Bella adaiwa kuiba wimbo BSS

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,072
1,250
Hali ndani ya jumba la ‘Kili BSS’ imeanza kuwa ya ubishani kutokana na baadhi ya washiriki kutaka mwenzao Christabella Kombo aondolewe mjengoni. Sababu ya kumchongea mwenzao Christabella, ni tuhuma kwamba aliiba wimbo wa watu wenye maudhui ya ukimwi na kujifanya kuwa ni wake, jambo ambalo limewakera kwavile wao walihangaika usiku mzima wakitunga nyimbo zao za ukimwi wenyewe kama walivyotakiwa na mmoja wa wadhamini, FHI.
Wakiwa katika mahojiano na `Maza House', washiriki hao walisema Christabella maarufu kwa jina la `Bella', aondolewe kwa wizi wa wimbo huo waliodai ameukwapua kwa kundi la THT.
Washiriki tisa kati ya 10 wanaoendelea kuishi katika nyumba hiyo, walimuelezea `Maza House' kuwa hawako tayari kuona mwenzao anafanya ujanja ili kukomba zawadi ya wimbo huo na pia ni bora aondoshwe mjengoni.
Hata hivyo, Bella alijitetea mbele ya Maza House kuwa wimbo huo ni mali yake na aliutunga wakati akitayarisha albamu yake ya injili ambayo bado hajarekodi.
Chiby ambaye tayari amekiri kwa Maza House kuwa anajihisi kumzimia Bella kuliko kawaida, alimwambia Maza House kuwa hoja zinazotolewa na washiriki wenzake zinatokana na majungu na fitna baada ya kugundua mrembo huyo ni mkali katika uimbaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom