Bei za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zashuka Tanzania kwa mwezi Desemba

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) nchini Tanzania imetangaza bei za kikomo kwa bidhaa za mafuta nchini humo zitakazoanza kutumika kuanzia kesho Jumatano Desemba 4, 2019.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Desemba 3, 2019 kwa vyombo vya habari na kaimu mkurugenzi mkuu wa Ewura, Nzinyangwa Mchany imesema bei za jumla na rejareja za mafuta za petroli dizeli na mafuta ya taa zimepungua.

Mchany amesema mafuta hayo ni yale yaliyoingia kupitia bandari ya Dar es Salaam ambayo yamepungua ukilinganisha na mwezi uliopita.

“Kwa Desemba 2019, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa Shilingi 31/lita (sawa na asilimia 1.39), Shilingi 33/lita (sawa na asilimia 1.52) na Shilingi 43/lita (sawa na asilimia 2.02)” amesema

“Bei za jumla za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa Shilingi 30.46/lita (sawa na asilimia 1.47) na Shilingi 32.63/lita (sawa na asilimia 1.60) na Shilingi 42.63/lita (sawa na asilimia 2.14)”

Amesema bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli yanayoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga na Mtwara nazo zimepungua ikilinganishwa na mwezi uliopita

“Punguzo la bei za mafuta katika soko la ndani kwa mafuta yaliyoingizwa nchini kupitia bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara linatokana na kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia na gharama za usafirishaji (BPS premiums)” amesema
 

Attachments

  • Bei-Kikomo-za-Bidhaa-Mafuta-ya-Petroli-Kuanzia-Jumatano-Tar-4-Desemba-2019-Kiswahili.pdf
    268.6 KB · Views: 3
Nafikiri kwakuwa ni msimu wa sikukuu ndomana bei zipo down, imekaa vema
 
1575523725982.png

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa nchini kwa mwezi Desemba, zinazoonesha kupungua. Hali hiyo inafanya wananchi katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, kufurahia punguzo hilo hasa kwa wale wanaotumia vyombo vya moto vya usafiri.

Akitangaza bei kikomo hizo jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Nzinyangwa Mchany alisema bei hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia leo Desemba 4 na zitadumu kwa mwezi mmoja. Alisema bei hizo kwa rejareja, zimepungua kwa shilingi kati ya 31 hadi 55 kulingana na mkoa na kwamba bei kikomo kwa ujumla wa mikoa yote, itakuwa kuanzia Sh 2,075 hadi 2,405 kwa lita moja ya mafuta aina ya petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Mchany alisema bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa yaliyoingizwa nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam, zimepungua kutoka Sh 39 ya mwezi uliopita hadi kufika Sh 31 kwa mwezi huu sawa na asilimia 1.39. Aidha alisema bei za jumla, nazo zimepungua ukilinganisha na mwezi uliopita na kwamba bei za jumla za petroli, dizeli na mafuta ya taa, zimepungua kwa Sh 30.46 kwa lita moja sawa na asilimia 1.47.

Alisema bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia Bandari ya Tanga, nazo zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 6 Novemba 2019.

Kwa mwezi Desemba 2019, bei za rejareja za petroli na dizeli kwa mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara) zimepungua kwa Sh 38 kwa lita sawa na asilimia 1.74 na Sh 46 kwa lita sawa na asilimia 2.09 Mchany alisema kupungua kwa bei hizo, kumetokana na bei ya mafuta kwnye soko la dunia kushuka na pia gharama za uzafirishaji kupungua pia. Kwa maana hiyo, bei kikomo ya mafuta jijini Dar es Salaam kwa mafuta ya petroli ni Sh 2,161 , dizeli ni Sh 2,125 na mafuta ya taa ni Sh 2,075.

Aidha alisema bei hizo zimepungua kwa mikoa yote. Alieleza kwamba bei kikomo za mafuta kwa eneo husika, zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.

Chanzo: Habari Leo
 
HIKI NI KISHINDO CHA AWAMU YA TANO. Kama Mbowe kaongezewa muda wa Uenyekiti CHADEMA, basi na sisi tunamuongezea JPM muda wa kutawala hadi 2030. Habari ndiyo hiyo...
 
Isitiri aibu yako Mungu ametuumbia mafuvu ili tufiche mengi mengine muwe mnayaacha humo humo.
Bei za mafuta hupanda na kushuka miaka yote.
Mwambie kama tumbo lilivyokuwa halipo kama kiyoo cha kuona nini linaendelea ndani ndivyo aibu zetu hasa za uelewa (ufinyu wa ubongo) zinatakiwa zifichwe
 
Hizi nyege mbaya sana !
HIKI NI KISHINDO CHA AWAMU YA TANO. Kama Mbowe kaongezewa muda wa Uenyekiti CHADEMA, basi na sisi tunamuongezea JPM muda wa kutawala hadi 2030. Habari ndiyo hiyo...
 
HIKI NI KISHINDO CHA AWAMU YA TANO. Kama Mbowe kaongezewa muda wa Uenyekiti CHADEMA, basi na sisi tunamuongezea JPM muda wa kutawala hadi 2030. Habari ndiyo hiyo...
Vizuri wakubaliane wote wawili kila mmoja awe for life katika nafasi yake!
 
Wamerejesha bei ya September! hakuna jipya !!!
mbona ilikuwa hiyo, wakaipandisha ili waje waishushe kutengeneza story!
kumbe ndo bei
 
Back
Top Bottom