Beki tatu (housegirl) mwizi na mchawi take care

wagagagigikoko

Senior Member
Dec 5, 2010
163
49
Tulikuwa na wasichana wawili wa kazi na mmoja aliondokaga akabaki mmoja; hivyo tukawa ktk harakati za kutafuta potential replacement ili wawe wawili.
Here comes the story part I.
Jana 21.08.2012 nlipotoka job, wife alinipa taarifa kuwa mdogo wangu wa kike (mwenye salon ya kike kimanga) alimpigia simu kuwa amepata msichana na atakuja nae home jioni akifunga saluni.
Ikabidi nimpigie simu mdogo wangu ili anipe full information.
Mdogo wangu akanimbia majira ya jioni uyo msichana alifika Saluni kwake akidai anatafuta kazi za ndani. Uyo msichana akasema yeye alikuwa anfanya kazi morogoro but ametoroka kwani alikuwa anateswa na mama mwenye nyumba.uyo msichana akizidi kuongeza kuwa yeye hana mawasiliano ya ndugu yeyote ila baba yake anishi mwanza but hanjui mama yake. Basi mdogo wangu akamuonea huruma akamkaribisha saluni ilia je nae home jioni na nifanye nae mahojiano ya kina.
Jana majira ya saa 3 usiku baada ya wao kurejea home na kula chakula ikabidi nianze kumhoji yule binti.Akanitajia jina lake na umri wake 15yrs, na nia yake ni kufanya kazi za ndani na akipata pesa ataenda kwao kusalimia then angerudi tena kuendelea na kazi yake.
Ni binti mdogo na nilitamani kumsaidia.
Baada ya kupata maelezo kutoka kwake; nilimuambia kwa sababu hatumfahamu ni lazima tukatoe report kwa balozi/mjumbe kabla hajaenda kulala na alikubali.
Nikaenda kwa mjumbe akawa ameshalala; ikabidi nimwambie wife kesho asubuhi (yaani leo) wakiamka waende kwa balozi/mjumbe kutoa taarifa na kuandikishana.
Leo asubuhi najiandaa kwenda kazini; kumbe yule binti ametoroka mapema asubuhi after mlango na geti kufunguliwa. Majirani wakasema walimuona katoka na viatu mkononi wakazani anaenda kutupa taka coz alikuwa anafagiafagia nje. Kuangalia vitu sebuleni na chumbani kwa kina dada ikaonekana everything is OK.
Basi nikawmambia mdogo wangu na kijana flani wa jirani wamfuatilie then mimi nikaondoka zangu kuelekea job.
Here comes the story part II.
Majira ya saa 4 asubuhi nikiwa job nilimpigia simu mdogo wangu anitaarifu yaliyojiri:
Akaniambia yule binti walimuona na akakimbilia nursery school flani karibia na barakuda na kwa msaada wa raia wengine walimkamata.Walimpiga kidogo na kumsachi. Walimkuta na elfu 90 na alikiri kuwa aliziiba ktk wallet ya mdogo wangu. Ikabidi mdogo wangu achukue bodaboda wakaenda nae hadi saluni kwake kimanga ili akamhoji zaidi.
Yule binti akasema kuwa alitudanganya hajatokea morogoro but anaishi na bibi ake mbagala na ule ndo mchezo wake yeye na bibi yake.
Akasema kuwa bib ake ni mchawi na huwa anamtumaga kwa nyumba za watu kwa mbinu ya kuomba kazi but baadae wanaiba na kuchukua watoto wadogo kimazingara.
Akaongeza kuwa hao watoto wadogo huwa wanawachukua misukule na wengine wakiwa wakubwa wanatumwa kama alivyotumwa yeye.
Yote hayo aliyasema bila woga huku watu wakiwa wamemzunguka pale saluni.
Akasema kuwa jana alipoingia getini bibi ake alikuja kimazingara but ghafla macho yake yalianza kumuwasha na hakuwa na amani. Kuona vile bibi ake akaondoka.
Ilipofika muda wa kulala alienda kuoga but aliporudi chumbani alimkuta mdogo wangu anasali ndipo alipigwa na miale ya blue na nyekundu akakimbia kurudi sebuleni.
Aliporudi sebuleni alimkuta wife anachek TV nae wife akashtuka kumuona yule binti hana amani.
Baade yule binti akaenda kulala ndipo wife akachukua maji ya Baraka akanyunyiza pale mlangoni na sebuleni kisha akaenda kulala.
Yule binti akazidi kuelezea kuwa usiku hakulala kwani aliteseka sana na kuweweseka na bibi ake alipokuja kimazingara hawakuweza kuchukua watoto ikabidi aondoke na kumuacha yule binti kwani alikuwa kaishiwa nguvu.
Akasema tangu aanze iyo kazi hajawahi kukamatwa na akmeshangaa sisi tumeweza kumkamata na kueleza siri zake. Akasema bibi ake alimjia kimazingara na akamwambia asirudi kwake kwani ametoa siri.
Alionesha CHALI alizochanjwa na bibi ake kama kinga na alipokuwa anapigwa hakusikia maumivu yoyote.
Alielezea mambo mengi ambayo mdogo wangu hakuweza kunielezea ktk simu kwani nae alikuwa anatetemeka kutoamini yaliyoukuwa yanatokea. Walimuachia akaondoka zake.
I felt so sorry for my twins but I thank GOD wamebaki salama.
Tuwe makini sana na wasichana wa kazi ndugu zangu; you may share it to your relatives and beloved.
 
