Bei ya mafuta imefika 105 USD kwa pipa. Tanzania tutafute mafuta yetu, kuna siku tutalia na kusaga meno

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,312
8,214
Bei ya mafuta imefika 105 USD kwa pipa Tanzania tutafute mafuta Yetu.

Kufuatia Mzozo unaoendelea kati ya Ukraine na Urusi bei ya mafuta imepanda na kuvuka dola mia moja kwa mara ya kwanza tangu miaka saba iliyopita, ambapo ongezeko hilo limesababishwa na hofu baada ya mzalishaji mkubwa Urusi kufanya mashambulio nchini Ukraine. Urusi ni mzalishaji muhimu wa mafuta baada ya Saudi Arabia.
Bei ya mafuta ghafi barani Ulaya imefikia dola 105 na senti 79 kwa pipa.

Screenshot_20220225_214516.jpg



The price of oil has reached 105 USD per barrel.

Following the ongoing conflict between Ukraine and Russia oil prices have risen to more than $ 100 for the first time in the last seven years, an increase caused by panic after a major Russian producer carried out an attack in Ukraine.

Russia is the largest oil producer after Saudi Arabia. The price of crude oil in Europe has reached $ 105 and 79 cents per barrel.

Screenshot_20220225_215250.jpg


Source: ITV and CNBC
 
Ukijumlisha na TOZO, watu watapanda mwendo kasi kudadek. Wengine watarudi enzi za baiskeli.
 
Kwani huko Mtwara na Zanzibar si kuna mafuta! Kwanini yasichimbwe?
 
Kwa makadirio bei itakuwa sawa tsh ngap kwa liter
Pipa linakuwa na lita kama mia hamsini na kenda, hazizifiki 160 kama sikosei.. Sasa hapo we piga hesabu 160/105 utapata bei ya lita moja, kisha uzidisha na pesa yetu ya madafu, hapo bado hayajasafirishwa, hayajakutana na kodi(tozo) zaidi ya 16 hapa kwa mama samia suluhu..

You will know, you don't know(utajua hujui) kudadeki
 
Ni wakati sasa serikali ya Tanzania kulaani vikali kile kinachofanywa na urusi kwa nchi ya Ukraine
 
hapa Tz bei ya mafuta ikipanda watu watamlaumu rais Samia kimsingi ht huu mgogoro wa ukraine na russia walishaanza kumlaumu yeye wakaacha tu walipopewa shule kdg
 
Na hapo tembo kapigana na swala je,tembo kwa tembo wakipigana itakuwaje..?
 
Pipa linakuwa na lita kama mia hamsini na kenda, hazizifiki 160 kama sikosei.. Sasa hapo we piga hesabu 160/105 utapata bei ya lita moja, kisha uzidisha na pesa yetu ya madafu, hapo bado hayajasafirishwa, hayajakutana na kodi(tozo) zaidi ya 16 hapa kwa mama samia suluhu..

You will know, you don't know(utajua hujui) kudadeki
Kwa haraka haraka ni kama 1500TZS sasa ukiweka Nauli, tozo na mark up kwa ajili ya Faida ndio hapo sasa tutajua hatujui
 
Mafuta yetu ya Zanzibar yakianza kuchimbwa sio ya muungano, wabara mlijue hilo.
 
Tuna viongozi viazi, hawana maono, hawatizami kesho ya mtanzania zaidi ya leo ya kwao, ile gesi tusingeichezea, tukakubali kugharamaika hata kwa mkopo kufungua kiwangmda cha kubadili gesi kuwa mafuta sasa hivi tunaula kiuwepesi, ila sababu ya 10% wanatuzamisha tu.
Gesi kuwa mafuta?

Hii teknolojia ya wapi?
 
Back
Top Bottom