Bei ya sukari yapaa tena

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
8,132
5,785
Wakuu,

Natumai mu wazima wa afya,

Lengo la mada hii ni kutaka tupeane bei sukari kwa maeneo mbalimbali mlioko hapa nchini. Ndani ya wiki moja sukari imeongezeka kutoka tsh.105000 hadi tsh.113000 kwa kiroba cha 50kg mkoa wa Ruvuma hakuna maelezo yoyote kutokana na ongezeko hilo.
 
Kwa kweli hata sielewi tatizo lipo wapi.Tumeambiwa Makusanyo yameongezeka,Mafisadi wamedhibitiwa,Watumishi hewa wameondolewa na waliokuwa wanategemea maisha ya ujanjaujanja hawapo tena.Kwa nini sasa bei ya vitu inazidi kupaa badala ya kupungua?.Lini tutapata unafuu wa maisha kama mishahara na madaraja hayapandi wakati bei ya vitu inazidi kupanda?
 
kuna haja ya kupewa mwongozo ni masikini wepi ambao mheshimiwa huwa anawazungumzia
 
Kama kawaida ya kila mwaka kipindi cha masika viwanda vya sukari vimeanza kufungwa na sukari imepanda bei.

Hapa Arusha bei ya jumla imepanda kutoka tzs 98,000 kwa mfuko wa kilo 50 hadi TZS 1050,00. Bei ya rejareja ni TZS 2,500 kwa kilo kutoka 2,200.

Tunaomba Waziri Mkuu atoe tamko kama hii ni halali na serikali inachukua hatua gani kuziba pengo kama kuna upungufu.
 
Hata Mwanza imepanda...ila nasikia viwanda vimesimamisha uzalishaji....
 
Kama kawaida mtasikia kuwa kuna wafanyabiashara wameficha sukari. Yule mtu wenu ataikamata awagawie bure!
Lakiniii, hivi desturi ya kubugia sukari wabongo mliitoa wapi?! Tafuteni mbadala, Sukari ni mbaya kwa afya.
 
Back
Top Bottom