Beki wa Simba Che Malome,siku ya tarehe 05.11.2023 wakati wanakandwa kichapo cha mbwa mwizi kutoka kwaa watani zao Yanga, alionyeshwa kadi mbili za manjano.
Kitu ambacho kilipaswa kupewa card nyekundu, lakini refa na wasaidizi wake hawakuliona hili sijui hawakuwa na kumbukumbu vizuri, Che Malome hakutoka nje kwa adhabu ile, alicheza tu.
Juzi kati, kati ya Mechi ya Simba na Namungo,Che Malome alicheza tena, Simba walimchezesha mchezaji mwenye card nyekundu kwa sababu zipi?
Bodi ya Ligi mko wapi? TFF mko wapi? Wapeni Namungo ushindi wa point tatu na magoli mawili kama kanuni inavyotamka.

- Tunachokijua
- Kuna mjadala unaendelea mitandaoni na pia mdau wa JamiiForums.com amehoji kama ni kweli kuna mchezaji wa Simba, Che Fondoh Malone alipewa kadi mbili za njano na akaendelea kucheza katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, Jijini Dar es Salaam, Novemba 5, 2023.
Uhalisia ulivyo
Dakika ya 22, mchezaji wa Simba, Fabrice Ngoma alimchezea faulo Stephane Aziz Ki wa Yanga, Refa akapuliza filimbi wakati huo Che Malone alikuwa anaenda kuupiga mpira, kisha akasogea kwa refa kulalamika akidai haikuwa faulo.
Wakati Mwamuzi anatoa kadi ya njano kwa Ngoma, aliyekuwa karibu ni Che Malone akilalamika, hivyo kadi ilienda kwa Ngoma na si Che Malone kama inavyodhaniwa.
Hata hivyo, Dakika ya 85, Wakati Yanga imepata penati, Che Malone akawa anaonekana analalamika muda mrefu kwa Mwamuzi akilalamikia uamuzi wake, ndipo Mwamuzi akageuka na kumpa kadi ya njano Che Malone.
Hivyo, si kweli kuwa Che Malone alipewa kadi mbili za njano ndani ya mchezo.
Mchezo huo wenye kubeba hisia za wapenzi wengi wa Soka ndani na nje ya Tanzania uliisha kwa Simba kupokea kipigo kikali cha goli 5-1.
Kwa mujibu wa tovuti ya michezo ya Goal.com, mchezo kati ya Simba na Yanga upo kwenye orodha ya mechi zenye upinzani mkubwa zaidi Afrika (Derby), ambao hufahamika zaidi kama "The Kariakoo Derby"
Mashabiki wengi kutoka ndani na nje ya nchi husafiri nankukutana pamoja ili kutazama mchezo wa watani hawa wa jadi waliodumu kwenye soka la ushindani kwa miaka mingi, kabla hata Tanzania haijapata uhuru.