Bei ya mafuta ya kupikia inawaondoa mamalishe barabarani, Serikali ichukue hatua za haraka

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Familia nyingi hapa nchini inawategemea akina mama katika maisha yao ya kila siku.

Mara nyingi mamalishe wamekuwa wakipika chapati, vitumbua, maandazi n.k kwa ajili ya kupata fedha ya kulisha familia zao.

Ni ukweli usiopingika kuwa athari ya kupanda kwa mafuta ya kupikia imewatoa barabarani ni familia nyingi zimekuwa hoi.

Serikali inaona hili na tunasubiri wachukue hatua za haraka isije ikawa kama suala la sukari ambayo ilipanda toka tshs.1,500 mpaka 3,000 na Serikali imenyamaza mpaka leo.
 
Kwanini awamu hii vitu vinaadimika Mara kwa Mara?
Sukari
Cement
Mafuta
Awamu ya kwanza tunajua ilikua Ni Vita ya nduli ndio ilisababisha, the tukainjoi Maisha kuanzia aliposhika AHM mpaka alipo ondoka Mh. JK
 
Mbona walisema kuna meli ya hayo mafuta kutoka nje imeshatia nanga bandarini! Na hivyo hili tatizo kubakia kuwa historia!! Bado tu hayajasambazwa kwa sisi walaji?

Tulianza na sukari, tukaja kwenye cement! Na sasa tuko kwenye mafuta ya kula! Tutafika tu.
 
Alizeti 5 litres 28,0000 Singida Fresh. Wengine kama Sun drop naona itakuwa 30,000 plus. Sukari bei ndiyo sijui. Mpaka chumvi imepanda bbeiro. Sembe ndiyo usiseme. Maharaja je ambayo ni mboga ya wengi mtaani? Aise life imekuwa kitendawili.
 
Mama ntilie wabadilishe mapishi badala ya maandazi wauze skonzi na mabanzi plus mikate ya ufuta, vibibi au watengeneze maandazi ya kupambia ambayo hayatumii mafuta mengi
 
Huyu Daniel Hajui Kujiereza Ni Darasa ra Saba
Ila Kwenye Matatizo Yenu Atawatetea Kule Bungeni
 
Back
Top Bottom