*Beijing Olympics 2008*

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
--Wana JF, michezo ya Olympics 2008 huko Beijing China iko mlangoni tu, je Tanzania imejiaandaa vipi na michezo ya mwaka huu?

--Ni akina nani wanajiandaa kutuwakilisha na nikwenye michezo ipi?

--Je tunamatumaini gani safari hii?

SteveD.
 
--Wana JF, michezo ya Olympics 2008 huko Beijing China iko mlangoni tu, je Tanzania imejiaandaa vipi na michezo ya mwaka huu?

--Ni akina nani wanajiandaa kutuwakilisha na nikwenye michezo ipi?

--Je tunamatumaini gani safari hii?

SteveD.

Wawakilishi au Watalii wetu?...:( Sidhani kama tutaambua hata medali moja huko China hasa ukitilia maanani performance ya wanamichezo wetu katika miaka ya karibuni na pia ukosefu wa maandalizi ya kutosha. Ni bora hiyo nauli yao na per day zingetumika kununua madawati mashuleni au kujenga vyoo katika mashule ambayo hayana vyoo.
 
Huenda Waktaka Kujaribu Kupeleka Ile Biashara Ambayo Sasa Wanamichezo Wetu Wameamua Kuifanya
 
kwa bongo kama alivyosema mdau bubu..bongo choka mbaya tu mpaka sasa ni hiyo riadha wanayotegemea..mwanamasumbwi kumbe fani yake ni kubeba kete ngumu aliingia kwa ajili ya urahisi wa kusafirisha kete nje.Nategemea kama kawaida ya wabongo timu ya viongozi itakuwa kubwa na uchache wa wanamichezo!!! hiyo ndo summer time olympics!! kungekuwa na michezo kama bao hapo kidogo najua wa bongo wangeweza fika mbali!!!
 
Wanariadha watajwa:

Wanariadha Olimpiki kwenda Beijing keshokutwa
Na Sosthenes Nyoni
Date::7/17/2008

WANARIADHA Saba watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Olimpiki Beijing, China mapema Agosti wataondoka nchini keshokutwa tayari kwa michuano hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania, (RT) Suleiman Nyambui alisema kuwa wanariadha hao bado wanaendelea na mazoezi katika kambi yao ya pamoja jijini Arusha.

Aliwataja wanariadha wanaounda timu hiyo kuwa ni pamoja na Samson Ramadhan, Fabian Joseph, Getuli Bayo na Mohamed Msenduki.

Pia wamo Dickson Marwa, Zakia Mrisho na Mwera Samwel.

"Kwa kweli maendeleo ni mazuri, wanariadha wote wapo kwenye safi na wanaendelea na mazoezi jijini Arusha, na tumeamua waondoke mapema ili waweze kuendelea na mazoezi na kuzoea hali ya hewa ya China kabla ya kuanza mashindano"alisema Nyambui.
Source: mwananchi.co.tz


SteveD.
 
sasa wawakilishi wenyewe ndio hao drug pushers kuna ahueni hapa?
 
ahueni itoke wapi? mwana!!mwaka huu hatuna chetu kwenye olympics...wakimbiaji wale viwango vyao nimeona si vyakutisha sana.Tutegemee miujiza
 
--Wana JF, michezo ya Olympics 2008 huko Beijing China iko mlangoni tu, je Tanzania imejiaandaa vipi na michezo ya mwaka huu?

SteveD.

...matumaini yapo, tena makubwa tu, yote inategemeana na 'mwanariadha' atavyoamka siku ya mashindano, na air pollution iliyoko huko huenda ika tu favor :) fingers crossed!

...mimi najiandaa kushangilia wanariadha wengine toka Afrika, hususan Dibaba sisters na Kenenisa Bekile toka Ethiopia.

...RIP UMISETA, UMISHUMTA, ...

 
Jamani tusikate tamaa! Nadhani tulisha shinda miaka ya nyuma. Juma Ikangaa na Filbert Bayi (hope got the names right) Nadhani kama serikali itawapa makocha na wawakilishi motisha zaidi watashinda. Nani alikuwa anawa train hawa wakimbiaji?? Kuna mtu ameniambia kwamba Juma Ikangaa bado anakimbia kila wiki kutoka Dar mpaka Kibaha nakurudi!
 
Jamani tusikate tamaa! Nadhani tulisha shinda miaka ya nyuma. Juma Ikangaa na Filbert Bayi (hope got the names right) Nadhani kama serikali itawapa makocha na wawakilishi motisha zaidi watashinda. Nani alikuwa anawa train hawa wakimbiaji?? Kuna mtu ameniambia kwamba Juma Ikangaa bado anakimbia kila wiki kutoka Dar mpaka Kibaha nakurudi!

