Bei Ya Umeme Juu Kwa Asilimia Moja

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
251
11
WAKATI SAKATA LA RICHMONDULI LIKIWA LIMEWAKALI KOONI WANACCM HUKO DODOMA,TANESCO YAONGEZA BEI YA UMEME KWA ASILIMIA 1 KWA WATEJA WAKE WOTE. JE TUTAFIKA?

TANESCO yamwongezea mteja mzigo
SOURCE: MAJIRA
Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa mara nyingine imeanzisha mbinu zaidi za kumkamua mteja wake kwa kuongeza asilimia moja katika malipo yake ya LUKU na Ankara.

Kwa mujibu wa matangazo ya shirika hilo kwenye vyombo vya habari jana, watoa huduma za maji na nishati nchini wanapaswa kuchangia asilimia moja ya mapato yao kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (EWURA).

"Kwa mujibu wa sheria namba 414 ya EWURA kifungu cha 43(3) watoa huduma za maji na nishati wanapaswa kuchangia asilimia moja ya mapato yao kwa EWURA.

"Kutokana na sheria hiyo, kuanzia Februari mosi mwaka huu, TANESCO imeingiza gharama hiyo ya asilimia moja, kwenye malipo ya umeme na kuonesha kwenye risiti za kununua umeme wa LUKU na ankara," lilisema tangazo la TANESCO jana.

Ili kufafanua hatua hiyo, shirika hilo ambalo hivi karibuni lilipandisha bei ya umeme wake, lilibainisha kuwa kuanzia wakati huo ankara zake zitasomeka: "VAT(20%)+ EWURA CHARGES (1%)" na kwenye risiti itakuwa: "VAT(20%)+EWURA CHARGES (1%)".

Wakati huo huo, Shirika hilo limewaeleza wateja wake kuwa muda wa kulipa madeni ya umeme bila riba ya asilimia mbili inayotozwa kwa wateja wenye madeni, umeongezwa kuanzia Februari mosi hadi Aprili 30 mwaka huu.

"Kama mtakumbuka, wakati wa kampeni ya kukusanya madeni mwishoni mwa mwaka jana, wateja ambao wamelimbikiza madeni ya umeme, walitakiwa kulipia madeni yao yote na hivyo kupewa motisha ya kufutiwa riba inayotozwa kwa wateja waliolimbikiza madeni," ilisema taarifa ya TANESCO.

Ilisema kwa hali hiyo, wateja ambao hawakuweza kulipa madeni yao wakati wa kampeni, wanaombwa kulipa madeni yao ili waweze kupewa motisha ya kufutiwa riba katika kipindi cha miezi mitatu.

Ilisisitiza kuwa kwa wateja ambao watashindwa kulipia madeni yao katika muda uliotolewa, hatua stahili zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kukatiwa umeme.
 
rroo. nawaampiaga mijitu yoooooote inayotumiaga miumeme muanzege kuipaga miumeme. mimi naiipiaga tu. nimerichukuwaga ritaaramu rimoja rikakandamizaga riruku rao. rinapuyanga rifuliji. rinapuyanga riruninga. rinapuyangaga rijikoraumeme. inapuyangaga mipangaboi ire ya sikuizi wanaitagaga miyoyozi. nasisi uku tunayogo. rakini haturipagi mipesa mingi. tunaripagaga rierufu ishilini kwa limwezi rote. muwaipiege mukomeshane. rikikundamizaga nawenyewe murikandamizege mukiaracha mutageuke kama ire miswairi inajifanyaga mijanamuke.
 
Yaani mpaka sasa TANESCO hawajaona kuwa wananchi wamelemewa huo mzigo wanaotwishwa?ama kweli maisha bora kwa kila mtanzania yameyeyuka.Umeme juu,petrol juu??? uchumi unakua kwa kiwango cha asilimia.....????????
 
Maisha bora kwa kila mtanzania,umeme mpaka vijijini ambako watu wanaishi chini ya dollar moja kwa siku,TUTAFIKA?
 
Wakalaumiwa hao wanasiasa wanao kutana sasa hivi ktk "kijiwe" chao huko Dodoma kwa kutufikisha hapa.

Tutawaona wabaya Tanesco lakini hawana budi kufanya hayo wanayo yafanya kwani mzigo wa kulipa IPTL, Songas na hili balaa la Richmond ni mkubwa kwao na serikali wameshafuta ruzuku kwa Tanesco sasa njia ya pekee kwa Tanesco kujikwamua kutoka kwenye hili balaa ni kum-bebesha mzigo mtumiaji wa mwisho tu.

Way forward sasa ni alternative energy mtu kama una uwezo nunua solar, windmill, biogas etc ushakuwa ubwege sasa...
 
Kama wananchi wa tanzania wameamka kama Mwakeyembe na kama timu yake..Ni wakati watz ,..waamake wajimwage barabarani waandamane wagome..kabasaaaa!!! Na wadai wote waliohusika kuwafikaisha hapo..warejeshe mafao waliyoiba!! na kama bado mahesabau haya balance kiasi kingine serekali ya Kikwete ijaziee ..maaana ndio waliwaweka hao wakinalowasa...SASA INATOSHA UPUUZI WA EL NA WENZAKE HATUWEZI KUUFIDIA..!!
 
Mbona wabongo wanaumia na bei ya umeme. Jamani eh kweli tunaumia. Na hao mafisadi bado wana tamba na pesa zao za offshore.
 
Back
Top Bottom