Bei ya mafuta yapanda maradufu. Petroli bei yaongezeka kwa kati ya Tsh. 100 - 321

Cha kushangaza mafuta haya yalinunuliwa kwa bei iliyokuwa chini kabla ya vita hiyo ya Ukraine. Iweje bei ipandishwe haraka namna hii? Wasiwasi wangu ni kwamba tunaandaliwa kisaikolojia kujiandaa na bei ambazo zitapanda zaidi hivi karibuni. Kaeni chonjo.
Mafuta yamenunuliwa March, Vita imeanza tarehe 24 Feb

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bei ya mafuta kwenye soko la dunia imepanda ila mechanism ya kuyapata mafuta huwa sio sawa Na pipi. Mafuta huendi Na kununua tu. Yanaagizwa kwa bulk purchase.

Halafu yanachimbwa, kusafishwa Na kusafirishwa ni span ya three month. How come price ireflect price ya February 25? Pia soko la Brent crude oil at the point no $105. Just bado hakuna justification ya price kuongezeka vile. Inabidi tuulize maswali kitaalamu. We ain't stupid!!
Haya andamana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuanzia kesho Jumatano, Aprili 6,2022 bei mpya ya petrol kwa mafuta yanayopokelewa kupitia Bandari ya Dar es salaam itakuwa Sh2,861 kutoka Sh 2,540 ikiwa ni ongezeko la Sh321.

Kwa upande wa dizeli bei mpya itakuwa Sh2,692 kutoka Sh2,403 ya sasa ikiwa ni ongezeko la Sh289. Bei ya mafuta ya taa itapanda kutoka Sh2,208 hadi Sh2,682 ikiwa ni wastani wa Sh474.

Maganga amesema mafuta ambayo yatapitia Bandari ya Tanga, bei ya petrol itakuwa Sh2,848 kutoka Sh2,563 ikiwa ni ongezeko la Sh285.

Kwa upande wa dizeli bei itaongezeka kutoka Sh2,484 hadi Sh2,779 ikiwa ni ongezeko la Sh295 kwa lita moja.

Mafuta ambayo yatapokewa kupitia Bandari ya Mtwara bei ya petrol kwa lita moja itakuwa Sh2,678 kutoka Sh2,577 ikiwa ni ongezeko la Sh100.

Bei ya dizeli kwa lita moja itakuwa Sh2,811 kutoka Sh2,530 ikiwa ongezeko la Sh281.
Ukitazama bei kwanini ongezeko la bei la Mtwara ambako ni mbali zaidi lipo chini kuliko la Dar
 
Magari ya umeme yanakuja lini ? Hivi wadau haya magari ya umeme kwa mnaoelewa kidogo tufahamisheni upande wa kuchaji hilo gari yatakuepo maeneo maalum kwa ajili ya kuchaji kama zilivyo petrol station au pia litakua na choice kwamba unaweza ukalichaji magetoni ?
Na kama zitakuepo hizo charging station vipi muda wa kulichaji labda basi liko njiani kwenda Mwanza !! Maana kama simu tu zinachajiwa kuanzia nusu saa vp Mabasi ?
Shida ipo pale pale, una gari la umeme Tanesco wanakuambia wana maintenance ya mitambo mwezi mzima.
 
Mafuta yamenunuliwa March, Vita imeanza tarehe 24 Feb

Sent using Jamii Forums mobile app
Refer #168
QUOTE
"Bei ya mafuta kwenye soko la dunia imepanda ila mechanism ya kuyapata mafuta huwa sio sawa Na pipi. Mafuta huendi Na kununua tu. Yanaagizwa kwa bulk purchase.

Halafu yanachimbwa, kusafishwa Na kusafirishwa ni span ya three month. How come price ireflect price ya February 25? Pia soko la Brent crude oil at the point no $105. Just bado hakuna justification ya price kuongezeka vile. Inabidi tuulize maswali kitaalamu. We ain't stupid!!" EOQ.
 
Wakati Serikali ikitangaza kurejesha Sh100 katika mafuta, watumiaji wa nishati hiyo watalazimika kufunga mkanda kutokana na bei kuendelea kupaa.

Bei ya nishati hiyo inapanda wakati wananchi wakilalamika kupaa kwa bei za bidhaa mbalimbali za vyakula hasa wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hata hivyo, vita vya Russia na Ukraine ambavyo vimedumu kwa zaidi ya mwezi sasa navyo vinatajwa kupandisha bei ya nidhati hiyo kwenye soko la dunia. Russia ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Jumanne Aprili 5, 2022 Mkurugenzi wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Gerald Maganga amesema kuanzia kesho Jumatano, Aprili 6,2022 bei mpya ya petrol kwa mafuta yanayopokelewa kupitia Bandari ya Dar es salaam itakuwa Sh2,861 kutoka Sh 2,540 ikiwa ni ongezeko la Sh321.

Kwa upande wa dizeli bei mpya itakuwa Sh2,692 kutoka Sh2,403 ya sasa ikiwa ni ongezeko la Sh289. Bei ya mafuta ya taa itapanda kutoka Sh2,208 hadi Sh2,682 ikiwa ni wastani wa Sh474.

Maganga amesema mafuta ambayo yatapitia Bandari ya Tanga, bei ya petrol itakuwa Sh2,848 kutoka Sh2,563 ikiwa ni ongezeko la Sh285.

Kwa upande wa dizeli bei itaongezeka kutoka Sh2,484 hadi Sh2,779 ikiwa ni ongezeko la Sh295 kwa lita moja.

Mafuta ambayo yatapokewa kupitia Bandari ya Mtwara bei ya petrol kwa lita moja itakuwa Sh2,678 kutoka Sh2,577 ikiwa ni ongezeko la Sh100.

Bei ya dizeli kwa lita moja itakuwa Sh2,811 kutoka Sh2,530 ikiwa ongezeko la Sh281.

Hata hivyo, Maganga amesema kuwa bei hizo zimejumuisha tozo ya Sh100 ambayo Serikali ilitangaza kuiondoa mwezi Machi, 2022 kabla ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kuirejesha akisema utaribu wa kuindoa haukufuatwa kwa kuwa fedha hiyo ilishapangiwa bajeti.

====

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI
KUANZIA JUMATANO, TAREHE 6 APRILI 2022

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 6 Aprili 2022. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-

(a) Bei za rejareja na jumla za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 2 Machi 2022. Kwa Aprili 2022, bei za rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa shilingi 321/Lita (sawa na asilimia 12.65), shilingi 289/Lita (sawa na asilimia 12.04) na shilingi 473/Lita (sawa na asilimia 21.45), mtawalia. Vilevile, ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa shilingi 320.32/Lita (sawa na asilimia 13.29), shilingi 288.49/Lita (sawa na asilimia 12.69) na shilingi 472.40/Lita (sawa na asilimia 22.72), mtawalia.

(b) Kwa Aprili 2022, bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara) zimeongezeka ikilinganishwa na bei zilizotolewa tarehe 2 Machi 2022. Kwa Aprii 2022, bei za rejareja za petroli na dizeli zimeongezeka kwa shilingi 285/lita (sawa na asilimia 11.12) na shilingi 295/lita (sawa na asilimia 11.90), mtawalia. Vilevile, ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za petroli na dizeli zimeongezeka kwa shilingi 284.22/Lita (sawa na asilimia 11.68) na shilingi 294.66/lita (sawa na asilimia 12.52) mtawalia. Kutokana na kuisha kwa mafuta ya taa kwenye matanki ya kuhifadhia yaliyopo Tanga, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.

(c) Kwa Aprili 2022, bandari ya Mtwara imepokea mafuta ya dizeli tu hivyo, kwa
Aprili 2022 bei za rejareja na jumla za mafuta ya petroli kwa mikoa ya Kusini
(Mtwara, Lindi na Ruvuma) zitakuwa sawa na zile zilizotangazwa tarehe 2 Machi 2022. Kwa upande wa dizeli, kwa Aprili 2022, bei za rejareja na jumla za dizeli zimeongezeka ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita. Bei ya rejareja ya dizeli imeongezeka kwa shilingi 281/lita (sawa na asilimia 11.12) na bei ya jumla ya dizeli imeongezeka kwa shilingi 279.99/lita (sawa na asilimia 11.67). Kwa kuwa hakuna matanki ya kuhifadhi mafuta ya taa katika bandari ya Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika

(d) Mabadiliko haya ya bei yanachangiwa na kubadilika kwa bei za mafuta katika soko la dunia, gharama za usafirishaji (BPS Premium) na thamani ya shilingi ukilinganisha na dola ya kimarekani.

(e) EWURA inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

(f) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(g) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (Price cap) au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa kupitia Magazeti ya Serikali Na. 2A na 57 ya tarehe 3 Januari 2022 na 28 Januari 2022, sawia.

(h) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

(i) Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.
Okay
 
Sirikali ipunguze tozo bei ishuke
Screenshot_20220504-132334.jpg

View attachment 2211180
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom