Bei zapanda baada ya Uchaguzi

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Sikupenda kuja huku ila kuna hili! Bei za bidhaa mbalimbali zimepanda kuanzia leo.
Kwa mfano maji ya Kilimanjaro yamepanda kwa kati ya shilingi 200 na 300. Je hii ni kufidia gharama za uchaguzi ama ni kuelekea kwenye nchi ya asali?
 
That is obvious, ni lazima bei zitapanda tu hata lita ya mafuta ya taa si ajabu ikafikia 1500
 
Consequences za maamuzi mabovu hazichukui muda kujidhihirisha.Muda si mrefu,walewale waliokuwa wakihangaika JK na CCM washinde wataanza kulalamikia jambo moja baada ya jingine.
 
Mwanzo wa ngoma ni lele. Karibu tucheze ngoma ya Bei za kuruka. Mwendo mdundo kama kawa. Hurreeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee JK. Sasa itakuwa bei kuruka kwa kasi zaidi, nguvu zaidi na ari zaidi. La kuvunda...............
 
Wewe ngoja mwaka ujao uanze ndo utaona watu wanavyolia tena wengi wao ni wale waliokuwa wahongwa tishirt za njano na vitenge mimi simo!
 
Wewe ngoja mwaka ujao uanze ndo utaona watu wanavyolia tena wengi wao ni wale waliokuwa wahongwa tishirt za njano na vitenge mimi simo!
Tena weka mkazo hapo, kuna tofauti kubwa kati ya waliokuwa wanavaa tshirt,kanga,kapelo, na wale wanaovaa MASHATI yakijani!...We chunguza kidogo tu, utaona classes za kufa mtu, na hence utajua hali ikianza kuwa ngumu ni wapi kati ya hao wataanza kulalama!
 
07.jpg

06.jpg
 
I side with you. Huitaji wala kuchunguza inaonekana waziiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Haya ndio matunda ya soko huria ambalo walaji hatuna umoja wa kututetea na hivyo wauzaji wanaweza wakala njama za kutuumiza sisi. Hapa ni mpaka yatokee yale yailyotokea Msumbiji hiv majuzi ndio watawala na wauzaji wetu watajua kwamba tunataabika, tunasulubikaa
 
Unapofanya mtihani si unategemea kupata matokeo! NDO HAYO!
ukila ujue UMELIWA!
 
mtakoma yeye kapita kwa ujanja wake si mlimktaa kumchagua sasa kacheza mpira umekubali kubali yahishe tule nyasi kama mramba alivyosema
 
tunaelekea nchi ya maziwa na asali hivyo wananchi msiwe na wasiwasi kabisa:A S-baby:
Sikupenda kuja huku ila kuna hili! Bei za bidhaa mbalimbali zimepanda kuanzia leo.
Kwa mfano maji ya Kilimanjaro yamepanda kwa kati ya shilingi 200 na 300. Je hii ni kufidia gharama za uchaguzi ama ni kuelekea kwenye nchi ya asali?
 
Yalitarajiwa yote hayo na bado mpaka warudishe fedha zilizotumika kwenye kampeni
 
Ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Tanzania yenye njaa imeanza. maisha bora kwa 'kila' mtanzania ndiyo hayoo yanaendelea kuja. Tusilaumiane. Tumechagua hovyo wenyewe, tukitendwa hovyo tusinene hovyo!
 
Duh poleni sana, lakini ndo kufidia gharama huko sasa, waliolazimishwa kuchapisha tshet wanahitaji fedha kufidia. Kuna msemo wa kiingereza unasema "you can take a donkey to the pond but you cant force it to drink." Sasa midhali tumechagua kwa kishindo acha tukipate. Na nadhani dola itafika sh 2000+ muda si mrefu.
 
Sasa napendekeza kitu kimoja. Kama mtu akilalamika maisha magumu na anakutaka umsaidie: muulize alikipa kura Chama Gani? Atapata aibu na kujifunza.
 
Haya ndio matunda ya soko huria ambalo walaji hatuna umoja wa kututetea na hivyo wauzaji wanaweza wakala njama za kutuumiza sisi. Hapa ni mpaka yatokee yale yailyotokea Msumbiji hiv majuzi ndio watawala na wauzaji wetu watajua kwamba tunataabika, tunasulubikaa
Tetea ufisadi lakini kuumia tutaumia sote.............nchi kamwe haiwezi kuendelea kama serikali iliyopo madarakani hailaumiwi wakati mambo yanakwenda vibaya.....................................iteteeni serikali ya mafisadi na watakapomaliza vya kuchakachua watatuchakachua sote uhai wetu bila ya huruma au kujali waliokuwa wanawapigia debe..........................
 
Nani Tanzania huwa ana riot kwa sababu ya kupanda bei hata ya mkate tu? Watanzania ndugu zangu ni watu wa ajabu sana! wao ili mradi kesho asubhi inakuja, hakuna anayejali imekuja vipi!
Nimeamua kutotoa msaada kabisa kwa mtu yeyote aliye na shida. Kila mtu afe na shida zake. Mie nitaendelea ku fight kivyangu kula na wanangu na wengine wacha wapate shida watajifunza. Sintaona huruma hadi wadanganyika wajifunze. I mean what I say. Na nimeshaanza operation hii. Kila mwenye shida hata kama iko katika uwezo wangu namuelekeza ofisi ya mbunge wa ccm. watakoma.
 
Back
Top Bottom