Bei ya kahawa yaanguka kwa zaidi ya asilimia 60

Njaare

JF-Expert Member
Sep 26, 2010
1,081
275
Katika msimu huu wa kuuza kahawa kanda ya kaskazini, bei ya kahawa imeshuka kutoka Tshs 5000 kwa msimu wa 2011/12 hadi Tsh 2000 kwa msimu wa mwaka 2012/13. Wakulima wengi wanalia kwa kupata hasara na wengine wanafikiria kungoa miche ya kahawa au kuitelekeza kama ilivyowahi kutokea miaka ya nyuma.

Je, Ni nini kimesababisha anguko hili? Je inahusika na kuchelewa kwa mishahara ya wafanyakazi au ni mchwa walioko ndani ya vyama vya ushirika? Au kwa sababu ya mikutano ya juzi?
 
Twahitaji kutengeneza soko letu la ndani pia tutoke nje ya nchi kama vile South Africa. Wakenya wameweza chai yao twainywa humu acha blue band.
 
Pole sana mkulima. Huku kwetu ikianguka tofauti ya bei ya ugnda na sisi ni kama 1000 tshs ,uganda wakiwa juu. Alfu serikali dhalimu insema hakuna kupeleka uganda. Kama mahindi yanazuiwa yasuzwe nje ya nchi kwa sababu ya njaa ,inakuwaje kwa mazao ya biashara?
 
tatizo la kuuza malighafi nje ya nchi matajiri wa Ulaya wanashusha bei wanavyotaka,tungekuwa na viwanda tungeuza kahawa(ambayo ipo tayari kwa kutumiwa) na kupanga bei sisi wenyewe.

kulima alime mkulima wa Tanzania bei apange mnunuzi wa Ulaya, hawa jamaa wanatuona mabwege sana.
 
kwanini vyama vya ushirika wasinunue hiyo kahawa waisindike wauze humu nchini na nchi za jirani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom