Bei ya mafuta duniani yaendelea kuanguka, lakini Watanzania bado wanalanguliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei ya mafuta duniani yaendelea kuanguka, lakini Watanzania bado wanalanguliwa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BAK, Dec 4, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Oil hits near 4-year low on weak economic news

  Thursday, December 4, 2008 | 7:38 AM ET

  The Associated Press

  Oil prices sank Thursday to lows last seen nearly four years ago as more bleak news from the world's largest economy reinforced speculation that crude could tumble below $40 US by the end of the year.

  After sinking more than $1 US earlier in the day to approach levels traded at in February 2005, light sweet crude was trading at $46.10 US, down 69 cents in electronic trading on the New York Mercantile Exchange by noon in Europe. The contract fell 17 cents overnight to settle at $46.79 US.

  "You could see prices testing $40 US by the end of the year because the economic data is really ugly at the moment," said Christoffer Moltke-Leth, head of sales trading at Saxo Capital Markets in Singapore.

  "Demand destruction is still very much the concern."

  Oil prices have tumbled about 69 per cent since peaking at $147.27 US in July. But trader and analyst Stephen Schork suggested that the price decline had some ways to go before bottoming out, despite the arrival of the cold season in the U.S. and elsewhere in the Western hemisphere, which traditionally drives up demand.

  "The only place colder than the [U.S.] Northeast and Midwest is the Floor of the NYMEX," he said in his Schork Report.

  Investors were dismayed at more poor economic news from the U.S. The Institute for Supply Management said Wednesday its services sector index fell to 37.3 in November from 44.4 in October. The reading was significantly lower than the 42 the market expected.

  The U.S. Labor Department reported that productivity rose at an annual rate of 1.3 per cent in the July-September quarter, down from a 3.6 per cent growth rate in the second quarter.

  Investors took little solace from a report showing U.S. crude inventories fell last week. For the week ended Nov. 28, crude inventories fell by 400,000 barrels, the Energy Department's Energy Information Administration said Wednesday.

  Analysts had expected a boost of two million barrels, according to a survey by Platts, the energy information arm of McGraw-Hill Cos.

  "People are really looking at economic figures right now and how bad a shape the world is in," Moltke-Leth said.

  The Organization of Petroleum Exporting Countries has signalled it plans to lower output quotas at a Dec. 17 meeting, adding to a production cut of 1.5 million barrels a day in October.

  But analysts are skeptical that an output reduction by OPEC can reverse the fall in the prices.

  "I don't think it will have a major impact in the near term," Moltke-Leth said. "However, low prices will increasingly lead drilling and exploration projects to be postponed or cancelled, so supply will become a concern in the medium term."

  In other Nymex trading, gasoline futures fell nearly three cents to $1.01 US a gallon. Heating oil dropped almost 2 pennies to $1.57 US a gallon while natural gas for January delivery was steady at $6.34 US per 1,000 cubic feet.

  In London, January Brent crude fell 74 cents to $44.70 US on the ICE Futures exchange.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Lipumba: Bei ya mafuta ishushwe

  na Sauli Giliard
  Tanzania Daima~Sauti ya watu

  MWENYEKITI wa Chama cha (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kutokana na bei ya mafuta kuendelea kuporomoka kila mara, Tanzania haina budi kushusha bei ya bidhaa hiyo ili kuwapunguzia wananchi ukali wa maisha.

  Mwanasiasa huyo, ambaye kitaaluma ni mchumi, aliliambia gazeti la Tanzania Daima, mwishoni mwa wiki kwamba bei ya mafuta imeshuka kwa kiasi kikubwa katika soko la dunia, jambo ambalo lilitakiwa lisababishe kushuka kwa bei ya petroli na dizeli nchini.

  Profesa Lipumba alisema kwa mwezi Julai mwaka huu, Tanzania ililazimika kupandisha bei ya mafuta kwani pipa moja iliweka historia kwa kufikia dola 147, lakini kwa sasa imeshuka kwa karibu asilimia 100, hivyo hakuna sababu ya bei ya bidhaa hiyo kubaki kuwa juu.

  Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa bidhaa hiyo imeendelea kushuka zaidi kwani hivi sasa, mafuta ghafi yanauzwa kwa dola za Marekani 40 na huenda bei hiyo ikaendelea kushuka.

