Bei ya Saruji ilipanda kutokana na kufungwa kwa kiwanda cha Dangote

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Kiwanda cha Dangote kinachozalisha Saruji kilichopo mkoani Mtwara, kilisimamisha uzalishaji wa Saruji kwa takribani wiki mbili ili kufanya usafi na ukarabati wa kiwanda.

Imedaiwa kuwa hali hiyo ilifanya bei ya Saruji ipae kiasi cha wananchi kulalamikia bei hizo. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa alitembelea Kiwandani hapo ili kujua kinachoendelea.

Mwanasheria wa kiwanda hicho, Clagu Chuma ameomba radhi kwa kutotoa taarifa kwa raia hali iliyopelekea bei kupanda kwa kasi kubwa.

Bei ya Saruji ilipanda hadi kufikia Tsh 35,000 kwa baadhi ya mikoa.

PIA SOMA: Wanyonge wenzangu: Bei ya Saruji huko kwenu ipo vipi?
 
Hii ni sababu ya kitoto.

Jana nimesikia mtu mmoja anasema eti sababu yya miradi ya maendeleo kutokusimama kipindi cha uchaguzi ndio maana simenti imepanda, hii ni sababu ya kitaahira pia.

CCM hata wakipewa miaka 700 hakuna kitu cha maana watatufanyia, ona wanachokifanya sasa, hakuna zaidi ya kuwafukarisha watanzania.

Halafu wanajiita serikali ya wanyonge 😂😂.
 
Sababu za kitoto kabisa, Watanzajia tunadharaulika kwa kuwa ni watu cheap sana.

Kuna viwanda vya cement karibu 16 nchini , hapo Mtwara tu vipo viwili, inakuwaje Dangote azime mtambo kwa wiki mbili tu halafu Bei ya cement ipae juu hadi kufikia 35000?
 
Mimi nadhani cement imepanda kwa sababu sasa hivi kila mwananchi hapa nchini anajenga nyumba ya kupangisha wapangaji kwa hio ni mwendo wa demand vs supply hapo.

Mitano tenaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Ina maana tangu kiwanda kianze uzalishaji hii ndiyo mara ya kwanza wanasimamisha uzalishaji ili kufanya ukarabati. Ccm wanaona kila mtu ni zuzu. Sasa azam naye akisimamisha uzalishaji ili kufanya ukarabati si mikate na sembe vingepanda bei. Hawa watu ni bure kabisa
Azam is so smart. Dangote ni mtu hatari sana. Kote alikowekeza kasababisha matatizo.
 
Back
Top Bottom