Bei ya Ng'ombe wa Maziwa

Bora ukafuga hata kitimoto endapo utakuwa mkiristo kuliko hao ngombe.(samahani)

usipowaogesha dawa na wao wakangatwa na kupe anayesababisha ugonjwa wa (ndagama) mwezi mmoja Ni mwingi Sana utaamka na mzoga.

wanahitaji matunzo ya Hali ya juu ili watoe faida unayoitaka wewe kinyume na hapo utakuwa umejiongezea majukumu yasiyo na msingi.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Upande wa kupe co kweli sababu hatuchungi Ng’ombe wanaokuja na nyasi wachache sana kuogesha ni ratiba tu unaweka dawa kibao na serikali imefuta kodi kwenye dawa za mifugo
 
Ni kweli mkuu Ila kupe anaweza akasafiri toka sehemu moja Hadi nyingine. mfano kwa hapa Moro Kuna wamasai wanaofuga ngombe wa kawaida Sasa hawa wanakuwa na kupe. Kama eneo alilopo ngombe wa maziwa Lina kawaida ya kupita ngombe wa kawaida lazima na yeye apate kupe tu. ndo maana wanaogeshwa kila baada ya muda fulani.

Nina uzoefu na Hawa ng'ombe ndo wamenisomesha shule.
 
Good advice, though kufuga nguruwe ni kitu nimefikiria kufanya pia.

Stick kwenye vision yako epukana na wakatishaji tamaa, ukiamua kufuga chochote kile lazima ujiandae kwa matibabu na usafi, hata hao nguruwe wanahitaji matibabu, kuku wanahitaji matibabu, hakuna mfugo usiohitaji matibabu kuna walioanza na nguruwe baadae wakaamia kufuga ng'ombe. Ukisikiliza watu hasa humu mitandaoni hutofanya chochote kwa sababu kila mmoja ana mtizamo wake.
 
That's cool
 
Ngombe akizaa baada ya miezi 4 unaweza kumpandisha Tena akiingia tu kwenye joto.na baada ya kuhakikisha ameshika mimba utaendelea kumkamua Hadi afikishe miezi 7toka siku apanidishwe Ina maana Ni miezi miwili kabla ya kuzaa ,hii itamfanya apate nguvu kipindi Cha kuzaa

Wakati wa kumkamua anatakiwa ale ashibe majani na maji ya kutosha Kama Mimi Nina ngombe anakunywa maji Lita 60 kwa siku asubuhi 20 mchna 20 na jioni 20
 
Habarini watu wa nguvu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Eti ng'ombe wa maziwa anaweza akawa anauzwa shilingi ngapi na naweza kumpata wapi (mimi nipo Morogoro), vipi kuhusu uzalishaji wa maziwa, anatoa lita ngapi kwa mkamuo mmoja na Je sehemu gani naweza nikauza maziwa yakaisha kwa haraka, hata kama ikiwa ni mkoani.

Natumaini majibu mazuri kutoka kwenu.
Ng'ombe wa maziwa wanapatikana katika mkoa wa mbeya wilaya ya Rungwe, ng'ombe mmoja anaweza toa lita 15 asubuhi na 13 jioni ivyo kwa siku inaweza toa lita 28 na kuendelea, ikumbukwe kwamba anazaa baada ya miez 9 anaanza kukamuliwa siku hiyo hiyo Lakin baada ya siku Tatu ndipo maziwa yanaweza kutumika na kuuzwa, kama anapata malisho bora, madini na mazingira safi atapata joto tena baada ya miez miwili na kupandwa na atakamuliwa mpaka mimba ifike miezi saba ataachishwa kwajili ya kumwandaa kuzaa tena. Wanapatikana kwanzia 1.5 kuendelea kama utahitaji mawasiliano zaidi namba zangu ni 0756416149, 0717847599. Nipo rungwe karibu saana namba ya voda ipo watsap hata picha ntakurushia kama utahitaji
 
Ahsante kaka kwa ushirikiano wako
 
watu wengi wametoa maelezo mazuri sana ila jambo napenda kukusisitizia wakati wa ununuzi wa ng'ombe hasa kwa mtu mmoja mmoja ni kupata historia ya uzao wa ng'ombe huyo, maana mama anaweza kuwa mzuri sana ila dume anaweza kuwa kituko yani si dume apatikanae kwenye ukoo wa maziwa.

