Belarus yafungia tovuti ya Deutsche Welle

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Mamlaka nchini Belarus imefungia tovuti ya shirika hili la utangazaji Deutsche Welle, DW, linalomilikiwa na serikali ya Ujerumani. Haya yametangazwa leo na shirika hili katika makao yake makuu mjini Bonn.

Utangazaji kwa lugha zote 32 za shirika hili umefungiwa katika taifa hilo pamoja na tovuti nyingine za habari.

Kulingana na tovuti ya DW, wizara ya habari ya Belarus ilihalalisha hatua hiyo na kusema kwamba maudhui ya DW zilihusisha masuala yaliyoorodheshwa kuwa ya itikadi kali na mahakama za nchi hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa DW Peter Limbourg ameuita uamuzi huo kuwa "wa kushangaza" na kuitaja hatua hiyo kama mahangaiko ya mamlaka nchini humo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani nchini Belarus, amesema kuwa balozi wake ametuma ombi la maelezo kwa wizara ya mambo ya nje ya Belarus na kutaka kufunguliwa kwa tovuti hiyo.
 
Back
Top Bottom