Bei ya petrol na mabadiliko ya hali ya hewa kuathiri uchumi wa tanzania-2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei ya petrol na mabadiliko ya hali ya hewa kuathiri uchumi wa tanzania-2010

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msharika, Mar 21, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ONGEZEKO la bei ya bidhaa za petroli na kuendelea kwa mvua nyingi za masika, vimeelezwa kutishia kuvuruga uchumi wa nchi kwa kuongeza bei ya huduma na bidhaa.

  Taarifa ya mpango wa usimamizi wa sera ya fedha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu iliyopo kwenye Ripoti ya Sera ya Fedha iliyotolewa na Benki Kuu (BoT) mwishoni mwa mwezi uliopita, imeeleza kuwepo kwa uwezekano wa kupanda kwa bei ya mafuta hayo ambako kutasababisha kuongezeka kwa bei ya bidhaa na huduma muhimu.

  Ongezeko la bei ya mafuta husababisha ongezeko la nauli ya huduma za usafiri ndani ya miji mbalimbali na usafiri wa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

  Pia ongezeko hilo la bei husababisha kuongezeka kwa gharama za usafiri wa bidhaa mbalimbali hasa za chakula cha nafaka kinachotumika kwa wingi mijini kutoka mashambani na kutishia ongezeko la bei ya chakula.

  BoT imesema ikiwa mvua zinazoendelea kunyesha zitaharibu mazao na miundombinu zitaongeza ugumu wa kupunguza ongezeko la bei ya vitu nchini.

  Kwa sasa mfumuko wa bei umepungua kutoka zaidi ya asilimia 10 iliyokuwepo kwa kipindi kirefu tangu mwishoni mwa mwaka jana na kufikia asilimia 9.6 mwezi uliopita kutokana na kupungua kwa bei ya chakula.

  BoT imeshauri serikali kutekeleza uamuzi wake wa kutaka kuuza chakula cha akiba kilichopo katika Hifadhi ya Chakula ya Taifa, ili kupunguza bei ya soko ya chakula kama moja ya njia ya kukabiliana na ongezeko la bei za bidhaa na huduma mbalimbali nchini.


  Pia imeitaka serikali kuwa tayari kukarabati kwa haraka miundombinu ya usafirishaji pale itakapoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

  Kwa upande wake, BoT imesema itakuwa makini kuratibu mzunguko wa fedha na soko la kubadilisha fedha, ili kukabiliana na dalili zozote zitakazoashiria kuongezeka kwa bei ya huduma na bidhaa kunakosababishwa na mzunguko mkubwa wa fedha au soko la kubadilisha fedha.

   
Loading...