Being a Sperm/Egg Donor or Surrogate Mother: Nini maoni yako, je tuna sheria zozote? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Being a Sperm/Egg Donor or Surrogate Mother: Nini maoni yako, je tuna sheria zozote?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Steve Dii, Nov 20, 2008.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wana JF, napenda kuuliza na kuomba maoni yenu kuhusiana na baadhi ya haya maswala magumu na kutatanisha katika maisha ya mwanadamu.

  Tanzania na Afrika kwa ujumla tuna tamaduni na mazingara magumu pale tunapokabiliwa na maswala yanayohitaji utaalam wa kisayansi na mwongozo wa kisheria ili kuyatatua. Mchanganyiko wa ulimwengu wa utandawazi na wimbi la teknohama katika mila na tamaduni zetu zinafanya uchukuzi wa majukumu au kutoa maoni kwa baadhi ya mambo uwe mgumu kwa namna moja au nyingine. Kwa wenzetu walioendelea kwenye teknohama na mbinu za utabibu swala hili ni gumu kwao pia lakini si kama sisi, siye ni zaidi. Mchanganyiko wa maadili, mila, teknolojia, tamaduni na yote yale tuyapitishayo kama maendeleo ni kitu ambacho kitaendelea kuwa kigumu kutatua, kuchanganua na hata kujadili katika jamii yoyote ile.

  Kwa vile hata tujitenge vipi na kujizuia kuyasikia kwa kiwango chochote kile, kwa kuzingatia hali halisi bado haya maswala katika matatizo ya uzazi yapo na yatazidi kuwepo. Vivyo hivo maswala ya ku-donate damu na viungo vingine vya mwilini nayo yatakuwepo na nadiriki kusema yatazidi kuwepo kadiri siku zinavyoenda mbele kwenye ulimwengu huu wa utandawazi.

  Hoja zangu na maswala ninayouliza ni kama ifuatavyo:

  1. Kutoka katika maadili yako, elimu yako au exposure yako ya maswala mbalimbali duniani; Je, una maoni au ushauri gani kwa mtu anayetaka ku-donate sperm au yai la kike kwa mtu anayemfahamu au asiyemfahamu?


  2. Again, kwa maadili yetu asilia; je, unamawaidha gani kwa mtu anayeamua kujiingiza katika surrogacy?

  3. Je, una pingamizi zozote kuhusiana na maswala ya ku-donate damu? Na kama huna pingamizi katika hili, je unapingamizi zozote zile pale mtu anapoamua ku-donate kiungo kimojawapo cha mwilini kwa ajili ya mwenzake?

  4. Je, una mawaidha gani kwa yule anayepokea damu kama dharura kwenye tiba?

  5. Je, Serikali yetu ina sheria zozote kuhusiana na mambo ya surrogacy, sperm donation na maswala ya "designer babies?" Kama hamna sheria au miongozo yoyote ile, je kuna itikadi au jitihada zozote kufatilia na kujitayarisha na maswala haya?

  Nitashukuru maoni yenu.

  SteveD.
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mawaidha yenu tafadhali...
   
Loading...