Bei za vyakula jijini Dar zapanda mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,295
33,079
attachment.php



BAADHI ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wamelalamikia bei kubwa za vyakula katika kipindi hiki cha Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwenye badhi ya masoko jijini humo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi wa jiji hilo Bw. Khamis Mshaka na Bi. Salma Jumbe, walisema baadhi ya wafanyabiashara wanapandisha bei ya vyakula ili kupata faida.

Walisema hali hiyo inawafanya wananchi wengi hasa wenye kipato kidogo washindwe kumudu bei za vyakula wanapokwenda sokoni.

“Tabia hii si nzuri na imekuwa ikijitokeza mara kwa mara unapofika wakati wa mfungo...bidhaa zilizopo sokoni si za Waislamu pekee, hivyo tunaziomba mamlaka husika zichukue hatua,” walisema.

Bi. Jumbe alisema, baadhi ya wafanya biashara wanaficha vyakula kwenye maghala ili siku zinavyozidi kwenda, waviuze kwa bei kubwa jambo ambalo serikali inapaswa kulifanyia uchunguzi ili kukomesha tabia hiyo.

Kwa upande wake, Bi.Maria Albert ambaye ni mamalishe, anayefanya biashara ya kuuza chakula kwenye Mtaa wa Kongo, Kariakoo, alisema kutokana na bei kubwa ya vyakula, wanashindwa kupata faida.
Alisema bei ya sasa kwa mhogo mmoja ni kuanzia sh .1,000 kutokana na ukubwa wake ambapo magimbi ni sh. 3,000 kwa sado moja tofauti na awali ambapo ilikuwa ni sh.1, 500.

Naye Bw. Brown Sanga, mfanyabiashara wa nafaka katika Soko la Kisutu, alisema ni dhambi kupandisha bei za vyakula katika kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani.

“Wafanyabiashara tunapaswa kuwa na ubinadamu hata kama tunatafuta pesa, tunatakiwa kusaidiana ili ndugu zetu Waislamu tusiwaweke katika mazingira magumu ya kutafuta futari,” alisema.

CloudsFM
 

Attachments

  • mihogo.jpg
    mihogo.jpg
    35.2 KB · Views: 128
Back
Top Bottom