Bei za nondo kupungua mwakani

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
BEI ya Nondo inatarajiwa kushuka kwa asilimia 25, kuanzia mwakani, baada ya kiwanda cha Nondo cha Kiluaa kukamilisha awamu ya pili ya ujenzi,ambayo itakuwa ikitengeneza Nondo 5,000 na vyuma vikubwa vya kujengea madaraja na matumizi mengine.

Kiluwa inatarajia hadi kufikia mwakani wawe wamekamilisha hatua hiyo, na uzalishaji uanze mara moja,ili kupunguza gharama za ununuaji wa nondo zinazotoka nje ya nchi kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya ujenzi.

Mbali na Nondo, pia watakuwa wakizalisha vyuma vikubwa ambavyo kwa sasa vinatolewa nje kwa ajili ya kujenga madaraja, pamoja na nguzo kubwa ambazo nyingi zinatumika katika ujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari,Mkurugenzi wa kiwanda hicho kilichopo Mlandizi mkoani Pwani, Mohamed Kiluwa, alisema lengo la kiwanda hicho ni pamoja na kuhakikisha wanazalisha vyuma vyenye thamani kubwa ambavyo vitakuwa vikiuzwa katika nchi mbalimbali za Afrika, na nje ya bara hilo.

Alifafanua zaidi ya kuwa, mara baada ya awamu hiyo kuanza, zoezi la uagizaji vyuma na nondo kutoka nje litasitishwa kwa sababu vyuma vitakavyotengenezwa hapo vina thamani kubwa kama vile vinavyoingizwa kutoka nje, kwa sababu hapa nchini havipatikani.

"Sasa hivi bado tunazalisha nondo 2,000 kwa siku,lakini tutakapoanza awamu ya pili tutakuwa tukizalisha nondo 5,000 kwa siku na kwa mwaka itakuwa nondo milionil 1.5, jambo ambalo pia litachangia ongezeko la ajira kwa vijana ambao hawana kazi,"alisema Kiluwa.

Alisema nondo ambazo wanatarajia kuanza kuzizalisha katika awamu ya pili zitakuwa bora zaidi kama ilivyo sasa ambazo wanatumia zinazotoka Uingereza na zina soko kubwa kutokana na uimara wake.

Alisema kutokana na hilo, wanaiomba Serikali ijitahidi kuzuia vyuma feki ambavyo vitaingizwa nchini, ili kuwasaidia wawekezaji wazawa ambao wameamua kuungana na Rais John Pombe Magufuli, kuhakikisha uchumi wa nchi unapanda, kupitia viwanda ambavyo vimeanza kazi ya kutengeza nondo.

Naye Mkurugenzi wa Kiluwa, Wang Zuojin ambaye anafanya kazi kwa kushirikiana na kiwanda hicho, alisema Tanzania kuna kila rasirimali, kwa hiyo kutokana na jitihada zinzofanywa na Rais wa awamu ya tano ya kutaka nchi iwe ya viwanda,Kiluwa imeamua kwenda na sera hiyo na tayari wameanza zoezi hilo la ujenzi lililofikia hatua za mwisho.

Alisema mara uzalishaji utakapoanza, kutakuwa hakuna haja ya kuagiza vyuma na nondo nje, badala yake kiwanda hicho kitakuwa kikiuza nje ya nchi nondo zake kutokana na ubora utakaokuwa nao.

Alisema wamefikia hatua nzuri, ambapo bado vitu vichache ili waanze kazi rasmi ya uzalishaji wa nondo halali katika kiwanda hicho ambacho kitakuwa kimoja kati ya viwanda vikubwa barani Afrika.

Source: Bei za nondo kupungua mwakani | Latest News, Sports, Business, Entertainment, Features, Columnist | IPPMEDIA
 
Kwa Dongote tuliambiwa simenti itakuwa elfu nane....lakini mpaka leo inauzwa bei gani.?
 
Back
Top Bottom