Juma Ikangaa mwaka jana alikuwa 50 yrs old kama sikosei na alisinda shinda marathoni za miaka ya themanini or early 90’s, Filbert Bayi ninavyoelewa, nayeye aliset some world records zamani miaka ya 74, 75. inawezekana ana umri kuliko Ikangaa, kwa misingi hiyo sidhani kama wanaweza kufurukuta sasa hivi, labda wao ndio wawe makocha!
 
Filbert Bayi, mita 1,500, 3,000, a mile.

Suleiman Nyambui, mita 5,000, 10,000

Zakayo Marekwa, kurusha Mkuki

Gidemis Shahanga, Marathon

Emannuel Mlundwa, Boxing

...hawa ndio kumbukumbu yangu inayonionyesha walifanya vizuri hata wengine kuvunja rekodi za dunia, kuanzia All African Games, Commonwealth Games mpaka Olympic Games miaka hiyo ya 70's na 80's, Juma Ikangaa yeye aling'ara hasa kwenye Marathon za kule Japan, na 1988-1990 kushika namba mbili (mara tatu mfululizo) kule Boston Marathon.

Baada ya hapo sijamsikia mwanariadha mwingine aliyetuwakilisha vyema zaidi ya familia ya Naali, na huyu Samson Ramadhan ambaye kama angepata motisha na maandalizi ya ukweli, huenda kwenye Marathon tungekuwa na angalau matumaini kwenye hiyo 'smog' huko china..

R.I.P BMT!!!
 
September, 1993
Beijing finishes second in voting for 2000 Games, losing out to Sydney, Australia

July, 2001
Beijing awarded the Games, defeating runner up Toronto in the vote by IOC members.

Winter, 2002
China announces a total of 37 venues will be used for the games, including 12 new stadiums

December, 2003
Construction begins on the spectacular Beijing National Stadium, also known as the Bird's Nest

August, 2004
Chinese athletes win 32 gold medals in Athens, Greece second only to USA in a clear statement they intend to dominate as hosts in 2008.

February, 2006
Officials announce more than seven million tickets will be on sale with half allotted to Beijingers

2007
Former IOC president Juan Antonio Samaranch, believed to be a major influence on China getting the Games, declares the Beijing Games will be the "best in Olympic history"

March 24, 2008
Olympic Torch Relay begins in Olympia Greece but runs into trouble at various times over the next month as human rights activists protest human rights abuses in Tibet

July 1, 2008
Chinese authorities announce drastic measures to control pollution by shutting down factories and limiting the use of cars

July 16, 2008
Beijing Olympic Village opens to mostly strong reviews

Opening Ceremony
2.00pm EAT, 7.00am ET, 6.00am CT, 4.00am PT
With their slogans "One World, One Dream" the 2008 Beijing Games are scheduled to begin. Will China be able to accumulate more gold medals than USA? After spending $100 billion to prepare for those Games, will the Games be successful to be remembered as the "best in Olympic history"? Stay tuned.
 
Hili halina mjadala. Tutaia aibu kama tulivyofanya kule Athens 4 years ago kwa sababu hakuna kilichorekebishwa after Athens

44as1.jpg
 
Hakuna kitu wewe subili vijana ndo kwanza wameingia mzigoni utaona mambo yao.Wameondoka na hirizi za kibongo bongo kwa hiyo watashinda tu msihofu unafikiri tutakosa hata kamedal kamoja???
 
Hiyo picha MMhm... kama hali ya hewa itakakuwa kama kwenye picha, basi TZ watarudi na Medali japo mbili!
 
Wanakwenda shopping kama kawa...kwa kila mwanamichezo mmoja, officials watano. Tutafika?
 
unajua sisi tunategemea sana riadha, na mambo ya mbio yanachangiwa sana na kuzoea hali ya hewa. Mimi linalonishangaza sana, waandaaji walijua fika kwamba kwa China ni kipindi cha joto (summer) ambapo joto linafikia nyuzi 38 ambazo hazijawahi kufika Dar. Hata hivyo kambi ya mazoezi wakaiweka Arusha kwenye joto 16 - 20 kwa kipindi hiki. HILO ndo KOSA la KIUFUNDI. kwanini wasingeweka kambi DAR au ZANZIBAR?

For sure they will not afford to win under this mistake, kumbuka ratiba yao inaonyesha watakimbia mchana saa 7.

anyway, they may perform miracles, but TOC should not repeat this stupid mistake.
 
Hili halina mjadala. Tutaia aibu kama tulivyofanya kule Athens 4 years ago kwa sababu hakuna kilichorekebishwa after Athens

kweli tutatia aibu athens. Ikiwa swala la michezo tunalifanya siasa?(What i meant to say is, "the thread is in the wrong area"!)...... Nafikiri ndivyo ilivyo siku zote kwenye michezo bongo siasa nyingi!!!

Lakini hamna aibu ndio kikomo cha uwezo na ubunifu wetu! Wabunifu wanapigwa chini, wenye uwezo wanavunjwa moyo!
Tutafika kweli?
 
Back
Top Bottom