Shukurani
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 253
- 11
WAKATI SAKATA LA RICHMONDULI LIKIWA LIMEWAKALI KOONI WANACCM HUKO DODOMA,TANESCO YAONGEZA BEI YA UMEME KWA ASILIMIA 1 KWA WATEJA WAKE WOTE. JE TUTAFIKA?
TANESCO yamwongezea mteja mzigo
SOURCE: MAJIRA
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa mara nyingine imeanzisha mbinu zaidi za kumkamua mteja wake kwa kuongeza asilimia moja katika malipo yake ya LUKU na Ankara.
Kwa mujibu wa matangazo ya shirika hilo kwenye vyombo vya habari jana, watoa huduma za maji na nishati nchini wanapaswa kuchangia asilimia moja ya mapato yao kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (EWURA).
"Kwa mujibu wa sheria namba 414 ya EWURA kifungu cha 43(3) watoa huduma za maji na nishati wanapaswa kuchangia asilimia moja ya mapato yao kwa EWURA.
"Kutokana na sheria hiyo, kuanzia Februari mosi mwaka huu, TANESCO imeingiza gharama hiyo ya asilimia moja, kwenye malipo ya umeme na kuonesha kwenye risiti za kununua umeme wa LUKU na ankara," lilisema tangazo la TANESCO jana.
Ili kufafanua hatua hiyo, shirika hilo ambalo hivi karibuni lilipandisha bei ya umeme wake, lilibainisha kuwa kuanzia wakati huo ankara zake zitasomeka: "VAT(20%)+ EWURA CHARGES (1%)" na kwenye risiti itakuwa: "VAT(20%)+EWURA CHARGES (1%)".
Wakati huo huo, Shirika hilo limewaeleza wateja wake kuwa muda wa kulipa madeni ya umeme bila riba ya asilimia mbili inayotozwa kwa wateja wenye madeni, umeongezwa kuanzia Februari mosi hadi Aprili 30 mwaka huu.
"Kama mtakumbuka, wakati wa kampeni ya kukusanya madeni mwishoni mwa mwaka jana, wateja ambao wamelimbikiza madeni ya umeme, walitakiwa kulipia madeni yao yote na hivyo kupewa motisha ya kufutiwa riba inayotozwa kwa wateja waliolimbikiza madeni," ilisema taarifa ya TANESCO.
Ilisema kwa hali hiyo, wateja ambao hawakuweza kulipa madeni yao wakati wa kampeni, wanaombwa kulipa madeni yao ili waweze kupewa motisha ya kufutiwa riba katika kipindi cha miezi mitatu.
Ilisisitiza kuwa kwa wateja ambao watashindwa kulipia madeni yao katika muda uliotolewa, hatua stahili zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kukatiwa umeme.