  "Kwa vile bei ya mafuta imeshuka, bei ya bidhaa hiyo nchini ilipaswa kuuzwa kwa sh 1,000 hadi 1,100 tofauti na bei ya sh 1,450 hadi 1,500 inayouzwa katika vituo vingi vya mafuta nchini," alisema Lipumba.

  Lipumba aliitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), kuamka kutoka usingizini na kuhakikisha bei ya mafuta inaendana na ile ya soko.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Kikwete awabana wenye mafuta
  Gloria Tesha
  Daily News; Monday,December 08, 2008 @20:00

  Rais Jakaya Kikwete ameingilia kati suala la bei ya mafuta kwa kuitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (Ewura) iwabane wafanyabiashara wa mafuta wanaokaidi kushusha bei. Ameshangazwa na hatua ya wafanyabiashara kupandisha kwa kasi bei ya mafuta yanapopanda, lakini wakapata kigugumizi kushusha malighafi hiyo ambayo hivi sasa bei yake katika soko la dunia imeshuka.

  Kutokana na hali hiyo, amesema amemwagiza Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, awasiliane na Ewura kuwabana wafanyabiashara. Rais Kikwete alisema hayo Dar es Salaam wakati akihutubia katika Baraza la Idd el Haj ambalo alikuwa mgeni rasmi.

  "Wauza mafuta walipandisha bei kwa kasi, mbona hawateremshi kwa kasi hiyo hiyo…hapa wanaingia kigugumizi," alihoji Rais Kikwete na kuongeza kwamba kama vile walivyokuwa hodari wa kupandisha, vivyo hivyo wanapaswa kuwa hodari wa kushusha.

  Kwa mujibu wa Rais Kikwete, wakati mafuta yalipopanda bei, pipa moja liliuzwa kwenye soko la dunia dola za Marekani 147 na sasa bei imeshuka na kufikia chini ya dola 46.Ameiagiza Ewura kwenda Botswana kupata uzoefu wa jinsi wanavyoendesha biashara hiyo kutokana na nchi hiyo kuwa na mfumo mzuri wa usimamizi bei ya mafuta.


  Wakati huo huo, Rais Kikwete amesema haitawavumilia wale wote wanaochochea ghasia za kidini na amewaelekeza viongozi wa dini kuwa inapotokea wakaona haja, waiambie serikali isaidie kuingilia kati kwa lengo kudhibiti ghasia hizo. Miongoni mwa mambo ambayo Rais Kikwete aliyakemea, ni pamoja na wale wanaochochea ghasia kwa lengo la kuleta chuki baina ya dini na dini na ghasia ndani ya dini moja wakiwamo wenye kuteka misikiti.

  Awali, Katibu Mkuu wa Bakwata, Ali Mzee, aliiomba serikali kulisaidia baraza lake kukemea vitendo sugu vya uvamizi wa misikiti vinavyofanywa na baadhi ya vikundi vya Waislamu, wakidai wanaokoa mali za Waislamu na kusema vinahatarisha amani.

  Rais Kikwete alisema vitendo vya uchochezi wa ghasia havina maslahi yoyote kwa jamii, na kwamba katika mfarakano wa kuchochea chuki dhidi ya dini nyingine, hakuna anayeweza kuibuka mshindi. Akizungumza kuhusu kuwapo kwa Baraza la Waislamu wa Tanzania (Bakwata),

  Rais Kikwete alisema Waislamu wanahitaji chombo imara cha kuwaunganisha, vinginevyo kukikosa, kunatoa nafasi kwa waumini hao kuyumbishwa na hatimaye kuangukia mikono mibaya ya kushawishiwa kufanya mambo yasiyohusu Uislamu. Alisema kuwapo kwa chombo husika, kunatoa nafasi kwao kuzungumzia masuala yao ya kiroho na kimwili. Alisema wanapokosa chombo cha namna hiyo, wanakosa umoja na mshikamano.

  Rais alielezea faraja yake kusikia kwamba Bakwata inafanya matayarisho ya uchaguzi wa ngazi zote. Alisema matumaini yake ni kwamba watachagua viongozi wapenda maendeleo watakaosukuma gurudumu la maendeleo na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii. Kwa mujibu wa Kikwete, serikali itaendelea kuheshimu uhuru wa raia wa kuabudu dini wanayoipenda na itaendelea kufanya kila iwezalo kuhakikisha uhuru huo unaheshimiwa.

