kawa mtu mzima siku hizi na utangazaji wake sio kama wakati ule alipokuwa kijana ssi unajua tena umri ukipita unawaza upate hela ya kula tu tofauti na ukiwa kijana unafanya kazi ili upande nngazi na upate umaarufu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom