Bei ya magari ya japani: Kwanini ni nafuu, kwa nini ipo juu

punguzo

Member
Joined
Jul 9, 2011
Messages
51
Points
0

punguzo

Member
Joined Jul 9, 2011
51 0
Mdau, Yafuatayo ni maoni yangu kwa haraka haraka,ambayo ni jibu kwa wadau fulani walioniuliza kwanini bei ya gari fulani ipo juu. Naomba kwa pamoja tuchangie kwa manufaa ya wote.

Najua, Watanzania wengi ni wazuri wa kulialia, kulalamika na kutafuta visababu vidodo vidogo ili wapunguziwe bei au wauziwe kwa bei ya chini sana( Mwisho wanaishia kununua vitu fake).

Pia imekuwa kama hulka yetu kudharau biashara za wenzetu, kuzikandia, kuponda, kusengenya na kuzidharirisha. Tumekuwa na tabia ya kushusha hadhi na bei ya bidhaa/biashara za wenzetu huku tukijifanya tunajua mazingira na mzunguko wa biashara hiyo wakati hatujui. Tunasahau ya kuwa tunaharibu biashara za watu mwingine (hii husababisha biashara nyingi kufa).

Kwa kifupi, Bei ya bidhaa hutokana na mazingira yanayoizunguka biashara hiyo, ubora na hadhi ya bidhaa, upatikanaji, ukubwa wa biashara/ kampuni, usafirishaji, umuhimu wa bidhaa, kodi, malengo ya muuzaji na mambo mengine mengi.

Kuhusu bei za magari yatokayo Japan, Siku za mwanzo watu wengi walikuwa wanaship magari ya wizi hivyo ilifanya kushusha bei halisi ya magari.

Pia kunawafanya biashara wengi( Hasa wakubwa) ambao wanakwepa kodi au wanatumia exemption fake, hawa wanasababisha kushuka kwa bei halisi ya magari , pia wanachangia kushuka kwa pato la serikali kwa kukwepa kodi.

Kutokana na kuyumba kwa uchumi wa dunia, Wajapan wengi walikosa kazi za kuajiliwa na kuamua kujiajiri katika sekta Magari used. Ikumbukwe ya kuwa Wajapan wengi wanauwezo wa kupata magari ya bure (Dumping cars) au magari ya bei nafuu yenye migogoro au yaliyopata ajari kwa bei ya chini kabisa hivyo kuwafanya wawe kwenye nafasi nzuri ya kuuza kwa bei ya chini.

Siku za nyuma, ambapo magari yalikuwa bei rahisi kuna baadhi ya makampuni makubwa ya kijapan yalinunua magari mengi na kuyaweka kwenye stock. Haya makampuni kwa sasa wanayauza haya magari kwa bei ya chini mno, ndo maana magari ya miaka ya nyuma ni bei rahisi sana kulinganisha na magari ya miaka ya hivi karibuni.

Kuna magari yaliyo athirika na mafuriko ya tsunami, active radiator, Nuclear, haya huuzwa kwa bei ya chini Mno na madhara yake kiafya ni makubwa mno ( KANSA NI ZA KUFIKIA). Pia injini zake ndo kama zinavyo waharibikia kila siku.

Kuna magari yanaitwa accedental/broken cars haya ni magari yaliyopata ajari, damped, damaged, yenye matatizo ya injini, na matatizo mengine mbalimbali na kuwa solved. Haya magari bei yake ni nafuu sana. Ukweli ni kwamba ongezeko la haya magari, limesababisha ongezeko la kushamili kwa biashara ya spare parts. Wabongo wengi wamenunua Magari haya na hata kabla ya mwaka mmoja kuisha wanajikuta wameingia katika biashara ya manunuzi ya spare parts. wanakwepa bei halisi ya magari au wanakwepa tofauti ya USD 1,000/ lakini ukichambua gharama za kufix hilo gari miaka miwili baada ya kulinunua utakuta ni sawa na gharama za kununua magari mawili kwa bei inayokubarika. Na ndio maana magari mengi bongo baada ya miaka miwili mitatu utayakuta juu ya mawe.

Anyway, kuna mazingira mengi yanayofanya magari ya japan kuwa bei chini na juu, unatakiwa kuwa makini, na kunamambo mengi sana yakujadili katika biashara hii, kuliko mtu kukurupuka na kuanza kushambulia biashara za watu hasa wajasiriamali wadogo wadogo.

