Bei za mafuta; tuliyataka wenyewe, sasa yanatukuta!

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Wakati wa awamu ya pili ya Mzee Mwinyi, wenye akili waliitaka Serikali iachane na biashara ya kuingiza mafuta nchini na kuyasafisha. Mwinyi alikuwa rais, Yona Kilaghane DG wa TPDC (ni mkuu wa TPDC hadi sasa! Sikumbuki Waziri wa Nishati alikuwa nani kati ya Rais Kikwete au Alnoor Kassum. Kilichofuata ni kukifunga kiwanda cha TIPER, mamia ya wafanyakazi kukosa ajira na kuibuka Makampuni ya kuagiza mafuta. Kwa kugundua makosa yetu, Serikali mwaka juzi ikaiagiza TPDC ianze kuagiza mafuta tena.
 
Pia serikali ikatoa amri kuwa makampuni binafsi yaingize mafuta kwa pamoja ili kujaribu kuzuia hujuma kwa uchumi, mafuta kuadimika na bei kupanda holela.

Hadi sasa hakuna kilichotekelezwa; TPDC haijaanza kuingiza mafuta wa makampuni yamegoma kuingiza mafuta kwa pamoja! Sasa tunaona jeuri ya wafanyabiashara na jinsi wanavyojibishana na serkali kwa ujeuri (rejea kauli ya mwenyekiti wao juzi).
Pamoja na kushushwa ushuru tangu Jul, bado hawataki kushusha bei za mafuta.
 
Wenzetu Kenya na Zambia bado wana viwanda vya kusafisha mafuta ghafi, sisi tumepotea kiwanda chetu na kuwa maskinisha Watz wenyetu kwa kuua chetu!

Hatujagundua upumbavu wetu had sasa? Matanki na Mitambo ya TIPER vipo, hivi hatuwezi kugundua mahali tumejikwaa na kuinuka tena? Pili, hivi kwa nini TPDC hawajaanza kuingiza mafuta? Hivi kwa nini agizo la kuwataka wafanyabiashara kuingiza mafuta pamoja halijtekelezwa? Serikali imechukua hatua gani kwa kupuuzwa kwa maagizo yake?

Tuliyataka, sasa yanatukuta!
 
Back
Top Bottom