Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,952
- 4,326
Wahenga walisema, 'Kufa kufaana'. Kwenye kila tatizo linalotokea hapa duniani huwa linafungua fursa kwa baadhi kufaidika nalo. Badala ya kukaa tunalialia linapotokea tatizo, tunapaswa kutazama upande wa pili wa shilingi kwamba tutafaidikaje na hilo tatizo. Hata lile tatizo kubwa la mlipuko wa covid 19, yapo makampuni na nchi zilizopiga pesa ile mbaya wakati wengine wakiwa wameji lockdown na zingependa mlipuko huu wa covid 19 uendelee kudumu!
Hii vita ya Urusi na Ukraine, mara tu ilipoanza nchi kama za Saudi Arabia na zingine zote za OPEC ziliona ni fursa, na zikaanza kupandisha bei ya mafuta yao. Nchi za Ulaya na Amerika walipoamua kususa mafuta ya Russia, nchi za OPEC na Saudia zikachangamkia fursa hiyo kwa kasi zaidi ya kuendelea kupandisha bei ya mafuta yao na hadi sasa yamefikia zaidi ya $ 120 kwa pipa. Kabla ya vita hii pipa lilikuwa linauzwa si zaidi ya $ 70. Nchi zingependa vita hii iendelee kudumu!
Russia ni mzalishaji mkubwa duniani wa mafuta haya ya petroli/ diseal na na gesi kwa kiwango cha theluthi moja ya mafuta yote duniani. Baada ya vita hii na nchi za Ulaya na Amerika kuanza kususia mafuta yake, Urusi imeteremsha sana bei ya mafuta yake hadi sasa kufikia $ 30 kwa pipa! Uchina na India wamechangamkia fursa hii, wananunua mafuta haya kutoka Russia na wangelipenda vita hii iendelee kudumu! Tukumbuke kuwa population ya China na India ni zaidi ya watu billion 3, yaani theluthi moja ya population ya dunia hii. Wao hawafungamani na upande wo wote kama sisi.
Sasa kwa nini na sisi tusichangamkie fursa hii ( na kupenda iendelee kudumu) kwa kununua mafuta haya toka Russia? Kuna tatizo gani tukifanya hivyo? Tunaogopa nini? Au watalaamu wety wa uchumi mnasemaje?

Unsold Oil Forces Russian Operator To Cap Pipeline Flows | OilPrice.com
Transneft, the Russian oil pipeline operator, has informed local oil companies that it would be capping the intake of yet-to-be-sold crude because of full storage as buyers in the West shun Russian oil
oilprice.com