Bei za mafuta zimelenga kudhoofisha uchumi na kuleta vurugu nchini

Fatma-Zehra

Senior Member
Oct 18, 2020
192
1,061
Kuanzia tarehe 1 July, bei za mafuta, kuanzia petrol, diesel, kerosene zitapanda kwa kiwango kisicho na chembe ya uungwana. Maisha yatapanda.

Mfumuko wa bei utapanda wakati kodi zitashuka maana hali naiona siyo nzuri sana.

Kushuka kwa kodi pamoja na kupanda kwa gharama za maisha italeta economic and social crises angalau kwa miaka kadhaa ijayo iliyojaa vituko vya Covid.

Katika kipindi cha uchumi wa dunia kutotabirika kama sasa, ni hatari kwa usalama wa taifa letu kuongeza bei za bidhaa na huduma muhimu kupitia ongezeko la mafuta.

Mama hapa kashauriwa vibaya. Abadili maamuzi. We love her.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,909
287,648
Hapo ulipodai maza kashauriwa vibaya mie nakupinga. Kama hawezi kufanya maamuzi binafsi bila kujali ushauri aliopewa na washauri wake kwa maslahi ya Watanzania basi kuna tatizo kubwa sana.

Nchi kama haina pesa aanze kulala mbele na mishahara na marupurupu ya Wabunge vyote ni vikubwa sana. Kuna Wabunge haramu 19 kila mwezi wanalipwa malipo haramu ya mabilioni ambayo hawastahili.
 
Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
2,185
3,495
Mbaya zaidi pesa karibu 70% itaishia kuwalipa viongozi posho na marupurupu huku wao maumivu ya kodi yakiwa mbali nao kwa sababu wanapewa mafuta bure na serikali.

Hapa maumivu ni kwa watu wa kipato cha kati, chini na maskini lakini sio wao viongozi wetu.
 
Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
9,877
16,574
Ina maana huyo mama enu hana akili ya kuamua lipi linafaa na lipi halifai!? Una uhakika gan kama kashauriwa na si yeye aliyeamua?
 
Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,800
11,863
Hapo ulipodai maza kashauriwa vibaya mie nakupinga. Kama hawezi kufanya maamuzi binafsi bila kujali ushauri aliopewa na washauri wake kwa maslahi ya Watanzania basi kuna tatizo kubwa sana.

Nchi kama haina pesa aanze kulala mbele na mishahara na marupurupu ya Wabunge vyote ni vikubwa sana. Kuna Wabunge haramu 19 kila mwezi wanalipwa malipo haramu ya mabilioni ambayo hawastahili.
Nimeona mlipuko wa ajabu wa mikutano ya watendaji wa serikali siku za hvi karibuni. Mikutano hii, inafanyika kwenye kumbi za kulipia, kinyume na miezi michache kadhaa iliyopita. Safari zimeongezeka kwa kasi.

Ninaona wafanyakazi wa Wizara ya fedha wanaiba mabilioni ya fedha, wakati huo huo serikali haina fedha.

Wabunge wanalipwa kama wageni waliotoka sayari Mars, na bado wanapiga debe waongezewe malipo.

Kama kweli serikali haina fedha, hizi za mambo haya zinatoka wapi? Mtu akifikiria kwamba tuna watoa maamuzi wabinafsi wasiofaa na wasiojali maslahi ya umma wala maumivu ya watu wengine atakufa anakosea? Hivi kweli serikali kama kweli inajali, inashindwaje kuongeza wigo wa walipa kodi, kwa kufufua makampuni ya serikali yenye uwezo wa kuongeza uwezo wanyonge ili walipe kodi nzuri kama Pride Africa, lilokuwa limezagaa kila kona watu wakipata huduma za fedha kwa shangwe, wakiboresha maisha na kulipa kodi? Ni kwlei kwamba hakuna mtu mwenye ubunifu na ufahamu wa njia za kuongeza mapato kwa serikali, badala yake wanaongeza bei za mafuta ili hao walala hoi wazidi kufa na familia zao?

Mama anaposhauriwa, ni lazima achukue shauri kama zilivyo hata kama ni dhahiri kuna harufu ya madhara na yeye ni mchumi?

Ninadhani anahitaji msaidizi wa uchambuzi. Vinginevyo, tunaweza kuenda vibaya kwa shauri zenye mrengo wa ubinafsi na kutokujali maisha ya wanyonge.
 
Buenos Aires

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,321
1,145
Hapo ulipodai maza kashauriwa vibaya mie nakupinga. Kama hawezi kufanya maamuzi binafsi bila kujali ushauri aliopewa na washauri wake kwa maslahi ya Watanzania basi kuna tatizo kubwa sana.

Nchi kama haina pesa aanze kulala mbele na mishahara na marupurupu ya Wabunge vyote ni vikubwa sana. Kuna Wabunge haramu 19 kila mwezi wanalipwa malipo haramu ya mabilioni ambayo hawastahili.

Alafu yule mbunge asie na huruma kwa wananchi anataka waongezewe salary 🤣🤣 akili za kipumbavu kabisa
 
Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
3,733
2,848
Hapo ulipodai maza kashauriwa vibaya mie nakupinga. Kama hawezi kufanya maamuzi binafsi bila kujali ushauri aliopewa na washauri wake kwa maslahi ya Watanzania basi kuna tatizo kubwa sana.

Nchi kama haina pesa aanze kulala mbele na mishahara na marupurupu ya Wabunge vyote ni vikubwa sana. Kuna Wabunge haramu 19 kila mwezi wanalipwa malipo haramu ya mabilioni ambayo hawastahili.
Tulizana wewe, nyie ndo mlitaka viongozi wapewe ushauli na kutotumia maamuzi binafsi sasa taena mnageuka vipi et atumie maamuzi binafsi?
Nyie ni popo hamjulikani.
 
6 Reactions
Reply
Top Bottom