Bei ya mafuta sasa inavuka Tshs 2,000 kwa lita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei ya mafuta sasa inavuka Tshs 2,000 kwa lita

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ntemi Kazwile, Mar 10, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jamani bei ya mafuta inazidi kupaa wiki iliyopita tulikuwa tunanunua diesel kwa Tshs1,750 kwa lita lakini jana yamefika Tshs 2,000 (ongezeko la zaidi ya 14%). Je inawezekana hii nayo ikawa moja wapo ya hujuma (kupandisha bei hovyo ili kujipatia unfair profits)kwa kisingizio cha vurugu za Mashariki ya Kati na Kasikazini mwa Afrika?
  Sukari tuliambiwa inatakiwa iwe Tshs1,700 lakini inaendelea kusonga na bado tunaambiwa sukari ipo ya kutosha je serikali yetu imeshindwa kusimamia sheria zilizopo?
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kutokana na kupanda kwa mafuta nimeachana na usafiri binafsi sasa natumia Daladala, Mungu aepushie mbali nisije nikasitisha hata Chai nyumbani kwangu kwasababu ya kupanda kwa bei ya sukari. Nadhani nikifikia hatua hiyo hata bibi yangu ninaye mlea nyumbani kwangu ambaye ni mwana CCM atanielewa nikwanini sitaki kuwasamehe walioba kura yangu ili waendelee kutawala japo uwezo hawana.
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Tufungeni mikanda ili somo lituingie haswaaa, ili hapo 2015 tukiambiwa "Piga kura, Linda kura yako" tuelewe mara moja maana yake.

  Ila kwa vile binadamu ni wepesi wa kusahau, nachelea kusema 2013 mambo yatanyooka kidogo, tutazoea hali ya maisha ya bei juu juu, then ccm watakuwa wamevuna vya kutosha wataanza kutuonjesha taratibu hadi 2015 tutakuwa tulishalegea na kusema "Hata ccm siyo wote mafisadi, kuna wenye uchungu na nchi". Kwisha habari!!

  We have to define our own rules and protect them.
   
 4. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Serikali imeshindwa kabisa kuongoza, imechanganyikiwa haijui ifanye nini na ianzie wapi! Ina fikiri CHADEMA ndo inasababisha yote haya!
   
Loading...