Lakini pia mwisho wa yote, wewe kama Mtanzania unayependa maendeleo na usiokwisha kuilaumu serikali ya CCM au unayetaka Chadema ilete mabadiliko, Unatakiwa kununua magari/ bidhaa kutoka kwenye makampuni ya watanzania wazalendo wenzako na sio kusujudu makampuni ya kigeni. Ukweli ni kwamba ukinunua magari kwenye kampuni ya kijapan utakuwa umesaidia kukuza uchumi wa taifa la japan, na kuwaongezaa ajira na kipato, na ukinunua kutoka kwenye kampuni la mzalendo mwezako utakuwa umesaidia kuongeza ajira na kipato kwa vijana wetu, umesaidia kuongeza pato la serikali kwa kupata kodi, utakuwa umesaidia maendeleo ya nchi na jamii yetu kwa sababu wamiliki wengi wa haya makampuni hutuma remmitances nyumbani, ambazo zinasaidia familia, zinajenga majumba, zinalipia karo na huduma za afya, pia wamiliki wengi wa haya makambuni wanatabia ya kuwekeza katika shughuri balimbali za kijamii na kimaendeleo.

Nina mengi sana ya kusema ila kwa sasa aksanteni !
 
Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Messages
9,771
Points
2,000

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2011
9,771 2,000
Una mpango wa kupandisha bei ya ma scraper yako toka japan?? Kuna sababu nyingine ya kufanya magari hayo kuwa cheaper,ila ume step at your interest line
 
punguzo

Member
Joined
Jul 9, 2011
Messages
51
Points
0

punguzo

Member
Joined Jul 9, 2011
51 0
Una mpango wa kupandisha bei ya ma scraper yako toka japan?? Kuna sababu nyingine ya kufanya magari hayo kuwa cheaper,ila ume step at your interest line
Kwanza mimi siwezi nikanunua au kuuza scraper, nimejaribu kuelezea hali halisi ya magari mengi wanayonunua na kuuziwa watanzania wengi, ndoa maana kutwa hawaishi kupeleka magari yao garage. Ndio, kunasababu nyingi za kufanya magari kuwa cheaper, mimi nimeelezea baadhi ya sababu na wewe kama unafahamu tafadhari jadili sababu nyingine ziwe postive au negative haijalishi kwa manufaa ya wote kuliko kunishambulia kuwa nimejadili for my own interests.
 
KASHOROBANA

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Messages
3,244
Points
1,500

KASHOROBANA

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2011
3,244 1,500
JAMANI KWA NINI UNUNUE GARI SHOWRUMs ZA TANZANIA? WKT ATA UYO MUUZAJ KANUNUA KT MTANDAO NA SASA ANATAKA KULA CHA JUU KINONO TU? NENDA KT MTANDAO UNAOUZA MAGARI MAZURI KWA BEI POA UTAYAKUTA UKO CHAGUA ZURI, LZM UZINGATIE LIWE LA MWAKA 2004 KUEPUKE UCHAKAVU, PAY THRU PAY TRADE KWA USALAMA WA DOLA ZAKO, MSIDANGANYWE
 
punguzo

Member
Joined
Jul 9, 2011
Messages
51
Points
0

punguzo

Member
Joined Jul 9, 2011
51 0
Una mpango wa kupandisha bei ya ma scraper yako toka japan?? Kuna sababu nyingine ya kufanya magari hayo kuwa cheaper,ila ume step at your interest line
Kweli JF ni kiboko, hii ina refrect tabia za Watanzania tulio wengi baada ya kujadili kitu wewe unaanza kunishambulia, tena unaonekana ni mvivu wa kusoma na hujui kuelewa. Mimi nimesema kunawadau wamenilalamikia kuwa nime-display bei juu, nikawambia sababu kuonyesha sio scraper wewe unakurupuka eti scraper zangu, kweli wewe nimuelewa au ndo kama nilivyo sema kuna watu wanadharau watu wengine na biashara zao hasa wajasiriamali wadogo wadogo? be postive mate!
 
King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
34,506
Points
2,000

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
34,506 2,000
Watanzania mna tamaa sana ndio maana watu hawataki kununua kwenu yani nyie cha juu mnaweka hadi dola 2000 kwa gari acheni hizo!!! Gari japani inauzwa usd1200 +ispection 200+freight 1000+jeck spare 100 Total 2500 lkn nyie mnauza hadi usd 5000 mwish 4500 usd CIF to Dsm acheni wizi nyie!!
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Messages
9,244
Points
2,000

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined May 7, 2010
9,244 2,000
Mdau, Yafuatayo ni maoni yangu kwa haraka haraka,ambayo ni jibu kwa wadau fulani walioniuliza kwanini bei ya gari fulani ipo juu. Naomba kwa pamoja tuchangie kwa manufaa ya wote.

Najua, Watanzania wengi ni wazuri wa kulialia, kulalamika na kutafuta visababu vidodo vidogo ili wapunguziwe bei au wauziwe kwa bei ya chini sana( Mwisho wanaishia kununua vitu fake).