..."Wakamuachia akaondoka Zake!"....Hii ndio imenifanya nicheke sana.
 
Hawa wafanyakazi wa ndani wa kuokotwa mitaani wana taabu sana. Tuwe makini.
 
Hahahaah! Kwa nini mkuu....!

...Mkuu Katavi, nimecheka kwa sababu nadhani mkuu Mgagagigikoko alikuwa anataka tu kutupa Ushuhuda kama ule tusioisha kupewa makanisani ba Sio kutoa mchango katika kujaribu kuliondoa tatizo hili.

Unamuachiaje Kibaka ambaye amekiri kukuibia shilingi 90 Alfu Zako?
Akienda kuendelea kufanyia wengine? Hili wewe halikuhusu kwa sababu umeishapata 90 Alfu zako?

Unamuachiaje Kibibi Gagula Dogodogo ambaye amekiri kumsaidia Bibi yake katika kuwachawia watu??
Kwa nini umuachie huru badala ya kumbeba mzobemzobe hadi huko kwa Bibi yake Mchawi na kuwasomba wote na kuwapeleka Polisi hata kama sio kwa mashitaka ya Ugagula basi angalau kwa mashitaka ya kusaidiana kukuibia shilingi Alfu 90 zako??

Yaani kwa sababu wewe Mapacha zako wamepona kuchawiwa basi unawaacha huru Wahalifu ili wakamfanyie MwanaJF mwenzao apoteze watoto wake??

Yote Tisa, Kumi ni kwa nini katika Karne hii ya Sayansi na Teknolojia Uamini maelezo ya Kichawi Gagula dogodogo bila angalau ku-doubt tu kwamba yanaweza maelezo ya kujitoa kwenye dhahama iliyomkuta??

Kwa nini umekubali kirahisi maelezo ya kichawi gagula dogodogo bila angalau kuchukua juhudi ndogon to ya kumtaka awapeleke kwa huyo Bibi yake??

Unajuaje kama saa hizi anamfanyia ndugu yako mwingine haya aliyokufanyia kwa sababu tu wewe uliamua kumuachia Huru bin Free????


....Ndio Maana Ninacheka Mkuu wangu Katavi.....!!
 
..."Wakamuachia akaondoka Zake!"....Hii ndio imenifanya nicheke sana.

See, Hii ndio JF. Hata mi nimecheka. I got this in my mails, though I see the details somewhere zinatofautinana kidogo.
While anything can be true ila if u need to analyse further ni kama story za shigongo vile. Mbona haina continuity?
 
Back
Top Bottom