Pia changamoto kubwa kwa wafugaji wengi hawana madume (hawakai na madume yalozaliwa) nikutokana na changamoto za madume ya ng'ombe. Ununuzi wa mbegu kwaajili ya kupandikiza nao ni changamoto baadhi ya sehemu kwahiyo watu hupandisha dume lolote liliopo karibu kwahiyo kwenye ununuzi wako zingatia haya, ni madogo ila impact yake ni kubwa sana katika utoaji wa maziwa
 
Stick kwenye vision yako epukana na wakatishaji tamaa, ukiamua kufuga chochote kile lazima ujiandae kwa matibabu na usafi, hata hao nguruwe wanahitaji matibabu, kuku wanahitaji matibabu, hakuna mfugo usiohitaji matibabu kuna walioanza na nguruwe baadae wakaamia kufuga ng'ombe. Ukisikiliza watu hasa humu mitandaoni hutofanya chochote kwa sababu kila mmoja ana mtizamo wake.
Inashuriwa kuchanganya. Nguruwe Wana homa yqo ikija wanakufa banda.lote utamkumbuka ngimbe
 
Upande wa kupe co kweli sababu hatuchungi Ng’ombe wanaokuja na nyasi wachache sana kuogesha ni ratiba tu unaweka dawa kibao na serikali imefuta kodi kwenye dawa za mifugo
Mkuu haohao kupe wachache wanaokuja na nyasi wanaweza kuleta ugonjwa kwa ng'ombe pia sio mpaka uchunge.
 
Ng'ombe wa maziwa wanapatikana katika mkoa wa mbeya wilaya ya Rungwe, ng'ombe mmoja anaweza toa lita 15 asubuhi na 13 jioni ivyo kwa siku inaweza toa lita 28 na kuendelea, ikumbukwe kwamba anazaa baada ya miez 9 anaanza kukamuliwa siku hiyo hiyo Lakin baada ya siku Tatu ndipo maziwa yanaweza kutumika na kuuzwa, kama anapata malisho bora, madini na mazingira safi atapata joto tena baada ya miez miwili na kupandwa na atakamuliwa mpaka mimba ifike miezi saba ataachishwa kwajili ya kumwandaa kuzaa tena. Wanapatikana kwanzia 1.5 kuendelea kama utahitaji mawasiliano zaidi namba zangu ni 0756416149, 0717847599. Nipo rungwe karibu saana namba ya voda ipo watsap hata picha ntakurushia kama utahitaji
Mkuu naona umesahau, kuna ng'ombe wengine mpaka maziwa kutakata na kufaa kutumiwa ni zaidi ya siku tatu tangu kuzaa
 
Wadau mnaotafuta Ngombe kuweni makini na picha za mtandaoni kama unaweza kumfuata ngombe huko anako uzwa na ukamkagua itapendeza zaidi. Picha nyingi za mtandaoni hazina uhalisia.
 
Habarini watu wa nguvu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Eti ng'ombe wa maziwa anaweza akawa anauzwa shilingi ngapi na naweza kumpata wapi (mimi nipo Morogoro), vipi kuhusu uzalishaji wa maziwa, anatoa lita ngapi kwa mkamuo mmoja na Je sehemu gani naweza nikauza maziwa yakaisha kwa haraka, hata kama ikiwa ni mkoani.

Natumaini majibu mazuri kutoka kwenu.
Vp ulishaanza ufugaji?
 
Wilaya ya Rungwe na Busokelo zinazalisha maziwa kwa wingi sana na ng'ombe wazuri wa maziwa wanapatikana kwa bei nafuu. Mitamba na Ndama breed nzuri kutoka kitulo wanapatikana

Mimi na organize wahitaji na kuwapeleka kwa wafugaji moja kwa moja ili kuwaepusha na madalali ambao wanafanya bei kuwa kubwa zaidi. Wapo ng'ombe wanaotoa lita zaidi ya 20 kwa siku Ndama wazuri mitamba na madume.

Wapo watu ambao tayari nimeshafanyanao kazi kwa ufanisi na kufanikisha mahitaji yao. Kwa wahitaji nitafute kwa namba 0756416149 FOR SURE YOU WILL NEVER REGRET.
 
Kwa wale wafugaji hasa wa mikoa yenye gharama kubwa ya chakula sasa Bei kubwa ya chakula isikukwamishe kufuga. Sasa unaweza pata chakula cha mifugo pia nafaka mbalimbali kwa bei halisi ya mkoani

Unachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na nasi katika group letu huwa tunapakia na kusafirisha hadi mkoa ulipo kwa bei ya mkoani na nafuu zaidi

Vyakula unavyoweza pata
1. Pumba za mahindi
2. Pumba za mpunga laini kwaajili ya nguruwe
3. Mashudu
4. Uduvi
5. Chakula cha kuchanganywa
6. Na vyakula vingine kwa order ya mteja husika kama uduvi, mahindi, chenga za dagaa, nk

Back
Top Bottom