Pia imekuwa kama hulka yetu kudharau biashara za wenzetu, kuzikandia, kuponda, kusengenya na kuzidharirisha. Tumekuwa na tabia ya kushusha hadhi na bei ya bidhaa/biashara za wenzetu huku tukijifanya tunajua mazingira na mzunguko wa biashara hiyo wakati hatujui. Tunasahau ya kuwa tunaharibu biashara za watu mwingine (hii husababisha biashara nyingi kufa).

Kwa kifupi, Bei ya bidhaa hutokana na mazingira yanayoizunguka biashara hiyo, ubora na hadhi ya bidhaa, upatikanaji, ukubwa wa biashara/ kampuni, usafirishaji, umuhimu wa bidhaa, kodi, malengo ya muuzaji na mambo mengine mengi.

Kuhusu bei za magari yatokayo Japan, Siku za mwanzo watu wengi walikuwa wanaship magari ya wizi hivyo ilifanya kushusha bei halisi ya magari.

Pia kunawafanya biashara wengi( Hasa wakubwa) ambao wanakwepa kodi au wanatumia exemption fake, hawa wanasababisha kushuka kwa bei halisi ya magari , pia wanachangia kushuka kwa pato la serikali kwa kukwepa kodi.

Kutokana na kuyumba kwa uchumi wa dunia, Wajapan wengi walikosa kazi za kuajiliwa na kuamua kujiajiri katika sekta Magari used. Ikumbukwe ya kuwa Wajapan wengi wanauwezo wa kupata magari ya bure (Dumping cars) au magari ya bei nafuu yenye migogoro au yaliyopata ajari kwa bei ya chini kabisa hivyo kuwafanya wawe kwenye nafasi nzuri ya kuuza kwa bei ya chini.

Siku za nyuma, ambapo magari yalikuwa bei rahisi kuna baadhi ya makampuni makubwa ya kijapan yalinunua magari mengi na kuyaweka kwenye stock. Haya makampuni kwa sasa wanayauza haya magari kwa bei ya chini mno, ndo maana magari ya miaka ya nyuma ni bei rahisi sana kulinganisha na magari ya miaka ya hivi karibuni.

Kuna magari yaliyo athirika na mafuriko ya tsunami, active radiator, Nuclear, haya huuzwa kwa bei ya chini Mno na madhara yake kiafya ni makubwa mno ( KANSA NI ZA KUFIKIA). Pia injini zake ndo kama zinavyo waharibikia kila siku.

Kuna magari yanaitwa accedental/broken cars haya ni magari yaliyopata ajari, damped, damaged, yenye matatizo ya injini, na matatizo mengine mbalimbali na kuwa solved. Haya magari bei yake ni nafuu sana. Ukweli ni kwamba ongezeko la haya magari, limesababisha ongezeko la kushamili kwa biashara ya spare parts. Wabongo wengi wamenunua Magari haya na hata kabla ya mwaka mmoja kuisha wanajikuta wameingia katika biashara ya manunuzi ya spare parts. wanakwepa bei halisi ya magari au wanakwepa tofauti ya USD 1,000/ lakini ukichambua gharama za kufix hilo gari miaka miwili baada ya kulinunua utakuta ni sawa na gharama za kununua magari mawili kwa bei inayokubarika. Na ndio maana magari mengi bongo baada ya miaka miwili mitatu utayakuta juu ya mawe.

Anyway, kuna mazingira mengi yanayofanya magari ya japan kuwa bei chini na juu, unatakiwa kuwa makini, na kunamambo mengi sana yakujadili katika biashara hii, kuliko mtu kukurupuka na kuanza kushambulia biashara za watu hasa wajasiriamali wadogo wadogo.

Lakini pia mwisho wa yote, wewe kama Mtanzania unayependa maendeleo na usiokwisha kuilaumu serikali ya CCM au unayetaka Chadema ilete mabadiliko, Unatakiwa kununua magari/ bidhaa kutoka kwenye makampuni ya watanzania wazalendo wenzako na sio kusujudu makampuni ya kigeni. Ukweli ni kwamba ukinunua magari kwenye kampuni ya kijapan utakuwa umesaidia kukuza uchumi wa taifa la japan, na kuwaongezaa ajira na kipato, na ukinunua kutoka kwenye kampuni la mzalendo mwezako utakuwa umesaidia kuongeza ajira na kipato kwa vijana wetu, umesaidia kuongeza pato la serikali kwa kupata kodi, utakuwa umesaidia maendeleo ya nchi na jamii yetu kwa sababu wamiliki wengi wa haya makampuni hutuma remmitances nyumbani, ambazo zinasaidia familia, zinajenga majumba, zinalipia karo na huduma za afya, pia wamiliki wengi wa haya makambuni wanatabia ya kuwekeza katika shughuri balimbali za kijamii na kimaendeleo.

