Bei ya mahindi Songea kizungumkuti, tofauti ya bei ya mahindi na mbolea ni kama mbingu na ardhi

Unajifanya mjinga ni mwenyewe your choice your future. Wasilalamike hiyo ndiyo future waliochagua
Hujitambui hivi kwenye nchi kuna rais wangapi w Jamhuri, acha umbulula .unajifanya mjuaji kumbe zero brain
 
By then. who that is making complaints acha utoto mpe mwenzie njia sio kejele after all unaweza kuta mtoto wa maka kula kulala bure
Nimempa suruhu nayo ni your choice your future usichague mtu ambaye anaona wivu hata jaji kwenda South kula bata unategemea nini
 
Debe la mahindi limeshuka mpaka 3,500/ sasa hivi, wakati mwaka jana liligonga Tsh 15,000. Hii ni hatari sana kwa wakulima. Msimu kama huu mwaka jana unga ulikuwa 38,000/ kwa kilo 25 pale Njombe mwaka jana na maharage yalikuwa Tsh 35,000/ kwa debe moja. Lakini mpaka jana unga 25kg pale njombe ni Tsh 20,000/ na maharage ni Tsh 30,000/ japokuwa vijijini kule Lupembe maharage ni Tsh 20,000/. Waliokopa pembejeo watalipaje madeni yao?

Nikiangalia jinsi ambavyo mkulima huyu anavyoshindwa kuchomoka kwenye lindi la umaskini, napata wasiwasi mkubwa na kizazi cha kesho juu ya kupenda kilimo. Zamani tulikuwa tunatoka kijijini kwenda mjini tukiwa na zawadi za unga/nafaka/maharage sasa hivi ni kinyume, inabidi uende na chakula kijijini.

Haya mambo ya kupiga marufuku kuuza chakula nje kwa kuhofia njaa, msalaba anabeba mkulima peke yake, hapa ndio kuna mzizi wa fitina.
 
Mkuu Natus umewaambia vyema kabisa,kwa mkoa wa ruvuma wanaweza kulima hata maharagwe na soya na ukapiga hela.Sio kusikiliza wanasiasa tu.Bali tafuteni wataalamu wa kilimo wawasaidie.Kilimo cha mazoea kimepitwa na wakati
Ndugu ni rahisi kusema ila kilichowakuta wakulima Ruvuma msimu huu mungu anajua, hizo soya ndo usiseme kabisa!
 
Ndugu ni rahisi kusema ila kilichowakuta wakulima Ruvuma msimu huu mungu anajua, hizo soya ndo usiseme kabisa!
Msimu huu hakuna cha mahindi wala maharage, maharage mapya yameshuka mpaka Tsh 15,000/ kwa debe kule Lupembe wakati ambapo msimu huu mwaka jana ilikuwa 35,000/ bila chenga. Mahindi ndio hayo Tsh 3,500/ mpaka 4000/ ukibahatika.

Hao hao Wanalizombe waliotia nguvu kwenye Tangawizi maeneo ya Madaba, bei imeshuka mpaka Tsh 500/ toka Tsh 4,000/ ya 2015.Na wale waliojishaua kulima Mbaazi, nadhani kila mtu anajua. Na sisi tuliootesha miti ya mbao maeneo ya Madaba biashara imedoda mbaya, hata wale wakuuza miche wanatoa macho, hakuna wa kununua.
 
Mkuu ni wapi huko debe la mahindi ni 3,500?

hapana hata mimi ni mkulima wa mahindi nina shamba sehem yenye ukame sijawahi tumia mifuko 3 kwa hekari 1, natumia kilo 20 tu kwa hekari moja na sio gunia 3
Ukilima heka 1 utatumia jumla ya mifuko 3 na ukizingatia mashart km palizi na kuweka mbolea kwa wakati utavuna gunia 17-22 kwa heka hivyo ukiuza hata gunia kea elf 20 utapata wastani Wa tsh400000 kwa heka wakati mbolea Itakuwa ni tsh 150,000. Tusikate tamaa tuendelee kulima
 
Kwani bei ya mahindi ikiwa 24000 na mbolea ikiwa 58000 kuna ahida gani? Kama ungekuwa unavuna gunia moja ndio ingekuwa tatizo. Kama unatumia mbolea mfuko m1 na unapata mahindi gunia 10 mbona sawa tu.

Limeni acheni uvivu
Kwa hiyo hizo gunia kumi,zilizalishwa kwa mbolea tu??, Hapo hujaweka gharama za kukodi shamba, kuandaa, kulima, kupanda, kununua mbegu, madawa, palizi, Kuvuna, kupura, kununua mifuko, kupakia, Usafirishaji kwenda Sokoni, hizi zote ni gharama za uzalishaji nje na mbolea, hivi kuna faida kweli hapo? Kumbuka hujaweka vitu km Mafuriko, ukame, na Wadudu wavamizi, mambo yanayoathiri sana mavuno.
 
Nahitaji tani 30 za mahindi ya sembe kila baada ya wiki mbili 0764800989 Alfred, kiwanda changu kiko Kigamboni
 
Ukilima heka 1 utatumia jumla ya mifuko 3 na ukizingatia mashart km palizi na kuweka mbolea kwa wakati utavuna gunia 17-22 kwa heka hivyo ukiuza hata gunia kea elf 20 utapata wastani Wa tsh400000 kwa heka wakati mbolea Itakuwa ni tsh 150,000. Tusikate tamaa tuendelee kulima
Gharama si mbolea tu, ni vingi sana mbolea ni kitu kimojawapo ili kufika hatua ya kuyapaki magunia ya mahindi. Kwa hali hii kazi tunayo sisi wakulima.
 
Back
Top Bottom