  Kwa upande wa maadili, alishutumu tabia ya kukumbatia desturi zisizo za Kitanzania. Alisema vitendo hivyo vinaitoa jamii katika mstari wa maadili mema, ikiwa ni pamoja na kupungua kwa maadili ya dini. Katika kile alichoeleza kuwa ni kuelekea pabaya, Rais aliwataka viongozi wa dini, wazazi na jamii kwa ujumla, kuona wajibu wao kuiongoza jamii katika maadili mema.

  Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliwatoa hofu Watanzania kwa kusema serikali itaendelea kudhibiti matumizi ya fedha na mali za umma. Aliwataka waendelee kuwa na imani na vyombo vya fedha. Alisema kila siku Gavana wa Benki Kuu (BoT) anakutana na watendaji wake kuhakikisha kwamba hali ya fedha inatengamaa.

  Kuhusu mauaji ya albino, aliwaomba viongozi wa dini kushirikiana na Serikali katika mapambano kwa kuwahubiria waumini kuwa mafanikio hayaji kwa ushirikina, bali yanategemea baraka za Mungu na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
   
 4. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Tatizo kwetu hapa ni regulatory authority, yaani EWURA hawana meno; au precisely wameingiwa virusi katika kutoa maamuzi ya kuunufaisha umma.
   
 5. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2008
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Hapa rais Kikwete ameonesha udhaifu ule ule wa kupiga kelele kama vile naye ni mwananchi wa kawaida kama sisi akina yahe.

  La msingi ni kwa national pressure groups kama oposition political parties kuchukua nafsi zao. Watoe shinikizo, waelimishe wananchi na waandae mgomo juu ya serikali (siyo petroleum companies) kwa kushindwa kustep up. Toka USD 147 kwa pipa hadi below USD 60 kwa pipa serikali inaendela kuwbembereza kwa lipi?? Serikali ina kazi gani sasa kama nayo inaendelea kubwabwaja tu???

  Chadema, CUF, UDP (vyenye wabunge) wahamasishe wananchi na waandae maandamano nchi nzima as long as watawafahamisha wananchi jinsi gani tunanyonywa. I am sure hii haitachukuliwa kama ya kisiasa bali ni ya kijamii zaidi na kunyonywa kiuchumi na wafanyabiashara wanaowekewa sheria na serikali zizizo na meno. Wa kuwajibishwa ni chama na serikali yake vilivyopewa madaraka na wananchi.
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ewura iliomba ipewe "MENO" imepewa, cha kushangaza haitumii madaraka yake kuwalinda consumers kama inavyotakiwa!! Huwezi kupanga bei za mafuta kwa kuwa na kongamano na stakeholders, Serikali inatakiwa kwa sasa iiwezesha TPDC[ shirika la petrol] ili liwe na uwezo wa kuagiza mafuta in bulk; wakifanya hivyo wao watakuwa price setters kwenye soko na wafanyabiasha wengine watashindwa kuwalangua wananchi kwani bei halali itakuwa imekwishajulikana.
   
 7. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  KWa nini mafuta yakipanda, makampuni ya mafuta yanapandisha mafuta ghafla. Lakini mafuta yakishuka,wao wanasita kushusha??

  MAfuta yana direct impact kwenye uchumi wa nchi. Gharama za uzalishaji zinapaa kama bei ya mafuta ni juu. Hapa ni kwa nini Wizara ya Fedha na uchumi isiingilie kati???

  Au kwa nini BOT isitoe tathmini ya athari za bei za mafuta?

  TPDC vipi, mbona haianzi kununua mafuta??

  Kutokana na bei ya mafuta kuwa na direct impact kwenye kila sekta. Wizara ya Biashara na Viwanda, Wizara ya Miundombinu, Wizara ya KIlimo, bei za mafuta ya ndege (utalii), Na wizara ya Nishati na madini.
  Actually inatakiwa baraza la MAwaziri likae na litoe maamuzi, sio kuwaomba walanguzi.

  Hata ikiwezekana Serikali ipunguze kodi kwenye fuel ili kuboost production, na uchumi hence serikali itajipatia kodi zaidi kutokana na uzalishaji kuongezeka. Wachumi mko wapi???

  Pia bei za Mafuta zinaleta inflation, bei za bidhaa zinapanda, gharama za maisha zinapanda.

  Kama hii haiwezekani basi, kuna mkono wa Wanasiasa waroho (mafisadi) kwenye biashara ya mafuta.

  Ewura kaa mkao wa kula, siri zote zitafichuka!!!!
   
Loading...