Nina mengi sana ya kusema ila kwa sasa aksanteni !
Umejitahidi lakini kumbuka kuwa tuko kwenye era ya globalization phase III.
 
punguzo

Member
Joined
Jul 9, 2011
Messages
51
Points
0

punguzo

Member
Joined Jul 9, 2011
51 0
Watanzania mna tamaa sana ndio maana watu hawataki kununua kwenu yani nyie cha juu mnaweka hadi dola 2000 kwa gari acheni hizo!!! Gari japani inauzwa usd1200 +ispection 200+freight 1000+jeck spare 100 Total 2500 lkn nyie mnauza hadi usd 5000 mwish 4500 usd CIF to Dsm acheni wizi nyie!!
USD1200 = 98,852Yen, Hakuna gari ya maana inayouzwa hiyo bei kama siyo stock ya zamani au ni accedental car. Ndio maana hamuishi kuzipeleka garage, Gharama nyingine unakaribia kwenye usahihi.

Kuhusu faida hata makampuni hayo ya kijapan huwa yanaweka faida kati ya dola 500- 1000 kulingana na ukubwa wa kampuni/ biashara. sasa kama unasema gari linauzwa USD 1200 inamaana hata wajapan wananunua gari kwa USD kati ya 200 - 700 kitu ambacho hakipo au ndo kama ninavyosema hiyo itakuwa dumped car bro!
 
lowale

Senior Member
Joined
Aug 10, 2012
Messages
198
Points
225

lowale

Senior Member
Joined Aug 10, 2012
198 225
mimi nataka kukuunguungisha wewe mtanzania mwenzangu ,ila swali langu ni hili hayo magari unayatengeeza wewe au nawe unaagiza hayo hayo ya bei rahisi yenye madhara unaweka hapo cha juu then unatuuzia ???????
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Messages
8,620
Points
1,225

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2009
8,620 1,225
Naona jamaa amekuja kujitangazia biashara yake imedodaaa......!
Siku hizi watu wajanja wanaagiza wenyewe.......!
Magari ya showrooms/yard yananyofolewa spares oroginal na kubandokwa vipuli vilivyochakaa linabaki likopo tu kwa muonekano mzuri kwa nje kumbe hamna kitu......!
Mie naagiza gari toka japani kamwe sinunui toka showroom/yard.........!
 
King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
34,506
Points
2,000

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
34,506 2,000
USD1200 = 98,852Yen, Hakuna gari ya maana inayouzwa hiyo bei kama siyo stock ya zamani au ni accedental car. Ndio maana hamuishi kuzipeleka garage, Gharama nyingine unakaribia kwenye usahihi.

Kuhusu faida hata makampuni hayo ya kijapan huwa yanaweka faida kati ya dola 500- 1000 kulingana na ukubwa wa kampuni/ biashara. sasa kama unasema gari linauzwa USD 1200 inamaana hata wajapan wananunua gari kwa USD kati ya 200 - 700 kitu ambacho hakipo au ndo kama ninavyosema hiyo itakuwa dumped car bro!
Acha hizo wewe ebu ingia mtandaoni uone gx100 cif usd 2000,gx110 3000 na verossa 3200! Au sio gari za maana hizo? Au mwenzetu unauza Aston Martin,Maybach,Vogue,Hummer,Limo?
 
aye

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
2,096
Points
1,500

aye

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
2,096 1,500
jamaa yangu alinunua gari showroom baada ya wiki mbili likaibiwa kufuatilia kakuta walibaki na funguo mmoja wakalichukua kama lao sina hamu na showroom zetu bora kuagiza kwa kuzingatia ubora mbona hao wa showroom nao wanaagiza au kunatofauti ya kuagiza mwenyewe na kuagiza mwenye showroom
 
Voice of Wisdom

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Messages
537
Points
225

Voice of Wisdom

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2011
537 225
kwani hizo kampuni zinayanunua hayo magari kutoka wapi? Je ni tanzania au nje ya tanzania?
Kama ni nje ya tanzania, je unajua kila gari inayoingia nchini lazima ilipiwe kodi?
Kama kila gari inayoingia nchini lazima kodi ilipwe unamaanisha nini unaposema tununue gari toka ktk kampuni za kitanzania ili tuchangie uchumi kwa kulipa kodi?
 
mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
11,804
Points
2,000

mgt software

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
11,804 2,000
huyu jamaa anajua kujipigia debe, mimi mzoefu wa kununua magari nje, nkaa nayo miaka hadi minne na kuuza, ina maana jaai hawana akili kukagua viwango, viwango vya gari vinakaguliwa na komputa baba, hizo zako ni story tu. Watanzania wenye yadi kama za wale jamaa wakina super tall na ndama mtoto wa ng'ombe ndio yadi unayotaka twende? mwenye mapepe na hela ndio ununua hapa , lkn yote sawa endelea kujipigia debe.
 
Forum statistics

Threads 1,392,813
Members 528,696
Posts 34,118,717
Top