Bei ya kivuko cha daraja la Kigamboni zapandishwa ghafla kipindi hiki cha korona, kutoka 1500 kwa gari Dogo hadi 2000

ngichinwe

Senior Member
Oct 15, 2018
156
430
Jana wakati naenda kwenye shughuli zangu asubuhi nilivuka vizuri kwa sh 1500, ila maajabu ni wakati narudi naambiwa kwamba TRA wametoa mabadiliko ya bei kwa magari madogo na kupandisha hadi sh 2000. Kuanzia Jana trh 30/04/2020.

Nikajiuliza daraja limejengwa na Mfumo wa NSSF.iweje bei waje kupanga
Unajua wakati swala la level seat linaanza daladala za Kigamboni zilifanya mgomo ili wapunguziwe malipo.walidai kwamba kulipola sh 5000 kila gari linapopita haitowezekana tena, na kweli isingewezekana la sivyo wangekuwa hesabu nzima wanaiacha darajani.

Sasa nadhani think tank wa TRA wakakaa wakaamua kuja na wazo la kuongeza bei upande wa pili.

Hivi jamani katika kipindi choote mkaona kipindi hiki cha korona ndio mpandishe bei darajani? Nimeamini kweli hamtujali kabisa RAIA wenu.
 
Hivi hizo elfu tano za daladala ni kwa kila route yanayovuka hapo darajani au ni mara moja tu kwa siku?
 
Aiseee niliwahi kuuliza hii kitu, nikaambiwa ni kila akipita tu kwahio kwenda na kurudi ni mwekundu!
 
Gari dogo inaanzia cc ngapi mbona mimi navuka toka mwaka jana kwa hiyo hiyo 2000 gari yangu ni cc 2000.
 
Ile akiba anayojidai nayo kila siku kuwa iko bank kuu ni ya maonesho au ya kutumia wakati wa dharura kama huu?
Akili za kitoto! Ukitumia akiba Bila mikakati ya kupata nyingine na hujui corona itaisha lini si ujuha
 
Du
Aiseee niliwahi kuuliza hii kitu, nikaambiwa ni kila akipita tu kwahio kwenda na kurudi ni mwekundu!
Duh Sasa hizo daladala wanapata shilingi ngapi kwa siku Kama kila route unatoa 5000,Kama umeenda route 7 kwa siku it means elfu 35 imekatika hapo
 
Gari dogo inaanzia cc ngapi mbona mimi navuka toka mwaka jana kwa hiyo hiyo 2000 gari yangu ni cc 2000.
Mkuu gari yako ni gari gani? Issue wanayoangalia ni kama kwenye kadi inasoma STATION WAGON wewe utalipia Tshs 2000, kama gari yako inasomeka kama saloon kwenye kadi utalipia Tshs 1500.Sasa haya mabadiliko yanayo zungumziwa hapa ni kwa wamiliki wa saloon cars kuanza kutozwa Tshs 2000 badala ya bei ya awali ya Tshs 1500.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo nimekuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom